< Mark 13 >

1 As he went out of the temple, one of his disciples said to him, "Teacher, see what kind of stones and what kind of buildings."
Yesu alipokuwa anatoka Hekaluni, mmoja wa wanafunzi wake alimwambia, “Mwalimu, tazama jinsi mawe haya na majengo haya yalivyo ya ajabu!”
2 And Jesus said to him, "Do you see these great buildings? There will not be left here one stone on another, which will not be thrown down."
Yesu akamwambia, “Je, unayaona majengo haya makubwa? Hakuna hata jiwe moja litakalosalia juu ya lingine; kila kitu kitabomolewa.”
3 As he sat on the Mount of Olives opposite the temple, Peter, James, John, and Andrew asked him privately,
Yesu alipokuwa ameketi juu ya mlima wa Mizeituni akielekea Hekalu, Petro, Yakobo, Yohane na Andrea wakamwuliza kwa faragha,
4 "Tell us, when will these things be? What is the sign that these things are all about to be fulfilled?"
“Twambie mambo haya yatatukia lini? Ni ishara gani itakayoonyesha kwamba mambo haya karibu yatimizwe?”
5 And Jesus began to say to them, "Be careful that no one leads you astray.
Yesu akaanza kuwaambia, “Jihadharini msije mkadanganywa na mtu.
6 Many will come in my name, saying, 'I am he.' and will lead many astray.
Maana wengi watakuja wakilitumia jina langu, wakisema, Mimi ndiye! nao watawapotosha watu wengi.
7 "When you hear of wars and rumors of wars, do not be troubled. Such things must happen, but the end is not yet.
Mtakaposikia juu ya vita na fununu za vita, msifadhaike. Mambo hayo lazima yatokee, lakini mwisho wenyewe ungali bado.
8 For nation will rise against nation, and kingdom against kingdom. There will be earthquakes in various places. There will be famines. These things are the beginning of birth pains.
Taifa moja litapigana na taifa lingine; utawala mmoja utapigana na utawala mwingine; kila mahali kutakuwa na mitetemeko ya ardhi na njaa. Mambo haya ni kama tu maumivu ya kwanza ya kujifungua mtoto.
9 But watch yourselves, for they will deliver you up to councils. You will be beaten in synagogues. You will stand before rulers and kings for my sake, as a testimony to them.
“Lakini ninyi jihadharini. Maana watu watawapelekeni mahakamani, na kuwapigeni katika masunagogi. Mtapelekwa mbele ya watawala na wafalme kwa sababu yangu ili mpate kunishuhudia kwao.
10 The Good News must first be preached to all the nations.
Lakini lazima kwanza Habari Njema ihubiriwe kwa mataifa yote.
11 When they lead you away and deliver you up, do not be anxious beforehand, or premeditate what you will say, but say whatever will be given you in that hour. For it is not you who speak, but the Holy Spirit.
Nao watakapowatieni nguvuni na kuwapeleka mahakamani, msiwe na wasiwasi juu ya yale mtakayosema; saa ile itakapofika, semeni chochote mtakachopewa, maana si ninyi mtakaosema, bali Roho Mtakatifu.
12 "Brother will deliver up brother to death, and the father his child. Children will rise up against parents, and cause them to be put to death.
Ndugu atamsaliti ndugu yake auawe; baba atamsaliti mwanae; watoto watawashambulia wazazi wao na kuwaua.
13 And you will be hated by everyone because of my name, but the one who perseveres to the end will be saved.
Watu wote watawachukieni ninyi kwa sababu ya jina langu. Lakini atakayevumilia mpaka mwisho ndiye atakayeokolewa.
14 But when you see the abomination of desolation, standing where it ought not (let the reader understand), then let those who are in Judea flee to the mountains,
“Mtakapoona Chukizo Haribifu limesimama mahali ambapo si pake, (msomaji na atambue maana yake!) Hapo watu walioko Yudea wakimbilie milimani.
15 and let him who is on the housetop not go down, nor enter in, to take anything out of his house.
Mtu aliye juu ya paa la nyumba asishuke kuingia nyumbani mwake kuchukua kitu.
16 Let him who is in the field not return back to take his coat.
Aliye shambani asirudi nyuma kuchukua vazi lake.
17 But woe to those who are with child and to those who nurse babies in those days.
Ole wao waja wazito na wanaonyonyesha siku hizo!
18 And pray that it won't be in the winter.
Ombeni ili mambo hayo yasitukie nyakati za baridi.
19 For in those days there will be oppression, such as there has not been the like from the beginning of the creation which God created until now, and never will be.
Maana wakati huo kutakuwa na dhiki ambayo haijatokea tangu Mungu alipoumba ulimwengu mpaka leo, wala haitatokea tena.
20 Unless the Lord had shortened the days, no flesh would have been saved; but for the sake of the chosen ones, whom he picked out, he shortened the days.
Kama Bwana asingepunguza siku hizo, hakuna binadamu ambaye angeokolewa. Lakini kwa ajili ya wateule wake, Bwana amezipunguza siku hizo.
21 Then if anyone tells you, 'Look, here is the Christ.' or, 'Look, there.' do not believe it.
“Basi mtu akiwaambieni, Tazama, Kristo yupo hapa! au Yupo pale! msimsadiki.
22 For there will arise false messiahs and false prophets, and will show signs and wonders, that they may lead astray, if possible, the chosen ones.
Maana watatokea kina Kristo wa uongo na manabii wa uongo, watafanya ishara na maajabu, ili kuwapotosha wateule wa Mungu, kama ikiwezekana.
23 But you watch. "I have told you all things beforehand.
Lakini ninyi jihadharini. Mimi nimewaambieni mambo yote kabla hayajatokea.
24 But in those days, after that oppression, the sun will be darkened, the moon will not give its light,
“Basi, siku hizo baada ya dhiki hiyo, jua litatiwa giza na mwezi hautaangaza.
25 the stars will be falling from heaven, and the powers that are in the heavens will be shaken.
Nyota zitaanguka kutoka angani, na nguvu za mbingu zitatikiswa.
26 Then they will see the Son of Man coming in clouds with great power and glory.
Hapo watamwona Mwana wa Mtu akija katika mawingu kwa nguvu nyingi na utukufu.
27 Then he will send out his angels, and will gather together his chosen ones from the four winds, from the farthest part of the earth to the farthest part of the sky.
Kisha atawatuma malaika wake; atawakusanya wateule wake kutoka pande zote nne za dunia, kutoka mwisho wa dunia mpaka mwisho wa mbingu.
28 "Now from the fig tree, learn this parable. When the branch has now become tender, and puts forth its leaves, you know that the summer is near;
“Kwa mtini jifunzeni mfano huu: Mara tu matawi yake yanapoanza kuwa laini na kuchanua majani, mnajua kwamba wakati wa kiangazi umekaribia.
29 even so you also, when you see these things coming to pass, know that it is near, at the doors.
Hali kadhalika nanyi mtakapoona mambo hayo yakitendeka, jueni kwamba Mwana wa Mtu yuko karibu sana.
30 Truly I say to you, this generation will not pass away until all these things happen.
Nawaambieni kweli, kizazi hiki hakitapita kabla ya mambo hayo yote kutukia.
31 Heaven and earth will pass away, but my words will not pass away.
Mbingu na dunia zitapita, lakini maneno yangu hayatapita kamwe.
32 But of that day or the hour no one knows, not even the angels in heaven, nor the Son, but only the Father.
“Lakini hakuna mtu ajuaye siku au saa hiyo itakuja lini; wala malaika wa mbinguni, wala Mwana; Baba peke yake ndiye ajuaye.
33 Watch, keep alert, and pray; for you do not know when the time is.
Muwe waangalifu na kesheni, maana hamjui wakati huo utafika lini.
34 "It is like a man, traveling to another country, having left his house, and given authority to his servants, and to each one his work, and also commanded the doorkeeper to keep watch.
Itakuwa kama mtu anayeondoka nyumbani kwenda safari akiwaachia watumishi wake madaraka, kila mmoja na kazi yake; akamwambia mlinzi wa mlango awe macho.
35 Watch therefore, for you do not know when the lord of the house is coming —at evening, or at midnight, or when the rooster crows, or in the morning;
Kesheni, basi, kwa maana hamjui mwenye nyumba atarudi lini; huenda ikawa jioni, usiku wa manane, alfajiri au asubuhi.
36 lest coming suddenly he might find you sleeping.
Kesheni ili akija ghafla asije akawakuta mmelala.
37 What I tell you, I tell all: Watch."
Ninayowaambieni ninyi, nawaambia wote: Kesheni!”

< Mark 13 >