< Colossians 1 >

1 Paul, an apostle of Christ Jesus by the will of God, and Timothy the brother,
Mimi Paulo, mtume wa Kristo Yesu kwa mapenzi ya Mungu, na ndugu Timotheo,
2 to the saints and faithful brethren in Christ at Colossae: Grace be to you, and peace, from God our Father.
tunawaandikia ninyi watu wa Mungu huko Kolosai, ndugu zetu waaminifu katika kuungana na Kristo. Tunawatakieni neema na amani kutoka kwa Mungu Baba yetu.
3 We give thanks to God, the Father of our Lord Jesus Christ, praying always for you,
Daima tunamshukuru Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, wakati tunapowaombea.
4 since we heard of your faith in Christ Jesus, and of the love which ye have to all the saints,
Maana tumesikia juu ya imani yenu katika Kristo Yesu na juu ya upendo wenu kwa watu wote wa Mungu.
5 on account of the hope which is laid up for you in the heavens, of which ye heard before in the word of the truth of the gospel,
Wakati ujumbe ule wa kweli, yaani Habari Njema, ilipowafikieni kwa mara ya kwanza, mlipata kusikia juu ya lile tumaini linalopatikana kwake. Kwa sababu hiyo imani na upendo wenu vinategemea jambo lile mnalotumainia ambalo mmewekewa salama mbinguni.
6 which is come to you, as it is in all the world, and is bearing fruit and growing, as it doth also in you, from the day ye heard it, and knew the grace of God in truth;
Habari Njema inazidi kuzaa matunda na kuenea ulimwenguni kote kama vile ilivyofanya kwenu ninyi tangu siku ile mliposikia juu ya neema ya Mungu na kuitambua ilivyo kweli.
7 even as ye learned from Epaphras our beloved fellow-servant, who is a faithful minister of Christ on your behalf;
Mlijifunza juu ya neema ya Mungu kutoka kwa Epafra, mtumishi mwenzetu, ambaye ni mfanyakazi mwaminifu wa Kristo kwa niaba yetu.
8 who also brought to our knowledge your love in the Spirit.
Yeye alitupa habari za upendo wenu mliojaliwa na Roho.
9 On this account we also, from the day we heard of it, cease not to pray for you, and to ask that ye may be filled with the knowledge of his will in all wisdom and spiritual understanding;
Kwa sababu hiyo tumekuwa tukiwaombeeni daima tangu tulipopata habari zenu. Tunamwomba Mungu awajazeni ujuzi kamili wa mapenzi yake, awajazeni hekima yote na elimu iletwayo na Roho wake.
10 that ye may walk worthily of the Lord so as to please him in all things, bearing fruit in every good work, and increasing in the knowledge of God;
Hapo mtaweza kuishi kama anavyotaka Bwana na kutenda daima yanayompendeza. Maisha yenu yatakuwa yenye matunda ya kila namna ya matendo mema na mtazidi kukua katika kumjua Mungu.
11 endued with all power according to the might of his glory unto all patience and long-suffering with joy;
Mungu awajalieni nguvu kwa uwezo wake mtukufu ili mweze kustahimili kila kitu kwa uvumilivu.
12 giving thanks to the Father, who enabled us to share in the inheritance of the saints in the light;
Na kwa furaha, mshukuruni Baba aliyewawezesha ninyi kuwa na sehemu yenu katika mambo yale Mungu aliyowawekea watu wake katika utawala wa mwanga.
13 who rescued us from the empire of darkness, and transferred us into the kingdom of his beloved Son;
Yeye alituokoa katika nguvu ya giza, akatuleta salama katika ufalme wa Mwanae mpenzi,
14 in whom we have our redemption, the forgiveness of our sins; —
ambaye kwa njia yake tunakombolewa, yaani dhambi zetu zinaondolewa.
15 who is the image of the invisible God, the first-born of the whole creation;
Kristo ni mfano wa Mungu asiyeonekana; ni mzaliwa wa kwanza wa viumbe vyote.
16 for in him were created all things, those in the heavens, and those on the earth, the visible and the invisible, whether thrones, or dominions, or principalities, or powers, all things have been created through him and for him;
Maana kwa njia yake vitu vyote viliumbwa duniani na mbinguni, vitu vinavyoonekana na visivyoonekana: wenye enzi, watawala, wakuu na wenye mamlaka. Vyote viliumbwa kwa njia yake na kwa ajili yake.
17 and he is before all things, and in him all things subsist.
Kristo alikuwako kabla ya vitu vyote; kwa kuungana naye, vyote vyadumu mahali pake.
18 And he is the head of the body, the church; since he is the beginning, the first-born from the dead, that he may be in all things pre-eminent;
Yeye ni kichwa cha mwili wake, yaani kanisa; yeye ni chanzo cha uhai wa huo mwili. Yeye ndiye mwanzo, mzaliwa wa kwanza aliyefufuliwa kutoka wafu, ili awe na nafasi ya kwanza katika vitu vyote.
19 for God was pleased that in him all the fullness should dwell, and by him to reconcile all things to himself,
Maana Mungu alipenda utimilifu wote uwe ndani yake.
20 having made peace through the blood of his cross, by him, I say, whether the things on earth, or those in the heavens.
Kwa njia yake Mungu alivipatanisha naye vitu vyote naam, viumbe vyote mbinguni na duniania; alileta amani kwa damu ya Kristo msalabani.
21 And you, that were once alienated, and enemies in your mind in wicked works, yet now hath he reconciled
Hapo kwanza ninyi pia mlikuwa mbali na Mungu na mlikuwa adui zake kwa sababu ya fikira zenu na matendo yenu maovu.
22 in the body of his flesh through his death, to present you holy and blameless and irreproachable in his sight;
Lakini sasa, kwa kifo cha Mwanae aliyeishi hapa duniani, Mungu amewapatanisha naye, kusudi awalete mbele yake mkiwa watakatifu, safi na bila lawama.
23 if ye indeed continue in the faith grounded and settled, and not moved away from the hope of the gospel, which ye heard, which hath been preached in the whole creation under heaven; of which I Paul became a minister.
Mnapaswa, lakini kuendelea kuwa imara na thabiti katika imani hiyo, na msikubali kusukumwa mbali na tumaini lile mlilopata wakati mlipoisikia Habari Njema. Mimi Paulo nimekuwa mtumishi wa hiyo Habari Njema ambayo imekwisha hubiriwa kila kiumbe duniani.
24 Now I rejoice in my sufferings for you, and fill up instead that which is wanting of the afflictions of Christ in my flesh on behalf of his body, which is the church;
Na sasa nafurahi kuteseka kwa ajili yenu, maana kwa mateso yangu hapa duniani, nasaidia kukamilisha kile kilichopungua bado katika mateso ya Kristo kwa ajili ya mwili wake, yaani kanisa.
25 of which I became a minister, according to the stewardship which God entrusted to me, for you, to fulfill the word of God,
Nami nimefanywa kuwa mtumishi wa kanisa kufuatana na mpango wake Mungu ambao alinikabidhi kwa faida yenu. Mpango wenyewe ni kuutangaza kwa ukamilifu ujumbe wake,
26 the mystery which hath been hidden for ages and generations, but hath been now revealed to his saints; (aiōn g165)
ambao ni siri aliyowaficha binadamu wote tangu milele, lakini sasa amewajulisha watu wake. (aiōn g165)
27 to whom it was the will of God to make known what is the riches of the glory of this mystery among the gentiles, which is Christ in you, the hope of glory;
Mpango wa Mungu ni kuwajulisha watu wake siri hii kuu na tukufu ambayo ni kwa ajili ya watu wote. Na, siri yenyewe ndiyo hii: Kristo yuko ndani yenu, na jambo hilo lamaanisha kwamba ninyi mtaushiriki utukufu wa Mungu.
28 whom we preach, warning every man, and teaching every man in all wisdom, that we may present every man perfect in Christ;
Kwa sababu hiyo tunamhubiri Kristo kwa watu wote; tunawaonya na kuwafundisha wote kwa hekima yote, ili tuweze kumleta kila mmoja mbele ya Mungu akiwa amekomaa katika kuungana na Kristo.
29 to which end I also am laboring, striving earnestly through his working, which worketh within me mightily.
Kwa madhumuni hayo mimi nafanya kazi na kujitahidi nikiitumia nguvu kuu ya Kristo ifanyayo kazi ndani yangu.

< Colossians 1 >