< Revelation 9 >

1 Then the fifth angel sounded his trumpet. I saw a star from heaven that had fallen to the earth. The star was given the key to the shaft of the bottomless pit. (Abyssos g12)
Kisha malaika wa tano akapiga tarumbeta yake. Nami nikaona nyota iliyokuwa imeanguka juu ya nchi kutoka mbinguni. Nayo ikapewa ufunguo wa shimo la Kuzimu. (Abyssos g12)
2 He opened the shaft of the bottomless pit, and smoke went up out of the shaft like smoke from a huge furnace. The sun and the air turned dark by the smoke pouring out of the shaft. (Abyssos g12)
Basi, nyota hiyo ikafungua shimo la Kuzimu, kukatoka moshi wa tanuru kubwa. Jua na anga vikatiwa giza kwa moshi huo wa Kuzimu. (Abyssos g12)
3 Out of the smoke locusts came on the earth, and they were given power like that of scorpions on the earth.
Nzige wakatoka katika moshi huo, wakaingia duniani wakapewa nguvu kama ya ng'e.
4 They were told not to damage the grass on the earth or any green plant or tree, but only the people who did not have the seal of God on their foreheads.
Wakaamrishwa wasiharibu nyasi za nchi wala majani wala miti yoyote, bali wawaharibu wale tu ambao hawakupigwa mhuri wa Mungu katika paji la uso.
5 They were not given permission to kill those people, but only to torture them for five months. Their agony would be like the sting of a scorpion when it strikes a person.
Nzige hao hawakuruhusiwa kuwaua watu, ila kuwatesa tu kwa muda wa miezi mitano. Maumivu watakayosababisha ni kama maumivu yanayompata mtu wakati anapoumwa na ng'e.
6 In those days people will seek death, but will not find it. They will greatly desire to die, but death will flee from them.
Muda huo watu watatafuta kifo lakini hawatakipata; watatamani kufa lakini kifo kitawakimbia.
7 The locusts looked like horses prepared for war. On their heads were something like crowns of gold, and their faces were like human faces.
Kwa kuonekana, nzige hao walikuwa kama farasi waliowekwa tayari kwa vita. Juu ya vichwa vyao walikuwa na taji zilizo kama za dhahabu, na nyuso zao zilikuwa kama za binadamu.
8 They had hair like women's hair, and their teeth were like lions' teeth.
Nywele zao zilikuwa kama nywele za wanawake, na meno yao yalikuwa kama meno ya simba.
9 They had breastplates like iron breastplates, and the sound of their wings was like the sound made by many chariots and horses running into battle.
Vifua vyao vilikuwa vimefunikwa kitu kama ngao ya chuma. Sauti ya mabawa yao ilikuwa kama sauti ya msafara wa magari ya farasi wengi wanaokimbilia vitani.
10 They had tails with stingers like scorpions; in their tails they had power to harm people for five months.
Walikuwa na mikia na miiba kama ng'e, na kwa mikia hiyo, walikuwa na nguvu ya kuwadhuru watu kwa muda wa miezi mitano.
11 They had as king over them the angel of the bottomless pit. His name in Hebrew was Abaddon, and in Greek he had the name Apollyon. (Abyssos g12)
Tena wanaye mfalme anayewatawala, naye ndiye malaika wa kuzimu; jina lake kwa Kiebrania ni Abadoni, na kwa Kigiriki ni Apolioni, yaani mwangamizi. (Abyssos g12)
12 The first woe is past. Look! After this there are still two disasters to come.
Maafa ya kwanza yamepita; bado mengine mawili yanafuata.
13 The sixth angel sounded his trumpet, and I heard a voice coming from the horns of the golden altar that is present before God.
Kisha malaika wa sita akapiga tarumbeta yake. Nami nikasikia sauti moja kutoka katika pembe nne za madhabahu ya dhahabu iliyokuwa mbele ya Mungu.
14 The voice said to the sixth angel who had the trumpet, “Release the four angels who are bound at the great Euphrates River.”
Sauti hiyo ikamwambia huyo malaika wa sita mwenye tarumbeta, “Wafungulie malaika wanne waliofungwa kwenye mto mkubwa Eufrate!”
15 The four angels who had been prepared for that hour, that day, that month, and that year, were released to kill a third of mankind.
Naye akawafungulia malaika hao wanne ambao walikuwa wametayarishwa kwa ajili ya saa hiyo ya siku ya mwezi huo, wa mwaka huohuo, kuua theluthi moja ya wanaadamu.
16 The number of the soldiers on horseback was 200,000,000. I heard their number.
Nilisikia idadi ya majeshi wapanda farasi ilikuwa milioni mia mbili.
17 This is how I saw the horses in my vision and those who rode on them: Their breastplates were fiery red, dark blue and sulfurous yellow. The heads of the horses resembled the heads of lions, and out of their mouths came fire, smoke, and sulfur.
Hivi ndivyo nilivyowaona hao farasi na wapanda farasi katika hiyo njozi: Walikuwa na ngao vifuani zilizokuwa moto mtupu, zenye rangi ya samawati na njano kama kiberiti. Vichwa vya hao farasi vilikuwa kama vya simba; na moto, moshi, na kiberiti vilikuwa vinatoka kinywani mwao.
18 A third of the people were killed by these three plagues: the fire, smoke, and sulfur that came out of their mouths.
Theluthi moja ya wanaadamu waliuawa kwa mabaa hayo matatu yaani, moto, moshi na kiberiti, yaliyokuwa yanatoka katika vinywa vyao;
19 For the power of the horses was in their mouths and in their tails—for their tails were like snakes, and they had heads with which they inflicted wounds on people.
maana nguvu ya farasi hao ilikuwa vinywani mwao na katika mikia yao. Mikia yao ilikuwa na vichwa kama nyoka, na waliitumia hiyo kuwadhuru watu.
20 The rest of mankind, those who were not killed by these plagues, did not repent of the deeds they had done, nor did they stop worshiping demons and idols of gold, silver, bronze, stone, and wood—things that cannot see, hear, or walk.
Wanaadamu wengine waliobaki ambao hawakuuawa na mabaa hayo, hawakugeuka na kuviacha vitu walivyokuwa wametengeneza kwa mikono yao wenyewe; bali wakaendelea kuabudu pepo, sanamu za dhahabu, fedha, shaba, mawe na miti, vitu ambavyo haviwezi kuona, kusikia wala kutembea.
21 Neither did they repent of their murders, their sorcery, their sexual immorality or their acts of theft.
Wala hawakutubu na kuacha kufanya mauaji, uchawi, uzinzi, na wizi.

< Revelation 9 >