< Romans 5 >
1 Being therefore justified by faith, we have peace with God through our Lord Jesus Christ;
Kwa kuwa tumehesabiwa haki kwa njia ya imani, tuna amani na Mungu kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo.
2 through whom we also have our access by faith into this grace in which we stand, and we rejoice in hope of the glory of God.
Kupitia yeye sisi pia tuna fursa kwa njia ya imani katika neema hii ambayo ndani yake tunasimama. Tunafurahi katika ujasiri atupao Mungu kwa ajili ya baadaye, ujasiri ambao tutashiriki katika utukufu wa Mungu.
3 Not only this, but we also rejoice in our sufferings, knowing that suffering works perseverance;
Siyo hili tu, lakini pia tunafurahi katika mateso yetu. Tunajua kwamba mateso huzaa uvumilivu.
4 and perseverance, proven character; and proven character, hope:
Uvumilivu huzaa kukubalika, na kukubalika huzaa ujasiri kwa ajili ya baadaye.
5 and hope does not disappoint us, because God's love has been poured out into our hearts through the Holy Spirit who was given to us.
Ujasiri huu haukatishi tamaa, kwa sababu upendo wa Mungu umemwagwa katika mioyo yetu kupitia Roho Mtakatifu, ambaye alitolewa kwetu.
6 For while we were yet weak, at the right time Christ died for the ungodly.
Kwa tulipokuwa tungali tu dhaifu, kwa wakati muafaka Kristo alikufa kwa ajili ya waovu.
7 For rarely does one die for the righteous. Yet perhaps for a good person someone might dare to die.
Kwa kuwa itakuwa vigumu mmoja kufa kwa ajili ya mtu mwenye haki. Hii ni kwamba, pengine mtu angethubutu kufa kwa ajili ya mtu mwema.
8 But God commends his own love toward us, in that while we were yet sinners, Christ died for us.
Lakini Mungu amehakikisha upendo wake mwenyewe kwetu, kwa sababu wakati tulipokuwa tungali wenye dhambi, Kristo alikufa kwa ajili yetu.
9 Much more then, being now justified by his blood, we will be saved from God's wrath through him.
Kisha zaidi ya yote, sasa kwa kuwa tumehesabiwa haki kwa damu yake, tutaokolewa kwa hiyo kutoka katika gadhabu ya Mungu.
10 For if, while we were enemies, we were reconciled to God through the death of his Son, much more, being reconciled, we will be saved by his life.
Kwa kuwa, ikiwa wakati tulipokuwa maadui, tulipatanishwa na Mungu kwa njia ya kifo cha mwanae, zaidi sana, baada ya kuwa tumekwisha patanishwa, tutaokolewa kwa maisha yake.
11 Not only so, but we also rejoice in God through our Lord Jesus Christ, through whom we have now received the reconciliation.
Siyo hivi tu, bali pia tunafurahi katika Mungu kupitia Bwana Yesu Kristo, kupitia yeye ambaye sasa tumepokea upatanisho huu.
12 Therefore, as sin entered into the world through one man, and death through sin; and so death passed to all people, because all sinned.
Kwa hiyo basi, kama kupitia mtu mmoja dhambi iliingia duniani, kwa njia hii kifo kiliingia kwa njia ya dhambi. Na kifo kikasambaa kwa watu wote, kwa sababu wote walifanya dhambi.
13 For until the law, sin was in the world; but sin is not charged when there is no law.
Kwa kuwa hadi sheria, dhambi ilikuwa duniani, lakini dhambi haihesabiki wakati hakuna sheria.
14 Nevertheless death reigned from Adam until Moses, even over those whose sins weren't like Adam's disobedience, who is a foreshadowing of him who was to come.
Hata hivyo, kifo kilitawala kutoka Adamu hadi Musa, hata juu ya wale ambao hawakufanya dhambi kama kutotii kwa Adamu, ambaye ni mfano wa yeye ambaye angekuja.
15 But the free gift is not like the trespass. For if by the trespass of the one the many died, much more did the grace of God, and the gift by the grace of the one man, Jesus Christ, abound to the many.
Lakini hata hivyo, zawadi ya bure si kama kosa. Kwa kuwa ikiwa kwa kosa la mmoja wengi walikufa, zaidi sana neema ya Mungu na zawadi kwa neema ya mtu mmoja, Yesu Kristo, imezidi kuongezeka kwa wengi.
16 The gift is not as through one who sinned: for the judgment came by one to condemnation, but the free gift came of many trespasses to justification.
Kwa kuwa zawadi si kama matokeo ya yule ambaye alifanya dhambi. Kwa kuwa kwa upande mwingine, hukumu ya adhabu ilikuja kwa sababu ya kosa la mtu mmoja. Lakini kwa upande mwingine, kipawa cha bure kinachotoka katika kuhesabiwa haki kilikuja baada ya makosa mengi.
17 For if by the trespass of the one, death reigned through the one; so much more will those who receive the abundance of grace and of the gift of righteousness reign in life through the one, Jesus Christ.
Kwa maana, ikiwa kwa kosa la mmoja, kifo kilitawala kupitia mmoja, zaidi sana wale ambao watapokea neema nyingi pamoja na kipawa cha haki watatawala kupitia maisha ya mmoja, Yesu Kristo.
18 So then as through one trespass, all people were condemned; even so through one act of righteousness, all people were justified to life.
Hivyo basi, kama kupitia kosa moja watu wote walikuja kwenye hukumu, ingawa kupitia tendo moja la haki kulikuja kuhesabiwa haki ya maisha kwa watu wote.
19 For as through the one man's disobedience many were made sinners, even so through the obedience of the one, many will be made righteous.
Kwa kuwa kama kupitia kutotii kwa mtu mmoja wengi walifanywa wenye dhambi, hivyo kupitia utii wa mmoja wengi watafanywa wenye haki.
20 The law came in besides, that the trespass might abound; but where sin abounded, grace abounded more exceedingly;
Lakini sheria iliingia pamoja, ili kwamba kosa liweze kuenea. Lakini mahali ambapo dhambi ilizidi kuwa nyingi, neema iliongezeka hata zaidi.
21 that as sin reigned in death, even so grace might reign through righteousness to everlasting life through Jesus Christ our Lord. (aiōnios )
Hii ilitokea ili kwamba, kama dhambi ilivyotawala katika kifo, ndivyo hata neema inaweza kutawala kupitia haki kwa ajili ya maisha ya milele kupitia Yesu Kristo Bwana wetu. (aiōnios )