< Colossians 1 >

1 Paul, an apostle of Christ Jesus through the will of God, and Timothy our brother,
Paulo, mtume wa Kristo Yesu, kwa mapenzi ya Mungu, na Timotheo ndugu yetu:
2 to the saints and faithful brothers in Christ at Colossae: Grace to you and peace from God our Father.
Kwa ndugu watakatifu na waaminifu katika Kristo, waishio Kolosai: Neema na amani zitokazo kwa Mungu Baba yetu ziwe nanyi.
3 We give thanks to God the Father of our Lord Jesus Christ, praying always for you,
Siku zote tunamshukuru Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, tunapowaombea ninyi,
4 having heard of your faith in Christ Jesus, and of the love which you have toward all the saints,
kwa sababu tumesikia kuhusu imani yenu katika Kristo Yesu, na upendo wenu mlio nao kwa watakatifu wote:
5 because of the hope which is laid up for you in heaven, of which you heard before in the word of truth, the Good News,
imani na upendo ule utokao katika tumaini mlilowekewa akiba mbinguni, na ambalo mmesikia habari zake katika neno la kweli, yaani, ile Injili
6 which has come to you; even as it is in all the world and is bearing fruit and growing, as it does in you also, since the day you heard and knew the grace of God in truth;
iliyowafikia ninyi. Duniani kote Injili hii inazaa matunda na kuenea kama ilivyokuwa kwenu tangu siku ile mlipoisikia na kuielewa neema ya Mungu katika kweli yote.
7 even as you learned of Epaphras our beloved fellow servant, who is a faithful servant of Christ on our behalf,
Mlijifunza habari zake kutoka kwa Epafra, mtumishi mwenzetu mpendwa, yeye aliye mhudumu mwaminifu wa Kristo kwa ajili yenu,
8 who also declared to us your love in the Spirit.
ambaye pia ametuambia kuhusu upendo wenu katika Roho.
9 For this cause, we also, since the day we heard this, do not cease praying and making requests for you, that you may be filled with the knowledge of his will in all spiritual wisdom and understanding,
Kwa sababu hii, tangu siku ile tuliposikia habari zenu, hatujakoma kuomba kwa ajili yenu na kumsihi Mungu awajaze ninyi maarifa ya mapenzi yake katika hekima yote ya kiroho na ufahamu.
10 that you may walk worthily of the Lord, to please him in every way, bearing fruit in every good work, and increasing in the knowledge of God;
Nasi tunaomba haya ili mpate kuishi maisha yanayostahili mbele za Bwana, na mpate kumpendeza kwa kila namna: mkizaa matunda kwa kila kazi njema, mkikua katika kumjua Mungu,
11 strengthened with all power, according to the might of his glory, for all endurance and perseverance with joy;
mkiwa mmetiwa nguvu kwa uwezo wote kwa kadiri ya nguvu yake yenye utukufu, ili mpate kuwa na wingi wa saburi na uvumilivu. Nanyi kwa furaha
12 giving thanks to the Father, who has qualified you to share in the inheritance of the saints in the light;
mkimshukuru Baba, ambaye amewastahilisha kushiriki katika urithi wa watakatifu katika ufalme wa nuru.
13 who delivered us out of the power of darkness, and transferred us into the Kingdom of the Son of his love;
Kwa maana ametuokoa kutoka ufalme wa giza na kutuingiza katika ufalme wa Mwana wake mpendwa,
14 in whom we have our redemption, the forgiveness of our sins;
ambaye katika yeye tunao ukombozi, yaani msamaha wa dhambi.
15 who is the image of the invisible God, the firstborn over all creation.
Yeye ni mfano wa Mungu asiyeonekana, mzaliwa wa kwanza wa viumbe vyote.
16 For by him all things were created, in the heavens and on the earth, things visible and things invisible, whether thrones or dominions or rulers or authorities; all things have been created by him and for him.
Kwake yeye vitu vyote vilivyoko mbinguni na juu ya nchi viliumbwa: vitu vinavyoonekana na visivyoonekana, viwe ni viti vya enzi au falme, au wenye mamlaka au watawala; vitu vyote viliumbwa na yeye na kwa ajili yake.
17 He is before all things, and in him all things are held together.
Yeye alikuwepo kabla ya vitu vyote, na katika yeye vitu vyote vinashikamana pamoja.
18 He is the head of the body, the church, who is the beginning, the firstborn from the dead; that in all things he might have the preeminence.
Yeye ndiye kichwa cha mwili, yaani kanisa, naye ndiye mwanzo na mzaliwa wa kwanza kutoka kwa wafu, ili yeye awe mkuu katika vitu vyote.
19 For all the fullness was pleased to dwell in him,
Kwa kuwa ilimpendeza Mungu kwamba utimilifu wake wote ukae ndani yake,
20 and through him to reconcile all things to himself, making peace through the blood of his cross through him, whether things on the earth or things in heaven.
na kwa njia yake aweze kuvipatanisha vitu vyote na yeye mwenyewe, viwe ni vitu vilivyo duniani au vilivyo mbinguni, kwa kufanya amani kwa damu yake, iliyomwagika msalabani.
21 You, who once were alienated and were hostile in your minds, doing evil deeds,
Hapo kwanza mlikuwa mmetengana na Mungu, na mlikuwa adui zake katika nia zenu kwa sababu ya mienendo yenu mibaya.
22 yet now he has reconciled in the body of his flesh through death, to present you holy and without blemish and blameless before him,
Lakini sasa Mungu amewapatanisha ninyi kwa njia ya mwili wa Kristo kupitia mauti, ili awalete mbele zake mkiwa watakatifu, bila dosari wala lawama,
23 if it is so that you continue in the faith, established and firm, and not moved away from the hope of the Good News which you heard, which is being proclaimed in all creation under heaven; of which I, Paul, have become a servant.
ikiwa mnaendelea katika imani yenu mkiwa imara na thabiti, pasipo kuliacha tumaini lililoahidiwa katika Injili. Hii ndiyo ile Injili mliyoisikia, ambayo imehubiriwa kwa kila kiumbe chini ya mbingu, na ambayo mimi Paulo nimekuwa mtumwa wake.
24 Now I rejoice in my sufferings for your sake, and I am completing in my flesh what is lacking in the sufferings of Christ for the sake of his body, which is the church;
Sasa nafurahia kule kuteseka kwangu kwa ajili yenu, na katika mwili wangu ninatimiliza yale yaliyopungua katika mateso ya Kristo kwa ajili ya mwili wake, ambao ni kanisa.
25 of which I was made a servant, according to the stewardship of God which was given me toward you, to fulfill the word of God,
Mimi nimekuwa mtumishi wa kanisa kwa wajibu alionipa Mungu ili kuwaletea ninyi Neno la Mungu kwa ukamilifu:
26 the mystery which has been hidden for ages and generations. But now it has been revealed to his saints. (aiōn g165)
Hii ni siri iliyokuwa imefichika tangu zamani na kwa vizazi vingi, lakini sasa imefunuliwa kwa watakatifu. (aiōn g165)
27 To them God was pleased to make known the glorious riches of this mystery among the non-Jews, which is Christ in you, the hope of glory;
Kwao, Mungu amechagua kujulisha miongoni mwa watu wa Mataifa utukufu wa utajiri wa siri hii, ambayo ni Kristo ndani yenu, tumaini la utukufu.
28 whom we proclaim, admonishing everyone and teaching everyone all wisdom, that we may present everyone perfect in Christ Jesus;
Yeye ndiye tunayemtangaza, tukimwonya kila mtu na kumfundisha kila mtu kwa hekima yote ili tuweze kumleta kila mmoja akiwa amekamilika katika Kristo.
29 for which I also labor, struggling according to his power, which works in me mightily.
Kwa ajili ya jambo hili, ninajitaabisha, nikijitahidi kwa kadiri ya nguvu zake ambazo hutenda kazi ndani yangu kwa uweza mwingi.

< Colossians 1 >