< Jude 1 >
1 Jude, a servant of Jesus Christ, and brother of James, to the called, loved in God the Father and kept by Jesus Christ:
Yuda, mtumwa wa Yesu Kristo, na ndugu yake Yakobo, kwa wale ambao wameitwa, wapendwao katika Mungu Baba, na waliotunzwa kwa ajili ya Yesu Kristo:
2 Mercy and peace and love be multiplied to you.
rehema na amani na upendo viongezwe kwenu.
3 Beloved, while giving all diligence to write to you, I found it necessary to write to you concerning the common salvation, exhorting you to contend earnestly for the faith which was once delivered to the saints.
Wapenzi, wakati nilipokuwa nikifanya kila juhudi kuwaandikia ninyi kuhusu wokovu wetu sote, ilinilazimu kuwaandikia kwa ajili ya kuwashauri ili mshindanie kwa uaminifu imani ambayo ilikuwa imekabidhiwa mara moja tu kwa waamini.
4 For there have stealthily crept in certain men who were of old appointed beforehand for this condemnation, ungodly men, turning the grace of our God into wantonness, and denying the only Sovereign, and our Lord Jesus Christ.
Kwa sababu watu fulani wamejiingiza kwa siri kati yenu - watu ambao walitiwa alama kwa ajili ya hukumu - watu wasio wataua ambao hubadili neema ya Mungu wetu kuwa ufisadi, na kumkana Bwana wetu pekee na Bwana Yesu Kristo.
5 But I wish to remind you as once knowing it all, that the Lord, having saved the people out of the land of Egypt, afterward destroyed those who believed not;
Sasa napenda kuwakumbusha ninyi ingawa kuna wakati mlijua kwa ukamilifu kwamba Bwana aliwaokoa watu kutoka nchi ya Misri, lakini baadaye kuwaangamiza wale ambao hawakuamini.
6 and the angels which kept not their principality, but left their own dwelling-place, he hath kept in everlasting chains under darkness unto the judgment of the great day; (aïdios )
Na malaika ambao hawakuilinda enzi yao wenyewe lakini wakaacha makao yao maalum Mungu amewaweka katika minyororo ya milele, ndani ya giza, kwa ajili ya hukumu ya siku ile kuu. (aïdios )
7 even as Sodom and Gomorrah, and the cities about them, in like manner with them giving themselves over to fornication, and going away after strange flesh, are set forth for an example, suffering the vengeance of everlasting fire. (aiōnios )
Kama vile Sodoma na Gomora na miji iliyoizunguka, ambayo pia ilijiingiza yenyewe katika uasherati na wakafuata tamaa isiyo ya asili. Walioneshwa kama mifano ya wale ambao huteseka katika hukumu ya moto wa milele. (aiōnios )
8 Yet in like manner these dreamers defile the flesh, despise dominion, and rail at dignities.
Hali kadhalika, kwa njia ile ile waota ndoto hawa pia huchafua miili yao, na hukataa mamlaka, na wananena uongo dhidi ya mtukufu.
9 Yet Michael the archangel, when contending with the Devil he disputed about the body of Moses, dared not bring against him a railing accusation, but said: The Lord rebuke thee.
Lakini hata Mikaeli malaika mkuu, wakati alipokuwa akishindana na ibilisi na kuhojiana naye kwa ajili ya mwili wa Musa, hakuthubutu kuleta hukumu ya uongo dhidi yake, lakini badala yake alisema, “Bwana akukemee!”
10 But these rail at the things which they know not; but what things they understand naturally, as brute beasts, in these they corrupt themselves.
Lakini watu hawa huleta uongo dhidi ya chochote wasicho kifahamu. Na kile wasicho kifahamu- kile ambacho wanyama wasio na akili hujua kwa silika- haya ndiyo yaliyo waharibu.
11 Woe to them! for they have gone in the way of Cain, and rushed on in the error of Balaam for reward, and perished in the gainsaying of Korah.
Ole wao! Kwa kuwa wametembea katika njia ya Kaini, na kulifuata kosa la Balaamu. Wameangamia katika uasi wa Kora.
12 These are the rocks in your feasts of love, feasting together without fear, feeding only themselves; clouds without water, carried away by winds; trees in late autumn, without fruit, twice dead, plucked up by the roots;
Hawa ni miamba katika sherehe zenu za upendo, wakisherehekea bila aibu, wakijilisha tu wenyewe. Ni mawingu yasiyo na maji, yanayobebwa na upepo, ni miti iliyopukutika isiyo na matunda iliyo kufa mara mbili, iliyong'olewa mizizi
13 raging waves of the sea, foaming out their own shame; wandering stars, for whom is reserved the blackness of darkness for ever. (aiōn )
Ni mawimbi ya bahari yenye kelele yakitoa aibu yao wenyewe, Ni nyota zinazorandaranda ambazo weusi wa giza umetunzwa kwa ajili yao milele. (aiōn )
14 Yea, and against these Enoch, the seventh from Adam, prophesied, saying, “Behold, the Lord cometh in the midst of his holy myriads,
Enoko, wa saba katika orodha ya Adamu, alitabiri kuhusu wao, akisema, “Tazama! Bwana anakuja na maelfu kwa maelfu ya watakatifu wake,
15 to execute judgment upon all, and to convict all the ungodly among them of all the deeds of their ungodliness which they committed; and of all the hard things which ungodly sinners spoke against him.”
ili afanye hukumu juu ya kila mtu, na kutia hatia wote wasiomcha Mungu juu ya matendo yao yote waliyokwishafanya katika njia zisizo za kitauwa, na kwa maneno yote ya ukali ambayo wasio watauwa wameyanena dhidi yake.”
16 These are murmurers, complaining of their lot, walking according to their own lusts; and their mouth speaketh great swelling words; admiring men's persons, for the sake of profit.
Hawa ni wale wanung'unikao, walalamikao ambao hufuata tamaa zao za uovu, wajivunao mno, ambao kwa faida yao hudanganya wengine.
17 But do ye, beloved, remember the words which were before spoken by the apostles of our Lord Jesus Christ;
Lakini ninyi, wapenzi, kumbukeni maneno ambayo yalinenwa zamani na mitume wa Bwana Yesu Kristo.
18 that they told you that at the last time there would be scoffers, walking according to their own ungodly lusts.
Walisema kwenu, “Katika wakati wa mwisho kutakuwa na watu wanaodhihaki ambao hufuata tamaa zao zisizo za kitauwa.”
19 These are they that separate themselves, sensual, not having the Spirit.
Watu hawa ni watenganishaji, wanatawaliwa na tamaa za asili, na hawana Roho.
20 But do ye, beloved, building up yourselves on your most holy faith, praying in the Holy Spirit,
Lakini ninyi, wapenzi, kama mjijengavyo katika imani yenu takatifu sana, na kama muombavyo katika Roho Mtakatifu,
21 keep yourselves in the love of God, looking for the mercy of our Lord Jesus Christ unto eternal life. (aiōnios )
jitunzeni katika upendo wa Mungu, na msubiri rehema ya Bwana wetu Yesu Kristo ambayo huwapatia uzima wa milele. (aiōnios )
22 And some rebuke when they contend; and others save, snatching them out of the fire; and on others have compassion
Onesheni rehema kwa wale walio na shaka.
23 with fear, hating even the garment spotted by the flesh.
Waokoeni wengine kwa kuwanyakua kutoka katika moto. Kwa wengine onesheni huruma kwa hofu, mkichukia hata vazi lililotiwa doa na mwili.
24 But to him that is able to keep them from falling, and to present them faultless before the presence of his glory with exceeding joy,
Sasa kwake awezaye kuwalinda msijikwae, na kuwasababisha msimame mbele ya utukufu wake, bila mawaa na kuwa na furaha kuu,
25 to the only God our Saviour, through Jesus Christ our Lord, is glory, majesty, dominion and power, before all time, and now, and for ever. Amen. (aiōn )
kwake Mungu pekee mwokozi kupitia Yesu Kristo Bwana wetu, utukufu uwe kwake, ukuu, uwezo na nguvu kabla ya nyakati zote, na sasa na hata milele. Amina. (aiōn )