< Acts 20 >
1 When the uproar had ceased, Paul sent for the disciples, and, with encouraging words, said goodbye to them, and started on his journey to Macedonia.
Baada ya zile ghasia kumalizika, Paulo aliwaita wanafunzi pamoja akawatia moyo, akawaaga, akaanza safari kwenda Makedonia.
2 After going through those districts and speaking many encouraging words to the disciples, he went into Greece, where he stayed three months.
Alipita katika sehemu zile, akinena na watu maneno mengi ya kuwatia moyo. Ndipo hatimaye akawasili Uyunani,
3 He was about to sail to Syria, when he learned that a plot had been laid against him by several of the Jewish leaders; so he decided to return by way of Macedonia.
ambako alikaa kwa muda wa miezi mitatu. Alipokuwa anakaribia kuanza safari kwa njia ya bahari kwenda Shamu, kwa sababu Wayahudi walikuwa wamefanya shauri baya dhidi yake, aliamua kurudi kupitia njia ya Makedonia.
4 He was accompanied by Sopater the son of Pyrrhus, of Beroea, Aristarchus and Secundus from Thessalonica, Gaius of Derbe, and Timothy, as well as by Tychicus and Trophimus of Roman Asia.
Paulo alikuwa amefuatana na Sopatro mwana wa Piro, Mberoya, Aristarko na Sekundo kutoka Thesalonike na Gayo, mtu wa Derbe, Timotheo pamoja na Tikiko na Trofimo kutoka sehemu ya Asia.
5 These people went to Troas and waited for us there;
Hawa watu walitutangulia wakaenda kutungojea Troa.
6 while we ourselves sailed from Philippi after the Passover, and joined them five days later at Troas, where we stayed for a week.
Lakini sisi tukasafiri kwa njia ya bahari kwa siku tano kutoka Filipi baada ya siku za Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu, nasi tukaungana na wengine huko Troa, ambako tulikaa kwa siku saba.
7 On the first day of the week, when we had met for the breaking of bread, Paul, who was intending to leave the next day, began to address those who were present, and prolonged his address until midnight.
Siku ya kwanza ya juma tulikutana pamoja kwa ajili ya kumega mkate. Paulo akaongea na watu, naye kwa kuwa alikuwa amekusudia kuondoka kesho yake, aliendelea kuongea mpaka usiku wa manane.
8 There were a good many lamps in the upstairs room, where we had met;
Kwenye chumba cha ghorofani walimokuwa wamekutania kulikuwa na taa nyingi.
9 and a young man named Eutychus, sitting at the window, was gradually overcome with great drowsiness, as Paul continued his address. At last, quite overpowered by his drowsiness, he fell from the third story to the ground, and was picked up for dead.
Kijana mmoja jina lake Eutiko, alikuwa amekaa dirishani, wakati Paulo alipokuwa akihubiri kwa muda mrefu, alipatwa na usingizi mzito, akaanguka kutoka ghorofa ya tatu, wakamwinua akiwa amekufa.
10 But Paul went down, threw himself on him, and put his arms around him. “Do not be alarmed,” he said, “he is still alive.”
Paulo akashuka chini, akajitupa juu yake na kumkumbatia, akasema, “Msishtuke, uzima wake bado umo ndani yake.”
11 Then he went upstairs; and, after breaking and partaking of the bread, he talked with them at great length until daybreak, and then left.
Kisha Paulo akapanda tena ghorofani, akamega mkate na kula. Baada ya kuongea mpaka mapambazuko, akaondoka.
12 Meanwhile they had taken the boy away alive, and were greatly comforted.
Watu wakamrudisha yule kijana nyumbani akiwa hai nao wakafarijika sana.
13 We started first, went on board ship, and sailed for Assos, intending to take Paul on board there. This was by his own arrangement, as he intended to go by land himself.
Tukatangulia melini tukasafiri mpaka Aso ambako tungempakia Paulo. Alikuwa amepanga hivyo kwa maana alitaka kufika kwa miguu.
14 So, when he met us at Assos, we took him on board and went on to Mitylene.
Alipotukuta huko Aso, tulimpakia melini, tukasafiri wote mpaka Mitilene.
15 The day after we had sailed from there, we arrived off Chios, touched at Samos the following day, and the next day reached Miletus;
Kutoka huko tuliendelea kwa njia ya bahari, na kesho yake tukafika mahali panapokabili Kio. Siku iliyofuata tukavuka kwenda Samo, na kesho yake tukawasili Mileto.
16 for Paul had decided to sail past Ephesus, so as to avoid spending much time in Roman Asia. He was making haste to reach Jerusalem, if possible, by the Festival at the close of the Harvest.
Paulo alikuwa ameamua tusipitie Efeso ili asitumie muda mwingi huko sehemu za Asia, kwa sababu alikuwa anatamani kama ikiwezekana kufika Yerusalemu kabla ya siku ya Pentekoste.
17 From Miletus, however, he sent to Ephesus and invited the church elders to meet him;
Paulo akiwa Mileto, alituma mjumbe kwenda Efeso kuwaita wazee wa kanisa waje wakutane naye.
18 and, when they came, he said to them, “You know well the life that I always led among you from the very first day that I set foot in Roman Asia,
Walipofika akawaambia, “Ninyi wenyewe mnajua jinsi nilivyoishi katikati yenu muda wote tangu siku ya kwanza nilipokanyaga hapa Asia.
19 serving the Lord, as I did, in all humility, amid the tears and trials which fell to my lot through the plots of some of the Jewish leaders.
Nilimtumikia Bwana kwa unyenyekevu wote na kwa machozi nikivumilia taabu na mapingamizi yaliyonipata kutokana na hila za Wayahudi.
20 I never shrank from telling you anything that could be helpful to you, or from teaching you both in public and in private.
Mnajua kwamba sikusita kuhubiri jambo lolote ambalo lingekuwa la kuwafaa ninyi, lakini nilifundisha hadharani na nyumba kwa nyumba.
21 I earnestly pointed both Jews and Greeks to the repentance that leads to God, and to faith in Jesus, our Lord.
Nimewashuhudia Wayahudi na Wayunani kwamba inawapasa kumgeukia Mungu kwa kutubu dhambi na kumwamini Bwana wetu Yesu Kristo.
22 And now, under spiritual constraint, I am here on my way to Jerusalem, not knowing what will happen to me there,
“Nami sasa nimesukumwa na Roho, ninakwenda Yerusalemu wala sijui ni nini kitakachonipata huko.
23 except that in town after town the Holy Spirit plainly declares to me that imprisonment and troubles await me.
Ila ninachojua tu ni kwamba Roho Mtakatifu amenionya kuwa vifungo na mateso vinaningoja.
24 But I count my life of no value to myself, if only I may complete the course marked out for me, and the task that was allotted me by the Lord Jesus – which was to declare the good news of the love of God.
Lakini siyahesabu maisha yangu kuwa ya thamani kwangu, kama kuyamaliza mashindano na kukamilisha ile kazi Bwana Yesu aliyonipa, yaani, kazi ya kuishuhudia Injili ya neema ya Mungu.
25 And now, I tell you, I know that none of you will ever see my face again – you among whom I have gone about proclaiming the kingdom.
“Nami sasa najua ya kuwa hakuna hata mmoja miongoni mwenu ambaye nimemhubiria Ufalme wa Mungu katika kwenda kwangu huku na huko, atakayeniona uso tena.
26 Therefore I declare to you this day, that my conscience is clear in regard to the fate of any of you,
Kwa hiyo nawatangazia leo, sina hatia ya damu ya mtu awaye yote.
27 for I have not shrunk from announcing the whole purpose of God regarding you.
Kwa kuwa sikusita kuwatangazia mapenzi yote ya Mungu.
28 Be watchful over yourselves, and over the whole flock, of which the Holy Spirit has placed you in charge, to shepherd the church of God, which he won for himself at the cost of his life.
Jilindeni nafsi zenu na mlilinde lile kundi lote ambalo Roho Mtakatifu amewaweka ninyi kuwa waangalizi wake. Lichungeni kanisa lake Mungu alilolinunua kwa damu yake mwenyewe.
29 I know that, after my departure, merciless wolves will get in among you, who will not spare the flock;
Najua kwamba baada yangu kuondoka, mbwa mwitu wakali watakuja katikati yenu ambao hawatalihurumia kundi.
30 and from among yourselves, too, people will arise, who will teach perversions of truth, so as to draw away the disciples after them.
Hata kutoka miongoni mwenu watainuka watu na kuupotosha ukweli ili wawavute wanafunzi wawafuate.
31 Therefore, be on your guard, remembering how for three years, night and day, I never ceased, even with tears, to warn each one of you.
Hivyo jilindeni! Kumbukeni kwamba kwa miaka mitatu sikuacha kamwe kuwaonya kila mmoja kwa machozi usiku na mchana.
32 And now I commend you to the Lord and to the message of his love – a message which has the power to build up your characters, and to give you your place among all those who have become Christ’s people.
“Sasa nawakabidhi kwa Mungu na kwa neno la neema yake, linaloweza kuwajenga na kuwapa ninyi urithi miongoni mwa wote ambao wametakaswa.
33 I have never coveted anyone’s gold or silver or clothing.
Sikutamani fedha wala dhahabu wala vazi la mtu yeyote.
34 You, yourselves, know that these hands of mine provided not only for my own wants, but for my companions also.
Ninyi wenyewe mnajua kwamba mikono yangu hii imetumika kwa mahitaji yangu na ya wale waliokuwa pamoja nami.
35 I left nothing undone to show you that, laboring as I labored, you ought to help the weak, and to remember the words of the Lord Jesus, how he said himself – ‘It is more blessed to give than to receive.’”
Katika kila jambo nimewaonyesha kwamba kwa njia hii ya kufanya kazi kwa bidii imetupasa kuwasaidia wadhaifu, mkikumbuka maneno ya Bwana Yesu mwenyewe jinsi alivyosema, ‘Ni heri kutoa kuliko kupokea.’”
36 When Paul had finished speaking, he knelt down and prayed with them all.
Paulo alipomaliza kusema haya akapiga magoti pamoja nao wote akaomba.
37 All were in tears; and throwing their arms around Paul’s neck, they kissed him again and again,
Wote wakalia, wakamkumbatia Paulo na kumbusu,
38 grieving most of all over what he had said – that they would never see his face again. Then they escorted him to the ship.
Kilichowahuzunisha zaidi ni kwa sababu ya yale maneno aliyosema kwamba kamwe hawatauona uso wake tena. Wakaenda naye mpaka kwenye meli.