< Jeremiah 24 >
1 Yahweh showed me something. Behold, two baskets of figs were placed before Yahweh's temple. (This vision happened after Nebuchadnezzar, king of Babylon, took into exile Jehoiachin son of Jehoiakim, king of Judah, the officials of Judah, the craftsmen and the metalworkers from Jerusalem and brought them to Babylon.)
Baada ya Yekonia mwana wa Yehoyakimu mfalme wa Yuda, pamoja na maafisa, mafundi stadi na wahunzi wa Yuda, kuchukuliwa kutoka Yerusalemu kwenda Babeli na Nebukadneza mfalme wa Babeli kwenda uhamishoni huko Babeli, Bwana akanionyesha vikapu viwili vya tini vilivyowekwa mbele ya Hekalu la Bwana.
2 One basket of figs was very good, like first ripe figs, but the other basket of figs was so very bad that they could not be eaten.
Kikapu kimoja kilikuwa na tini nzuri sana, kama zile za mavuno ya kwanza. Kikapu cha pili kilikuwa na tini dhaifu sana, mbovu mno zisizofaa kuliwa.
3 Yahweh said to me, “What do you see, Jeremiah?” I said, “Figs. Figs that are very good and figs that are so very bad they cannot be eaten.”
Kisha Bwana akaniuliza, “Je, Yeremia, unaona nini?” Nikamjibu, “Ninaona tini zile zilizo nzuri ni nzuri sana, lakini zilizo dhaifu ni mbovu mno zisizofaa kuliwa.”
4 Then the word of Yahweh came to me, saying,
Kisha neno la Bwana likanijia:
5 “Yahweh, God of Israel, says this: I will look on the exiles of Judah for their benefit, just like these good figs, the exiles whom I have sent out from this place to the land of Chaldea.
“Hili ndilo Bwana, Mungu wa Israeli, asemalo: ‘Kama zilivyo hizi tini nzuri, ndivyo ninavyowaona kuwa bora watu wa uhamisho kutoka Yuda, niliowaondoa kutoka mahali hapa kwenda katika nchi ya Wakaldayo.
6 I will set my eyes on them for good and restore them to this land. I will build them up, and not tear them down. I will plant them, and not uproot them.
Macho yangu yatakuwa juu yao kwa ajili ya kuwapatia mema, nami nitawarudisha tena katika nchi hii. Nitawajenga wala sitawabomoa, nitawapanda wala sitawangʼoa,
7 Then I will give them a heart to know me, for I am Yahweh. They will be my people and I will be their God, so they will turn to me with all their heart.
nitawapa moyo wa kunifahamu mimi, kwamba mimi ndimi Bwana. Watakuwa watu wangu, nami nitakuwa Mungu wao, kwa maana watanirudia kwa moyo wao wote.
8 But like the bad figs that are too bad to be eaten—this is what Yahweh says—I will act in this way with Zedekiah, king of Judah, with his officials, and with the rest of Jerusalem who remain in this land or go to stay in the land of Egypt.
“‘Lakini kama zilivyo zile tini dhaifu, ambazo ni mbovu mno zisizofaa kuliwa,’ asema Bwana, ‘ndivyo nitakavyomtendea Sedekia mfalme wa Yuda, maafisa wake na mabaki wengine kutoka Yerusalemu, wawe wamebaki katika nchi hii, au wanaishi Misri.
9 I will turn them into a frightening thing, a disaster, in the sight of all the kingdoms on earth, a disgrace and a subject for proverbs, taunts, and curses in every place where I will have driven them.
Nitawafanya kuwa chukizo kabisa na kitu cha kulaumiwa katika mataifa yote ya dunia, watakuwa aibu na kitu cha kudharauliwa, chombo cha dhihaka na kulaaniwa, popote nitakapowafukuzia.
10 I will send out sword, famine, and plague against them, until they are destroyed from the land that I gave them and their ancestors.”
Nitautuma upanga, njaa na tauni dhidi yao hadi wawe wameangamia kutoka nchi niliyowapa wao na baba zao.’”