< 2 Corinthians 6 >
1 As God's fellow workers, we urge you not to receive the grace of God in vain.
Basi, tukiwa wafanyakazi pamoja na Mungu, tunawasihi msikubali ile neema mliyopokea kutoka kwa Mungu ipotee bure.
2 For he says, “At a favorable time I listened to yoʋ, and in a day of salvation I helped yoʋ.” Behold, now is the favorable time; now is the day of salvation.
Mungu asema hivi: “Wakati wa kufaa nimekusikiliza, wakati wa wokovu nikakusaidia.” Basi, sasa ndio wakati wa kufaa, sasa ndiyo siku ya wokovu!
3 We are putting no obstacle in anyone's way, so that our ministry may not be discredited.
Kusudi tusiwe na lawama yoyote katika utumishi wetu, hatupendi kumwekea mtu yeyote kizuio chochote.
4 Rather, as servants of God we commend ourselves in every way: in great endurance, in afflictions, in hardships, in distresses,
Badala yake, tunajionyesha kuwa kweli watumishi wa Mungu kwa kila kitu: kwa uvumilivu mwingi wakati wa mateso, shida na taabu.
5 in beatings, in imprisonments, in riots, in labors, in sleepless nights, in hunger,
Tumepigwa, tumetiwa gerezani na kuzomewa hadharani; tumefanya kazi tukachoka; tumekesha na kukaa bila kula.
6 in purity, in knowledge, in patience, in kindness, in the Holy Spirit, in genuine love,
Tunajionyesha kuwa watumishi wa Mungu kwa usafi wa moyo, elimu, uvumilivu na wema; kwa Roho Mtakatifu, kwa upendo usio na unafiki,
7 in the word of truth, in the power of God; with weapons of righteousness for the right hand and the left,
kwa ujumbe wa kweli na kwa nguvu ya Mungu. Uadilifu ndiyo silaha yetu upande wa kulia na upande wa kushoto.
8 through glory and dishonor, through bad report and good report; regarded as deceivers, and yet true;
Tuko tayari kupata heshima na kudharauliwa, kulaumiwa na kusifiwa. Twadhaniwa kuwa waongo, kumbe twasema kweli;
9 as unknown, and yet well known; as dying, and behold, we live; as punished, and yet not put to death;
kama wasiojulikana, kumbe twajulikana kwa wote, kama waliokufa, lakini mwonavyo, sisi ni wazima kabisa.
10 as sorrowful, yet always rejoicing; as poor, yet making many rich; as having nothing, yet possessing everything.
Ingawa tumeadhibiwa, hatukuuawa; ingawa tunayo huzuni, twafurahi daima; ingawa tu maskini hohehahe, lakini twatajirisha watu wengi; twaonekana kuwa watu tusio na chochote, kumbe tuna kila kitu.
11 O Corinthians, we have spoken freely to you; our hearts have been opened wide.
Ndugu Wakorintho, tumezungumza nanyi kwa unyofu; mioyo yetu iko wazi kabisa.
12 You are not restricted by us, but by your own affections.
Kama mnaona kuna kizuizi chochote kile, kizuizi hicho kiko kwenu ninyi wenyewe, na si kwa upande wetu.
13 Now in return—I am speaking as I would to my own children—open your hearts to us.
Sasa nasema nanyi kama watoto wangu, wekeni mioyo yenu wazi kama nasi tulivyofanya.
14 Do not be unequally yoked with unbelievers. For what partnership is there between righteousness and lawlessness? What fellowship does light have with darkness?
Msiambatane na watu wasioamini. Je, wema na uovu vyapatana kweli? Mwanga na giza vyawezaje kukaa pamoja?
15 What harmony does Christ have with Belial? What portion does a believer have with an unbeliever?
Kristo anawezaje kupatana na Shetani? Muumini ana uhusiano gani na asiyeamini?
16 And what agreement does the temple of God have with idols? For you are the temple of the living God, just as God said, “I will dwell in them and walk among them. I will be their God, and they will be my people.
Hekalu la Mungu lina uhusiano gani na sanamu za uongo? Maana sisi ni hekalu la Mungu aliye hai. Kama Mungu mwenyewe alivyosema: “Nitafanya makao yangu kwao, na kuishi kati yao; Nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu.”
17 Therefore, come out from among them and be separate, says the Lord. Touch no unclean thing, and I will receive you.
Kwa hiyo Bwana asema pia: “Ondokeni kati yao, mkajitenge nao, msiguse kitu najisi, nami nitawapokea.
18 I will be a father to you, and you will be sons and daughters to me, says the Lord Almighty.”
Mimi nitakuwa Baba yenu, nanyi mtakuwa watoto wangu, waume kwa wake, asema Bwana Mwenye Uwezo.”