< Mark 9 >

1 And he said to them, Truly do I say to you, There are some of those standing here who will not taste of death, till they have seen that the kingdom of God hath come with power.
Na alisema kwao, “Hakika nasema kwenu, baadhi yenu kuna watu waliosimama hapa hawataonja mauti kabla ya kuuona ufalme wa Mungu ukija kwa nguvu.”
2 And after six days Jesus taketh with him Peter and James and John, and leadeth them up into a high mountain apart by themselves; and he was transfigured before them.
Na baada ya siku sita, Yesu aliwachukua Petro, Yakobo na Yohana pamoja naye mlimani, pekee yao. Ndipo alianza kubadilika mbele yao.
3 And his garments became glistening, very white, so as no fuller on earth can whiten.
Mavazi yake yakaanza kung'aa sana, meupe zaidi, meupe kuliko mng'arishaji yeyote duniani.
4 And there appeared to them Elijah with Moses; and they were talking with Jesus.
Ndipo Eliya pamoja na Musa walitokea mbele yao, na walikuwa wakiongea na Yesu.
5 And Peter answering saith to Jesus, Rabbi, it is good for us to be here; and let us make three tents, one for thee, and one for Moses, and one for Elijah.
Petro alijibu akamwambia Yesu, “Mwalimu, ni vyema sisi kuwa hapa, na tujenge vibanda vitatu, kimoja kwa ajili yako, kimoja kwa ajili Musa na kingine kwa ajili ya Eliya.”
6 For he knew not what to answer; for they were struck with terror.
(Kwa kuwa hakujua nini cha kusema, waliogopa sana.)
7 And there came a cloud overshadowing them; and a voice came out of the cloud, This is my beloved Son; hear him.
Wingu lilitokea na kuwafunika. Ndipo sauti ikatoka mawinguni ikisema, “Huyu ni mwanangu mpendwa. Msikieni yeye.”
8 And suddenly looking round, they no longer saw any one but Jesus alone with themselves.
Ghafla, walipokuwa wakitazama, hawakumuona yeyote pamoja nao, isipokuwa Yesu tu.
9 And as they came down from the mountain, he charged them to give no account of what they had seen to any one, till the Son of man should have risen from the dead.
Walipokuwa wanateremka kutoka mlimani, aliwaamuru kutokumwambia mtu yeyote yale yote waliyoyaona, mpaka Mwana wa Adamu atakapofufuka kutoka kwa wafu.
10 And they kept these words in mind, questioning one another what rising from the dead might mean.
Ndipo waliyatunza mambo wao wenyewe. Lakini walijadiliana wao kwa wao ni nini maana yake “kufufuliwa kutoka kwa wafu”
11 And they asked him, saying, How is it that the Pharisees and scribes say that Elijah must come first?
Walimwuliza Yesu,”Kwa nini waandishi husema lazima Eliya aje kwanza?”
12 And he said to them, Elijah cometh first, and restoreth all things. And how hath it been written of the Son of man? that he must suffer many things, and be set at nought.
Akawaambia, “hakika Eliya atakuja kwanza kuokoa vitu vyote. Kwa nini imeandikwa Mwana wa Adamu lazima apate mateso mengi na achukiwe?
13 But I say to you that Elijah hath come, and they have done to him whatever they would; as it hath been written concerning him.
Lakini nasema kwenu Eliya alikwisha kuja, na walimfanya kama walivyopenda, kama vile maandiko yasemavyo kuhusu yeye.”
14 And coming to the disciples, they saw a great multitude about them, and scribes debating with them.
Na waliporudi kwa wanafunzi, waliona kundi kubwa limewazunguka na Masadukayo walikuwa wanabishana nao.
15 And immediately the whole multitude on seeing him was struck with awe, and running to him, saluted him.
Na mara walipomwona, kundi lote lilishangaa na kumkimbilia kumsalimia.
16 And he asked them, About what are ye debating with them?
Aliwauliza wanafunzi wake, “Mnabishana nao juu ya nini?”
17 And one of the multitude answered him, Teacher, I have brought to thee my son, who hath a dumb spirit.
Mmoja wao katika kundi alimjibu, “Mwalimu, nilimleta mwanangu kwako; ana roho chafu ambayo humfanya asiweze kuongea,
18 And wherever it seizeth hold of him, it throweth him down; and he foameth and gnasheth his teeth; and he pineth away. And I spoke to thy disciples to cast it out, and they were not able.
na humsababishia kutetemeka na kumwangusha chini, na kutoka povu mdomoni na kusaga meno na kukakamaa. Niliwaomba wanafunzi wako kumtoa pepo, lakini hawakuweza.
19 He answereth and saith to them, O unbelieving generation! How long shall I be with you? How long shall I bear with you? Bring him to me.
Aliwajibu, “Kizazi kisichoamini, nitakaa nanyi kwa muda gani? Nitachukuliana nanyi hadi lini? Mleteni kwangu.”
20 And they brought him to him. And as soon as he saw him, the spirit convulsed him; and he fell on the ground, and wallowed, foaming.
Walimleta mtoto wake. Roho mchafu alipomwona Yesu, ghafla ilimtia katika kutetemeka. Mvulana alianguka chini na kutoa povu mdomoni.
21 And he asked his father, How long hath it been thus with him? And he said, From a child;
Yesu alimwuliza baba yake, “Amekuwa katika hali hii kwa muda gani?” Baba alisema, “Tangu utoto.
22 and it hath often cast him both into fire, and into water, to destroy him; but if thou art able to do any thing, have compassion on us, and help us.
Mara nyingine huanguka katika moto au kwenye maji, na kujaribu kumwangamiza. Kama unaweza kufanya chochote tuhurumie na utusaidie.”
23 Jesus said to him, If thou art able? All things are possible for him that believeth.
Yesu alimwambia, “Kama uko tayari? Kila kitu kinawezekana kwa yeyote aaminiye.”
24 The father of the child immediately cried out and said, I believe; help thou my unbelief.
Ghafla baba wa mtoto alilia na kusema, “Naamini! Nisaidie kutokuamini kwangu.”
25 And Jesus seeing that the multitude came running together, rebuked the unclean spirit, saying to it, Dumb and deaf spirit, I command thee, come out of him, and enter no more into him.
Wakati Yesu alipoona kundi linakimbilia kwao, alimkemea roho mchafu na kusema, “wewe roho bubu na kiziwi, nakuamuru mwache, usiingie kwake tena.”
26 And uttering a cry, and convulsing him much, it came out of him. And he became as one dead; so that very many said, He is dead.
Alilia kwa nguvu na kumhangaisha mtoto na roho alimtoka. Mtoto alionekana kama amekufa, Ndipo wengi walisema, “Amekufa,”
27 But Jesus, taking hold of his hand, raised him, and he stood up.
Lakini Yesu alimchukua kwa mkono akamwinua, na mtoto alisimama.
28 And when he had come into the house, his disciples asked him privately, Why could not we cast it out?
Wakati Yesu alipoingia ndani, wanafunzi wake walimwuliza faragha, “Kwa nini hatukuweza kumtoa?”
29 And he said to them, This kind can go out by nothing, except by prayer.
Aliwaambia, “kwa namna hii hatoki isipokuwa kwa maombi.”
30 And departing thence, they passed through Galilee; and he would not that any one should know it.
Walitoka pale na kupitia Galilaya. Hakutaka mtu yeyote ajue walipo,
31 For he taught his disciples, and said to them, The Son of man is about to be delivered up into the hands of men, and they will put him to death; and when he hath been put to death, after three days he will rise again.
kwa kuwa alikuwa anafundisha wanafunzi wake. Aliwaambia, “Mwana wa Adamu atafikishwa mikononi mwa watu, na watamuua. Atakapokuwa amekufa, baada ya siku tatu atafufuka tena.”
32 But they understood not what he said, and were afraid to ask him.
Lakini hawakuelewa maelezo haya, na waliogopa kumwuliza.
33 And they came to Capernaum; and having come into the house, he asked them, About what were ye disputing on the road?
Ndipo walifika Karperinaumu. Wakati akiwa ndani ya nyumba aliwauliza, ''Mlikuwa mnajadili nini njiani”?
34 But they were silent; for on the road they had been disputing with one another, who was greatest.
Lakini walikuwa kimya. Kwani walikuwa wanabishana njiani kwamba nani alikuwa mkubwa zaidi.
35 And sitting down, he called the twelve, and saith to them, If any one desire to be first, he will be last of all, and servant of all.
Alikaa chini akawaita kumi na wawili pamoja, na alisema nao, “Kama yeyote anataka kuwa wa kwanza, ni lazima awe wa mwisho na mtumishi wa wote.”
36 And he took a child, and placed him in the midst of them, and taking him in his arms, he said to them,
Alimchukua mtoto mdogo akamweka katikati yao. Akamchukua katika mikono yake, akasema,
37 Whoever receiveth one of these children in my name, receiveth me; and whoever receiveth me, receiveth not me, but him that sent me.
“Yeyote ampokeaye mtoto kama huyu kwa jina langu, pia amenipokea mimi, na ikiwa mtu amenipokea, hanipokei mimi tu, lakini pia aliyenituma.”
38 John said to him, Teacher, we saw one casting out demons in thy name who followeth not us; and we forbade him, because he did not follow us.
Yohana alimwambia, “Mwalimu tulimwona mtu anatoa pepo kwa jina lako na tukamzuia, kwa sababu hatufuati.”
39 But Jesus said, Forbid him not. For no one, who shall do a miracle in my name, can readily speak evil of me.
Lakini Yesu alisema, “Msimzuie, kwa kuwa hakuna atakayefanya kazi kubwa kwa jina langu na ndipo baadaye aseme neno baya lolote juu yangu.
40 For he that is not against us is for us.
Yeyote asiyekuwa kinyume nasi yuko upande wetu.
41 For whoever shall give you a cup of water to drink in my name, because ye belong to Christ, truly do I say to you, he will not lose his reward.
Yeyote atakayekupa kikombe cha maji ya kunywa kwa sababu uko na Kristo, kweli nawaambia, hatapoteza thawabu yake.
42 And whoever shall cause one of these little ones that believe to fall away, it would be better for him to have a great millstone hung round his neck, and be cast into the sea.
Yeyote anayewakosesha hawa wadogo waniaminio mimi, ingekuwa vyema kwake kufungiwa jiwe la kusagia shingoni na kutupwa baharini.
43 And if thy hand cause thee to fall away, cut it off. It is better for thee to enter into life maimed, than having the two hands to go away into hell, into the fire that is unquenchable. (Geenna g1067)
Kama mkono wako ukikukosesha ukate. Ni heri kuingia katika uzima bila mkono kuliko kuingia kwenye hukumu ukiwa na mikono yote. Katika moto “usiozimika”. (Geenna g1067)
(Zingatia: Mstari hii, “Mahali ambapo funza hawafi na moto usiozimika.” haumo katika nakala za kale).
45 And if thy foot is causing thee to fall away, cut it off; it is better for thee to enter into life lame, than having the two feet to be cast into hell. (Geenna g1067)
Kama mguu wako ukikukosesha, ukate. Ni vyema kwako kuingia uzimani ukiwa kilema, kuliko kutupwa hukumuni na miguu miwili. (Geenna g1067)
(Zingatia: Mstari huu, “Mahali ambapo funza hawafi na moto usioweza kuzimika” haumo kwenye nakala za kale).
47 And if thine eye is causing thee to fall away, pluck it out; it is better for thee to enter into the kingdom of God with one eye, than having two eyes to be cast into hell, (Geenna g1067)
Kama jicho lako likikukosesha ling'oe. Ni vyema kwako kuingia katika Ufalme wa Mungu ukiwa na jicho moja, kuliko kuwa na macho mawili na kutupwa kuzimu. (Geenna g1067)
48 where their worm dieth not, and the fire is not quenched.
Mahali palipo na funza wasiokufa, na moto usiozimika.
49 For every one will be salted with fire.
Kwa kuwa kila mmoja atakolezwa na moto.
50 Salt is good; but if the salt have lost its saltness, wherewith will ye season it? Have salt in yourselves, and be at peace with one another.
Chumvi ni nzuri, kama chumvi ikipoteza ladha yake, utaifanyaje iwe na ladha yake tena? Muwe na chumvi miongoni mwenu wenyewe, na muwe na amani kwa kila mmoja.”

< Mark 9 >