< Deuteronomy 14 >

1 You are the people of YHWH your God: you shall not cut yourselves, nor make any baldness between your eyes for the dead.
Ninyi ni watoto wa Bwana Mungu wenu. Msijichanje ama kujinyoa upara kwenye paji la uso kwa ajili ya aliyekufa,
2 For you are a holy people to YHWH your God, and YHWH has chosen you to be a people for his own possession, above all peoples who are on the face of the earth.
kwa maana ninyi ni taifa takatifu kwa Bwana Mungu wenu. Bwana amewachagua ninyi kuwa taifa la kipekee kutoka mataifa yote juu ya uso wa dunia, mwe tunu yake.
3 You shall not eat any abominable thing.
Msile kitu chochote ambacho ni machukizo.
4 These are the animals which you may eat: the ox, the sheep, and the goat,
Hawa ndio wanyama mtakaokula: ngʼombe, kondoo, mbuzi,
5 the deer, and the gazelle, and the roebuck, and the wild goat, and the ibex, and the antelope, and the chamois.
kulungu, paa, kongoni, paa mweupe, mbuzi-mwitu, pofu na kondoo wa mlimani.
6 Every animal that parts the hoof, and has the hoof cloven in two and chews the cud, among the animals, that may you eat.
Mnaweza kumla mnyama yeyote mwenye kwato zilizogawanyika mara mbili, pia yule anayecheua.
7 Nevertheless these you shall not eat of them that chew the cud, or of those who have the hoof cloven: the camel, and the hare, and the rabbit; because they chew the cud but do not part the hoof, they are unclean to you.
Hata hivyo, miongoni mwa wale wanaocheua au wale walio na kwato zilizogawanyika kamwe msile ngamia, sungura na pelele. Iwapo wanacheua, lakini hawana kwato zilizogawanyika; ni najisi kwenu kwa taratibu za kiibada.
8 The pig, because it has a split hoof, but doesn't chew the cud, is unclean to you: of their flesh you shall not eat, and their carcasses you shall not touch.
Nguruwe pia ni najisi; ingawa ana kwato zilizogawanyika, hacheui. Msile nyama yake wala kugusa mzoga wake.
9 These you may eat of all that are in the waters: whatever has fins and scales may you eat;
Katika viumbe hai vyote viishivyo kwenye maji, mnaweza kula yeyote aliye na mapezi na magamba.
10 and whatever doesn't have fins and scales you shall not eat; it is unclean to you.
Lakini chochote kisicho na mapezi na magamba msile; kwenu ni najisi.
11 Of all clean birds you may eat.
Mnaweza kula ndege yeyote aliye safi.
12 But these are they of which you shall not eat: the eagle, and the vulture, and the osprey,
Lakini wafuatao msiwale: tai, furukombe, kipungu,
13 and the kite, and the buzzard, and the vulture after its kind,
kengewa mwekundu, kengewa mweusi, mwewe wa aina yoyote,
14 and every raven after its kind,
kunguru wa aina yoyote,
15 and the ostrich, and the owl, and the seagull, and the hawk after its kind,
mbuni, kiruka-njia, dudumizi, kipanga wa aina yoyote,
16 the little owl, and the great owl, and the horned owl,
bundi, mumbi, bundi mkubwa,
17 and the pelican, and the vulture, and the cormorant,
mwari, nderi, mnandi,
18 and the stork, and the heron after its kind, and the hoopoe, and the bat.
korongo, koikoi wa aina yoyote, hudihudi na popo.
19 All winged crawling creatures are unclean to you: they shall not be eaten.
Wadudu wote warukao kwa makundi ni najisi kwenu, msiwale.
20 Of all clean birds you may eat.
Lakini viumbe vyote vyenye mabawa vilivyo safi mwaweza kula.
21 You shall not eat of anything that dies of itself: you may give it to the foreigner living among you who is within your gates, that he may eat it; or you may sell it to a foreigner: for you are a holy people to YHWH your God. You shall not boil a young goat in its mother's milk.
Msile kitu chochote mtakachokuta kimekufa. Mnaweza kumpa mgeni yeyote anayeishi katika mojawapo ya miji yenu, naye anaweza kula au mnaweza kumuuzia mtu wa nchi nyingine. Lakini ninyi ni watu watakatifu kwa Bwana Mungu wenu. Msitokose mwana-mbuzi katika maziwa ya mama yake.
22 You shall surely tithe all the increase of your seed, that which comes forth from the field year by year.
Hakikisheni mmetenga sehemu ya kumi ya mazao yote ya mashamba yenu kila mwaka.
23 You shall eat before YHWH your God, in the place which he shall choose, to cause his name to dwell there, the tithe of your grain, of your new wine, and of your oil, and the firstborn of your herd and of your flock; that you may learn to fear YHWH your God always.
Mtakula zaka za nafaka yenu, divai mpya, mafuta na wazaliwa wa kwanza wa makundi yenu ya ngʼombe na ya kondoo na mbuzi mbele za Bwana Mungu wenu pale mahali atakapopachagua kama maskani kwa ajili ya Jina lake, ili kwamba mpate kujifunza kumheshimu Bwana Mungu wenu daima.
24 If the way is too long for you, so that you are not able to carry it, because the place is too far from you, which YHWH your God shall choose, to set his name there, when YHWH your God shall bless you;
Lakini ikiwa mahali pale ni mbali sana nanyi mmebarikiwa na Bwana Mungu wenu na hamwezi kubeba zaka yenu (kwa sababu mahali pale Bwana atakapopachagua kuliweka Jina lake ni mbali sana),
25 then you shall turn it into money, and bind up the money in your hand, and shall go to the place which YHWH your God shall choose:
basi badilisheni zaka yenu kuwa fedha, mkaichukue hiyo fedha mwende nayo mahali Bwana Mungu wenu atakapopachagua.
26 and you shall bestow the money for whatever your soul desires, for cattle, or for sheep, or for wine, or for strong drink, or for whatever your soul asks of you; and you shall eat there before YHWH your God, and you shall rejoice, you and your household.
Tumieni hiyo fedha kununua chochote ukitakacho: ngʼombe, kondoo, divai au kinywaji chochote chenye chachu au chochote mnachotaka. Kisha ninyi na wa nyumbani mwenu mtaila mbele za Bwana Mungu wenu na kufurahi.
27 The Levite who is within your gates, you shall not forsake him; for he has no portion nor inheritance with you.
Msiache kuwajali Walawi waishio katika miji yenu, kwa kuwa hao hawana shamba wala urithi wao wenyewe.
28 At the end of every three years you shall bring forth all the tithe of your increase in the same year, and shall lay it up within your gates:
Mwishoni mwa kila mwaka wa tatu, leteni zaka zote za mazao ya miaka ile na uyahifadhi kwenye miji yenu,
29 and the Levite, because he has no portion nor inheritance with you, and the foreigner living among you, and the fatherless, and the widow, who are within your gates, shall come, and shall eat and be satisfied; that YHWH your God may bless you in all the work of your hand which you do.
ili Walawi (ambao hawana mashamba wala urithi wao wenyewe) na wageni, yatima na wajane wanaoishi kwenye miji yenu wapate kuja kula na kushiba, ili Bwana Mungu wenu apate kuwabariki ninyi katika kazi zote za mikono yenu.

< Deuteronomy 14 >