< Revelation 21 >
1 I saw a new heaven and a new earth: for the first heaven and the first earth have passed away, and the sea is no more.
Kisha nikaona mbingu mpya na nchi mpya, kwa kuwa mbingu ya kwanza na nchi ya kwanza zimekwishapita, na bahari haikuwepo tena.
2 I saw the holy city, New Jerusalem, coming down out of heaven from God, made ready like a bride adorned for her husband.
Niliona mji mtakatifu, Yerusalemu mpya, ambao ulikuja chini kutoka mbinguni kwa Mungu, ulioandaliwa kama bibi harusi aliyepambwa kwa ajili ya mumewe.
3 I heard a loud voice from the throne saying, "Look, the tabernacle of God is with humans, and he will dwell with them, and they will be his people, and God himself will be with them and be their God.
Nilisikia sauti kubwa kutoka kwenye kiti cha enzi ikisema, “Tazama! Makao ya Mungu yapo pamoja na wanadamu, naye ataishi pamoja nao. Watakuwa watu wake, na Mungu mwenyewe atakuwa nao na atakuwa Mungu wao.
4 And he will wipe away every tear from their eyes, and death will be no more, nor will there be mourning, nor crying, nor pain anymore, for the first things have passed away."
Atafuta kila chozi kutoka katika macho yao, na hapatakuwa na kifo tena, au kuomboleza, au kulia, au maumivu. Mambo ya zamani yamekwishakupita.
5 He who sits on the throne said, "Look, I am making all things new." He said, "Write, for these words are faithful and true."
Yeye ambaye alikuwa ameketi juu ya kiti cha enzi alisema, “Tazama! Nafanya mambo yote kuwa mapya.” Alisema, “Andika hili kwa sababu maneno haya ni ya hakika na kweli.”
6 He said to me, "It is done. I am the Alpha and the Omega, the Beginning and the End. I will give freely to him who is thirsty from the spring of the water of life.
Aliniambia, “Mambo haya yalikwisha kupita! Mimi ni Alfa na Omega, mwanzo na mwisho. Kwa yeyote aonaye kiu nitampatia kinywaji bila gharama kutoka katika chemchemi za maji ya uzima.
7 He who overcomes, I will give him these things. I will be his God, and he will be my son.
Yeye ashindaye atayarithi mambo haya, na nitakuwa Mungu wake, naye atakuwa mwanangu.
8 But for the cowardly, unbelieving, abominable, murderers, sexually immoral, sorcerers, idolaters, and all liars, their part is in the lake that burns with fire and sulfur, which is the second death." (Limnē Pyr )
Lakini kama ilivyo kwa waoga, wasioamini, wachukizao, wauaji, wazinzi, wachawi, waabudu sanamu, na waongo wote, sehemu yao itakuwa katika ziwa la moto wa kiberiti uunguzao. Hiyo ndiyo mauti ya pili.” (Limnē Pyr )
9 One of the seven angels who had the seven bowls, full of the seven last plagues came, and he spoke with me, saying, "Come here. I will show you the bride, the wife of the Lamb."
Mmoja wa malaika saba alikuja kwangu, mmoja ambaye alikuwa na mabakuli saba yaliyojaa mapigo saba ya mwisho na alisema, “Njoo hapa. Nitakuonesha bibi harusi, mke wa mwana kondoo.”
10 He carried me away in the Ruach to a great and high mountain, and showed me the holy city, Jerusalem, coming down out of heaven from God,
Kisha alinichukua mbali katika Roho kwenye mlima mkubwa na mrefu na alinionesha mji mtakatifu, Yerusalemu, ukishuka chini kutoka mbinguni kwa Mungu.
11 having the glory of God. Her light was like a most precious stone, as if it was a jasper stone, clear as crystal;
Yerusalemu ulikuwa na utukufu wa Mungu, na uzuri wake ulikuwa kama kito cha thamani, kama jiwe la kioo safi la yaspi.
12 having a great and high wall; having twelve gates, and at the gates twelve angels; and names written on them, which are the names of the twelve tribes of the children of Israel.
Ulikuwa na ukuta mkubwa, mrefu wenye milango kumi na miwili, pamoja na malaika kumi na wawili milangoni. Juu ya milango palikuwa pameandikwa majina ya makabila kumi na mawili ya wana wa Israeli.
13 On the east were three gates; and on the north three gates; and on the south three gates; and on the west three gates.
Upande wa mashariki palikuwa na milango mitatu, upande wa kusini milango mitatu, upande wa kaskazini milango mitatu, na upande wa magharibi milango mitatu.
14 The wall of the city had twelve foundations, and on them twelve names of the twelve emissaries of the Lamb.
Kuta za mji zilikuwa na misingi kumi na miwili, na juu yake palikuwa na majina kumi na mawili ya mitume kumi na wawili wa Mwana Kondoo.
15 He who spoke with me had for a measure, a golden reed, to measure the city, its gates, and its wall.
Mmoja aliyeongea nami alikuwa na kipimo cha fimbo iliyotengenezwa kwa dhahabu kwa ajili ya kupima mji, milango yake na kuta zake.
16 The city lies foursquare, and its length is as great as its breadth. He measured the city with the reed, one thousand three hundred eighty miles. Its length, breadth, and height are equal.
Mji uliwekwa ndani ya mraba; urefu wake ulikuwa sawa na upana wake. Alipima mji kwa kipimio cha fimbo, stadia 12, 000 kwa urefu (urefu wake, upana, na kimo vilifanana).
17 Its wall is one hundred forty-four cubits, by human measurement, that is, of an angel.
Vilevile alipima ukuta wake, unene wake ulikuwa dhiraa 144 kwa vipimo vya kibinadamu (ambavyo pia ni vipimo vya malaika).
18 The construction of its wall was jasper. The city was pure gold, like pure glass.
Ukuta ulikuwa umejengwa kwa yaspi na mji wenye dhahabu safi, kama kioo safi.
19 The foundations of the city's wall were adorned with all kinds of precious stones. The first foundation was jasper; the second, sapphire; the third, chalcedony; the fourth, emerald;
Misingi ya ukuta ilikuwa imepambwa na kila aina ya jiwe la thamani. La kwanza lilikuwa yaspi, la pili lilikuwa yakuti samawi, la tatu lilikuwa kalkedon, la nne zumaridi,
20 the fifth, sardonyx; the sixth, sardius; the seventh, chrysolite; the eighth, beryl; the ninth, topaz; the tenth, chrysoprasus; the eleventh, jacinth; and the twelfth, amethyst.
la tano sardoniki, la sita akiki, la saba krisolitho, la nane zabarajadi, la tisa yakuti ya manjano, la kumi krisopraso, la kumi na moja hiakintho, la kumi na mbili amethisto.
21 The twelve gates were twelve pearls. Each one of the gates was made of one pearl. The street of the city was pure gold, like transparent glass.
Milango kumi na miwili ilikuwa lulu kumi na mbili, kila mlango ulitengenezwa kutoka kwenye lulu moja. Mitaa ya mji ilikuwa dhahabu safi, ikionekana kama kioo safi.
22 I saw no temple in it, for the Lord God the Almighty and the Lamb are its temple.
Sikuona hekalu lolote ndani ya mji, kwa kuwa Bwana Mungu, ambaye anatawala juu ya vyote, na Mwana Kondoo ni hekalu lake.
23 The city has no need for the sun, neither of the moon, to shine, for the very glory of God illuminated it, and its lamp is the Lamb.
Mji haukuhitaji jua au mwezi ili kungaza juu yake kwa sababu utukufu wa Mungu uliangaza juu yake, na taa yake ni Mwana Kondoo.
24 The nations will walk in its light. The kings of the earth bring their splendor into it.
Mataifa watatembea kwa mwanga wa mji huo. Wafalme wa dunia wataleta fahari zao ndani yake.
25 Its gates will in no way be shut by day (for there will be no night there),
Milango yake haitafungwa wakati wa mchana, na hapatakuwa na usiku pale.
26 and they shall bring the glory and the honor of the nations into it so that they may enter.
Wataleta fahari na heshima ya mataifa ndani yake,
27 There will in no way enter into it anything profane, or one who causes an abomination or a lie, but only those who are written in the Lamb's Book of Life.
na hakuna kichafu kitakachoingia ndani yake. Wala yeyote ambaye afanyaye jambo lolote la aibu au udanganyifu hataingia, bali ni wale tu ambao majina yao yameandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana Kondoo.