< 2 Corinthians 13 >
1 This is the third time I am coming to you. "At the mouth of two or three witnesses will every word be established."
Hii ni mara ya tatu kwamba nakuja kwenu. “Kila shitaka lazima lijengwe na uthibitisho wa mashahidi wawili au watatu.”
2 I have said beforehand, and I do say beforehand, as when I was present the second time, so now, being absent, to those who have sinned before now, and to all the rest, that, if I come again, I will not spare;
Nimekwishashasema kwa hao waliotenda dhambi kabla na kwa wengine wote wakati nilipokuwa huko mara ya pili, na ninasema tena: Nitakapokuja tena, sitawavumilia.
3 seeing that you seek a proof of Christ who speaks in me; who toward you is not weak, but is powerful in you.
Nawaambia ninyi hili kwa sababu mnatafuta ushahidi kwamba Kristo ananena kupitia mimi. Yeye sio dhaifu kwenu, badala yake, yeye ni mwenye nguvu ndani yenu.
4 For indeed he was crucified through weakness, yet he lives through the power of God. For we also are weak in him, but we will live with him through the power of God toward you.
Kwa kuwa alisulibiwa katika udhaifu, lakini yu hai kwa nguvu za Mungu. Kwa kuwa sisi pia tu dhaifu ndani yake, lakini tutaishi naye kwa nguvu za Mungu miongoni mwenu.
5 Test your own selves, whether you are in the faith. Test your own selves. Or do you not know as to your own selves, that Jesus Christ is in you?—unless indeed you are disqualified.
Jichunguzeni wenyewe muone kama mko katika imani. Jipimeni wenyewe. Hamgundui kwamba Yesu Kristo yu ndani yenu? Yeye yumo, vinginevyo kama hamjathibitishwa.
6 But I hope that you will know that we are not disqualified.
Na nina ujasiri kwamba ninyi mtagundua kwamba sisi hatukukataliwa.
7 Now we pray to God that you do no evil; not that we may appear approved, but that you may do that which is honorable, though we are as reprobate.
Sasa tunaomba kwa Mungu kwamba msiweze kufanya chochote kibaya. Siombi kwamba sisi tuweze kuonekana tumepita jaribu, badala yake ninaomba kwamba muweze kufanya kilicho sahihi, Ingawa tunaweza kuonekana tumeshindwa jaribu.
8 For we can do nothing against the truth, but for the truth.
Kwa kuwa sisi hatuwezi kufanya lolote kinyume na kweli, lakini ni kwa ajili ya kweli tu.
9 For we rejoice when we are weak and you are strong. And this we also pray for, even your perfecting.
Kwa kuwa tunafurahi wakati tunapokuwa dhaifu nanyi mkiwa na nguvu. Tunaomba pia kwamba muweze kufanywa wakamilifu.
10 For this cause I write these things while absent, that I may not deal sharply when present, according to the authority which the Lord gave me for building up, and not for tearing down.
Nayaandika mambo haya wakati nikiwa mbali nanyi, ili kwamba wakati nikiwa pamoja nanyi sihitaji kuwaonesha ukali ninyi. Sihitaji kutumia mamlaka Bwana aliyonipaa mimi niwajenge na siyo kuwaharibu chini.
11 Finally, brothers, rejoice. Be perfected, be comforted, be of the same mind, live in peace, and the God of love and peace will be with you.
Hatimaye, ndugu wa kiume na wa kike, furahini! fanyeni kazi kwa ajili ya urejesho, mtiwe moyo, kubalianeni ninyi kwa ninyi, muishi katika amani. Na Mungu wa upendo na amani atakuwa pamoja nanyi.
12 Greet one another with a holy kiss.
Salimianeni kila mmoja kwa busu takatifu.
13 All the saints greet you.
Waumini wote wanawasalimu.
14 The grace of the Lord Jesus Christ, the love of God, and the fellowship of the Holy Spirit, be with you all.
Neema ya Bwana Yesu Kristo, upendo wa Mungu, na ushirika wa Roho Mtakatifu uwe pamoja nanyi nyote.