< 1 Thessalonians 2 >
1 For ye yourselves know, brethren, that our coming among you hath not been in vain;
Ndugu, ninyi wenyewe mnafahamu kwamba ziara yetu kwenu haikuwa bure.
2 but after we had suffered before and had been shamefully treated, as ye know, at Philippi, we were bold in our God to speak to you the gospel of God in much conflict.
Mnajua jinsi tulivyodhulumiwa na kutukanwa kule Filipi kabla ya kufika kwenu Thesalonike. Ingawa kulikuwa na upinzani mwingi, Mungu wetu alitujalia uhodari wa kuwahubirieni Habari Njema yake.
3 For our teaching is not from error, nor from impurity, nor in guile;
Jambo tunalosisitiza kwenu si jambo linalotegemea uongo au nia mbaya; wala hatupendi kumdanganya mtu yeyote.
4 but as we have been regarded by God as worthy to be intrusted with the gospel, so we speak, not as pleasing men, but God, who trieth our hearts.
Sisi twanena daima kama atakavyo Mungu kwani yeye alituona kwamba tunafaa, akatukabidhi hii Habari Njema. Si nia yetu kuwapendeza watu hata kidogo, bali twataka kumpendeza Mungu ambaye anajua mioyo yetu mpaka ndani.
5 For neither at any time did we use flattering words, as ye know, nor a cloak of covetousness, God is witness;
Ninyi mnajua kwamba sisi hatukuja kwenu na maneno matamu ya kubembeleza wala hatukutumia maneno ya kijanja ya kuficha ubinafsi fulani; Mungu ni shahidi!
6 nor from men sought we glory, either from you, or from others; though we might have used authority as apostles of Christ.
Hatukutafuta sifa kutoka kwa watu, wala kutoka kwenu, wala kutoka kwa mtu yeyote,
7 But we were gentle in the midst of you, even as a nurse cherisheth her own children;
ingawa sisi tukiwa mitume wa Kristo, tungeweza kudai mambo fulani kwenu. Lakini sisi tulikuwa Wapole kati yenu kama alivyo mama kwa watoto wake.
8 so having a strong affection for you, we were willing to impart to you, not only the gospel of God, but also our own souls, because ye became dear to us.
Tuliwapenda ninyi sana hata tukawa tayari kuwashirikisha si tu Habari Njema ya Mungu, bali pia na maisha yetu. Ndivyo mlivyokuwa wapenzi wetu!
9 For ye remember, brethren, our labor and toil, how laboring night and day, that we might not be burdensome to any of you, we preached to you the gospel of God.
Ndugu, mnakumbuka jinsi tulivyofanya kazi na kutaabika. Tulipowaleteeni Habari Njema ya Mungu tulifanya kazi mchana na usiku kusudi tusiwe mzigo kwa mtu yeyote miongoni mwenu.
10 Ye are witnesses, and so is God, how holily, and righteously, and unblamably we conducted ourselves toward you that believe;
Ninyi mnaweza kushuhudia, na Mungu pia ni shahidi, jinsi mwenendo wetu kati yenu ninyi mnaoamini ulivyokuwa mzuri, mwadilifu na usio na lawama.
11 as ye know how we exhorted, and encouraged, and charged every one of you, as a father doth his children,
Mnajua kwamba sisi tulimtendea kila mmoja wenu kama vile baba anavyowatendea watoto wake mwenyewe.
12 that ye should walk in a manner worthy of God, who is calling you to his own kingdom and glory.
Tuliwapeni moyo, tuliwafarijini na kuwahimiza ili mpate kuishi maisha yampendezayo Mungu ambaye aliwaiteni mshiriki Utawala na utukufu wake.
13 And for this cause we also thank God without ceasing, that, when ye received the word of God which ye heard from us, ye received it not as the word of men, but, as it is in truth, the word of God, which also is powerfully working in you that believe.
Tena tunayo sababu nyingine ya kumshukuru Mungu: tulipowaleteeni ujumbe wa Mungu, ninyi mliusikia mkaupokea, si kama vile ujumbe wa binadamu, bali kama ujumbe wa Mungu, na kweli ndivyo ulivyo. Maana Mungu anafanya kazi ndani yenu ninyi mnaoamini.
14 For ye, brethren, became imitators of the churches of God which are in Judaea in Christ Jesus; for ye also suffered the same things from your own countrymen, as they have from the Jews;
Ndugu, ninyi mmepatwa na mambo yaleyale yaliyoyapata makanisa ya Mungu kule Yudea, mambo yaliyowapata watu walio wake Kristo Yesu. Ninyi mlidhulumiwa na wananchi wenzenu kama vile wao walivyodhulumiwa na wenzao Wayahudi,
15 who both killed the Lord Jesus, and the prophets, and drove us out, and please not God, and set themselves against all men,
ambao walimuua Bwana Yesu na manabii, wakatutesa na sisi pia. Watu hao wanamchukiza Mungu, tena ni adui za kila mtu!
16 hindering us from speaking to the gentiles that they may be saved, —to fill up their sins always! But the wrath is come upon them to the end.
Hata walijaribu kutuzuia kuwahubiria watu wa mataifa mengine ujumbe utakaowaletea wokovu. Ndivyo walivyokamilisha orodha ya dhambi zote walizotenda siku zote. Lakini sasa hasira ya Mungu imewaangukia.
17 But we, brethren, having been bereaved of you for a short time, separated in body, not in heart, used the greater endeavors with much earnestness to see your face.
Ndugu, kuachana kwetu nanyi kulikuwa kwa muda tu, tena kuachana huko kulikuwa kwa mwili tu na si kwa roho. Kitambo kifupi baadaye, tulishikwa na hamu kubwa ya kuwaoneni tena!
18 Wherefore we purposed to come to you, that is, I Paul, once and again; but Satan hindered us.
Kwa hiyo tuliamua kuwatembeleeni tena. Nami, Paulo, nilijaribu kuja kwenu zaidi ya mara moja, lakini Shetani alituzuia.
19 For what is our hope, or joy, or crown of glorying? Is it not even ye, in the presence of our Lord Jesus at his coming?
Je, tutakaposimama mbele ya Bwana Yesu wakati atakapokuja, fahari ya ushindi wetu itakuwa nini? Itakuwa ni ninyi wenyewe; ninyi ndio tumaini letu na furaha yetu.
20 For ye are our glory and joy.
Naam, ninyi ni utukufu wetu na furaha yetu!