< Daniel 12 >
1 And, at that time, will Michael, the great ruler who standeth for the sons of thy people, make a stand, and there will be a time of trouble, such as never was since there was a nation, up to that time, —and, at that time, shall thy people, be delivered, every one found written in the book;
Katika kipindi hicho, Mikaeli, jemedari mkuu ambaye huwalinda watu wako, atainuka. Kutakuwa na wakati wa mateso ambao haujawahi kutokea tangu mwanzo wa taifa lolote mpaka kipindi hicho. Katika muda huo watu wako wataokolewa, yeyote ambaye jina lake litapatikana katika kitabu.
2 and, many of the sleepers in the dusty ground, shall awake, —these, [shall be] to age-abiding life, but, those, to reproach, and age-abiding abhorrence;
Na wengi wa wale waliolala katika mavumbi ya dunia watainuka. baadhi kwa uzima wa milele na baadhi kwa ajili ya fedheha na matwezo ya milele.
3 and, they who make wise, shall shine like the shining of the expanse, —and, they who bring the many to righteousness, like the stars to times age-abiding and beyond.
Wale wenye hekima watang'ara kama mng'ao wa anga la juu, na wale wenye kuwaelekeza wengine katika haki, watakuwa kama nyota milele na milele.
4 But, thou, Daniel, close up the words, and seal the book, until the time of the end, —many will run to and fro, and knowledge, shall abound.
Lakini wewe, Danieli, yafunge maneno haya; kihifadhi kitabu kikiwa kimetiwa chapa mpaka nyakati za mwisho. Watu wengi watakimbia huku na kule, na maarifa yataongezeka.
5 Then, I, Daniel, looked, and lo! two others, standing, —one on this side of the bank of the river, and one on that side of the bank of the river.
Kisha mimi, Danieli, nilitazama, na kulikuwa na malaika wengine wawili wamesimama. Mmoja alisimama katika upande huu wa ukingo wa mto, na mwingine alisimama katika ukingo wa upande mwingine wa mto.
6 And one said to the man clothed with linen, who was upon the waters of the river, How long shall be the end of the wonders?
Mmoja wao alimwambia mtu aliyevaa nguo za kitani, yeye aliyekuwa juu ya mkondo wa mto, “Je itachukua muda gani mpaka mwisho wa matukio haya ya kushangaza?”
7 And I heard the man clothed with linen who was upon the waters of the river, when he held up his right hand and his left unto the heavens, and sware by him that liveth unto times age-abiding, —For a set time and times and a half, and, when the dispersion of a part of the holy people, is brought to an end, then shall come to an end all these things.
Nilimsikia mtu yule aliyevaa nguo za kitani, aliyekuwa juu katika mkondo wa mto, aliinua mkono wake wa kuume na mkono wake wa kushoto kuelekea mbinguni na kuapa kwa yeye aishiye milele kwamba itakuwa kwa wakati, nyakati, na nusu wakati. Na wakati nguvu za watu watakatifu zitakapokuwa zimeshaharibiwa, mambo haya yote yatakuwa yamemalizika.
8 And, I, heard, but could not understand, —so I said, O my lord! what shall be the issue of these things?
Nilisikia, lakini sikufahamu. Basi nikamwuliza, “Bwana wangu, mambo haya yote yatakuwa na matokeo gani?”
9 Then said he, Go thy way, Daniel; for closed up and sealed are the words, until the time of the end.
Alisema, “Nenda zako Danieli, kwa kuwa maneno yamefungwa na kutiwa chapa mpaka wakati wa mwisho.
10 Many, will purify themselves and be made white and be refined, but the lawless, will act lawlessly, and none of the lawless, shall understand, —but, they who make wise, shall understand;
Watu wengi watakuwa wametakaswa, wameoshwa, na kusafishwa, lakini waovu wataenenda katika uovu.
11 and, from the time of the taking away of the continual [ascending-sacrifice], and the placing of the horrid abomination that astoundeth, [shall be] one thousand two hundred and ninety days.
Katika muda ule ambapo sadaka ya kawaida ya kuteketezwa itakapokuwa imeondolewa na chukizo la uharibifu liliosababisha ukiwa limesimamishwa, kutakuwa na siku zipatazo 1, 290.
12 Happy! is he that waiteth, and attaineth to one thousand three hundred and thirty-five days.
Ana heri mtu yule anayengojea mpaka mwisho wa siku 1, 335.
13 But, thou, go thy way to the end, —and thou shalt rest, and shalt rise to thy lot at the end of the days.
Unapaswa uondoke uende njia yako hata mwisho, na kisha utapumzika. Utainuka katika sehemu uliyopewa, mwishoni mwa siku.”