< Hebrews 9 >
1 The first covenant, then, had indeed ordinances of religious service, and a worldly sanctuary.
Sasa hata agano la kwanza lilikuwa na sehemu ya ibada hapa duniani na taratibu za ibada.
2 For a tabernacle was prepared, the first, wherein was the candlestick, and the table, and the show-bread; which is called the holy place:
Kwani katika hema kulikuwa na chumba kimeandaliwa, chumba cha nje, paliitwa mahali patakatifu. Katika eneo hili palikuwa na kinara cha taa, meza na mikate ya wonyesho.
3 and after the second veil, the tabernacle which is called the holy of holies,
Na nyuma ya pazia la pili kulikuwa na chumba kingine, paliitwa mahali patakatifu zaidi.
4 which had the golden altar of incense, and the ark of the covenant overlaid on every side with gold, wherein was the golden pot containing the manna, and the rod of Aaron which budded, and the tables of the covenant;
Mlikuwemo madhabahu ya dhahabu kwa kuvukizia uvumba. Pia mlikuwemo sanduku la agano, ambalo lilikuwa limejengwa kwa dhahabu tupu. Ndani yake kulikuwa na bakuli la dhahabu lenye manna, fimbo ya Haruni iliyoota majani, na zile mbao za mawe za agano.
5 and over it the cherubs of glory, overshadowing the mercy-seat; of which we cannot now speak particularly.
Juu ya sanduku la agano maumbo ya maserafi wa utukufu wafunika mabawa yao mbele ya kiti cha upatanisho, ambacho kwa sasa hatuwezi kuelezea kwa kina.
6 Now these things being thus prepared, into the first tabernacle indeed the priests enter at all times, performing the services;
Baada ya vitu hivi kuwa vimekwisha andaliwa, Makuhani kawaida huingia chumba cha nje cha hema kutoa huduma zao.
7 but into the second the high-priest alone once every year, not without blood, which he offereth for himself, and for the errors of the people;
Lakini kuhani mkuu huingia kile chumba cha pili pekee mara moja kila mwaka, na pasipo kuacha kutoa dhabihu kwa ajili yake binafsi, na kwa dhambi za watu walizozitenda pasipo kukusudia.
8 the Holy Spirit clearly showing this, that the way into the sanctuary hath not yet been made manifest, while the first tabernacle is yet standing:
Roho Mtakatifu anashuhudia kwamba, njia ya mahali patakatifu zaidi bado haijafunuliwa kwa vile ile hema la kwanza bado linasimama.
9 which is a figure for the present time, in accordance with which are offered both gifts and sacrifices, which have no power as to the conscience to perfect the worshipper,
Hili ni kielelezo cha muda huu wa sasa. Vyote zawadi na dhabihu ambavyo vinatolewa sasa haviwezi kukamilisha dhamiri ya anayeabudu.
10 being only ordinances pertaining to the flesh, which in addition to meats and drinks and divers washings are imposed until the time of reformation.
Ni vyakula na vinywaji pekee vimeunganishwa katika namna ya taratibu za ibada ya kujiosha. Vyote hivi vilikuwa taratibu za kimwili vilivyokuwa vimeandaliwa hadi ije amri mpya itakayowekwa mahali pake.
11 But Christ having appeared, as a high-priest of the good things to come, passing through the greater and more perfect tabernacle, not made with hands, that is, not of this creation, entered once for all into the sanctuary,
Kristo alikuja kama kuhani mkuu wa mambo mazuri ambayo yamekuja. kupitia ukuu na ukamilifu wa hema kuu ambayo haikufanywa na mikono ya watu, ambayo si wa ulimwengu huu ulioumbwa.
12 not with the blood of goats and calves, but by his own blood, and obtained for us everlasting redemption. (aiōnios )
Ilikuwa si kwa damu ya mbuzi na ndama, bali kwa damu yake mwenyewe kwamba Kristo aliingia mahali patakatifu zaidi mara moja kwa kila mmoja na kutuhakikishia ukombozi wetu wa milele. (aiōnios )
13 For if the blood of goats and bulls, and the ashes of a heifer sprinkling those who have been defiled, sanctify to the purifying of the flesh,
Kama kwa damu ya mbuzi na mafahari na kunyunyiziwa kwa majivu ya ndama katika hao wasiosafi walitengwa kwa Mungu na kufanya miili yao safi,
14 how much more shall the blood of Christ, who by his everlasting spirit offered himself without spot to God, purify your conscience from dead works, for the worship of the living God! (aiōnios )
Je si zaidi sana damu ya Kristo ambaye kupitia Roho wa milele alijitoa mwenyewe bila mawaa kwa Mungu, kuosha dhamiri zetu kutoka matendo mafu kumtumikia Mungu aliye hai? (aiōnios )
15 And for this cause he is the mediator of a new covenant, that, death having taken place for redemption from the transgressions under the first covenant, they who have been called may receive the everlasting inheritance which was promised. (aiōnios )
Kwa sababu hiyo, Kristo ni mjumbe wa agano jipya. Hii ndiyo sababu mauti imewaacha huru wote walio wa agano la kwanza kutoka katika hatia ya dhambi zao, ili kwamba wote walioitwa na Mungu waweze kupokea ahadi ya urithi wao wa milele. (aiōnios )
16 For where there is a testament there must of necessity be implied the death of the testator;
Kama kuna agano linadumu, ni lazima kuthibitishwa kwa kifo cha mtu yule aliyelifanya.
17 for a testament is of force after men are dead, since it is of no force while the testator is living.
Kwani agano linakuwa na nguvu mahali kunatokea mauti, kwa sababu hakuna nguvu wakati mwenye kulifanya akiwa anaishi.
18 Hence neither was the first covenant ratified without blood.
Hivyo hata si lile agano la kwanza lilikuwa limewekwa pasipo damu.
19 For when Moses had spoken every precept according to the Law to all the people, he took the blood of the calves and of the goats, with water, and scarlet wool, and hyssop, and sprinkled both the book itself and all the people,
Wakati Musa alipokuwa ametoa kila agizo la sheria kwa watu wote, alichukua damu ya ng'ombe na mbuzi, pamoja na maji, kitambaa chekundu, na hisopo, na kuwanyunyizia gombo lenyewe na watu wote.
20 saying, “This is the blood of the covenant which God enjoined in respect to you.”
Kisha alisema, “Hii ni damu ya agano ambayo Mungu amewapa amri kwenu”.
21 The tabernacle also and all the vessels of the service he in like manner sprinkled with the blood.
Katika hali ileile, aliinyunyiza damu juu ya hema na vyombo vyote vilivyotumiwa kwa huduma ya ukuhani.
22 And almost all things are according to the Law purified with blood, and without shedding of blood there is no remission.
Na kulingana na sheria, karibu kila kitu kinatakaswa kwa damu. Pasipo kumwaga damu hakuna msamaha.
23 It was necessary therefore that the copies of the things in the heavens should be purified with these; but the heavenly things themselves with sacrifices better than these.
Kwa hiyo ilikuwa lazima kwamba nakala za vitu vya mbinguni sharti visafishwe kwa hii dhabihu ya wanyama. Hata hivyo, vitu vya mbinguni vyenyewe vilipaswa kusafishwa kwa dhabihu iliyo bora zaidi.
24 For Christ did not enter into a sanctuary made with hands, which is only a copy of the true one, but into heaven itself, now to appear in the presence of God in our behalf.
Kwani Kristo hakuingia mahali patakatifu sana palipofanywa na mikono, ambayo ni nakala ya kitu halisi. Badala yake aliingia mbingu yenyewe, mahali ambapo sasa yuko mbele za uso wa Mungu kwa ajili yetu.
25 Nor yet to make an offering of himself many times, as the high-priest entereth into the holy place every year with blood of others;
Hakuingia kule kwa ajili ya kujitoa sadaka kwa ajili yake mara kwa mara, kama afanyavyo kuhani mkuu, ambaye huingia mahali patakatifu zaidi mwaka baada ya mwaka pamoja na damu ya mwingine,
26 for then must he have suffered many times since the foundation of the world; but now once in the end of the world he hath appeared, to put away sin by means of his sacrifice. (aiōn )
kama hiyo ilikuwa kweli, basi ingekuwa lazima kwake kuteswa mara nyingi zaidi tangu mwanzo wa ulimwengu. Lakini sasa ni mara moja hadi mwisho wa miaka aliyojifunua kuiondoa dhambi kwa dhabihu yake mwenyewe. (aiōn )
27 And as it is appointed to men once to die, but after this the judgment;
Kama ilivyo kwa kila mtu kufa mara moja, na baada ya hiyo huja hukumu,
28 so also Christ having been once offered up to bear the sins of many, will appear the second time, without sin, for the salvation of those who are waiting for him.
ndivyo hivyo Kristo naye ambaye alitolewa mara moja kuziondoa dhambi za wengi, atatokea mara ya pili, si kwa kusudi la kushughulikia dhambi, bali kwa ukombozi kwa wale wamgojeao kwa saburi.