< John 3 >
1 Now there was a man of the Pharisees named Nicodemus, a ruler of the Jewish people.
Basi kulikuwa na Farisayo ambaye jina lake Nikodemo, mmoja wa wajumbe wa baraza la Wayahudi.
2 This man came to him at night, and said to him, "Rabbi, we know that you are a teacher come from God, for no one can do these signs that you do, unless God is with him."
Mtu huyu alimwendea Bwana Yesu usiku na akamwambia, “Rabi, tunajua ya kuwa u mwalimu kutoka kwa Mungu, kwa maana hakuna mtu awezaye kutenda ishara hizi zote Mungu asipokuwa pamoja naye.”
3 Jesus answered him, "Truly, truly, I tell you, unless one is born again he cannot see the kingdom of God."
Yesu akamjibu, “Amini, amini, mtu hawezi kuingia katika ufalme wa Mungu asipozaliwa mara ya pili.”
4 Nicodemus said to him, "How can anyone be born when he is old? Can he enter a second time into his mother's womb, and be born?"
Nikodemo akasema,” Mtu anawezaje kuzaliwa akiwa mzee? Hawezi kuingia tumboni mwa mama yake mara ya pili na kuzaliwa, je anaweza?”
5 Jesus answered, "Truly, truly, I tell you, unless one is born of water and Spirit he cannot enter into the kingdom of God.
Yesu akajibu, “Amini, amini mtu sipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuingia katika ufalme wa Mungu.
6 That which is born of the flesh is flesh. That which is born of the Spirit is spirit.
Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili, na kilichozaliwa kwa Roho ni roho.
7 Do not be surprised that I said to you, 'You must be born again.'
Usishangae kwa sababu nilikuwambia, 'ni lazima kuzaliwa mara ya pili.'
8 The wind blows where it wants to, and you hear its sound, but do not know where it comes from and where it is going. So is everyone who is born of the Spirit."
Upepo huvuma popote upendapo na sauti yake mwaisikia, lakini hamjui utokako wala uendako. Ndivyo ilivyo hali ya kila aliyezaliwa na roho.
9 Nicodemus answered and said to him, "How can these things be?"
Nikodemo akajibu, kwa kusema, “Mambo haya yawezekanaje?”
10 Jesus answered him, "Are you the teacher of Israel, and do not understand these things?
Yesu akamjibu, “Wewe u mwalimu wa Israeli, hata hauyajui mambo haya?
11 Truly, truly, I tell you, we speak that which we know, and testify of that which we have seen, but you do not accept our testimony.
Amini, amini, nakuambia, kile tunachokifahamu twakishuhudia kwa kile tulichokiona. Lakini hampokei ushuhuda wetu.
12 If I told you earthly things and you do not believe, how will you believe if I tell you heavenly things?
Kama nimewambia mambo ya hapa duniani na hamuamini, mtawezaje kuamini kama nikiwambia mambo ya mbinguni?
13 And no one has ascended into heaven, but he who descended out of heaven, the Son of Man, who is in heaven.
Maana hakuna aliyepanda juu kutoka mbinguni isipokuwa yeye aliyeshuka, Mwana wa Adamu.
14 And as Moses lifted up the serpent in the wilderness, even so must the Son of Man be lifted up,
Kama vile Musa alivyomwinua nyoka jangwani, vivyo hivyo Mwana wa Adamu lazima ainuliwe,
15 so that everyone who believes in him may have life without end. (aiōnios )
ili kwamba wote watakaomwamini wapate uzima wa milele. (aiōnios )
16 For this is how God loved the world: he gave his only Son, so that everyone who believes in him will not perish but have life without end. (aiōnios )
Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, kwamba akamtoa mwanae wa pekee, ili kwamba mtu yeyote amwaminiye asiangamie bali awe na uzima wa milele. (aiōnios )
17 For God did not send his Son into the world to judge the world, but that the world should be saved through him.
Kwa sababu Mungu hakumtuma mwanae duniani ili auhukumu ulimwengu, bali kwamba ulimwengu uokolewe katika yeye.
18 The one who believes in him is not judged, but the one who does not believe has been judged already, because he has not believed in the name of the only Son of God.
Amwaminiye Yeye hatahukumiwa. Yeye asiyemwamini tayari ameshahukumiwa kwa sababu hajaliamini jina la Mwana pekee wa Mungu.
19 This is the judgment, that the light has come into the world, and people loved the darkness rather than the light, because their works were evil.
Hii ndiyo sababu ya hukumu, ya kwamba nuru imekuja ulimwenguni, lakini wanadamu wakapenda giza zaidi ya nuru kwa sababu matendo yao yalikuwa maovu.
20 For everyone who does evil hates the light, and does not come to the light, so that his works will not be exposed.
kila mtu atendaye mabaya huichukia nuru wala haji nuruni ili matendo yake yasije yakawekwa wazi.
21 But the one who does the truth comes to the light, that his works may be revealed, that they have been done in God."
Lakini, yeye atendaye kweli huja kwenye nuru ili matendo yake yaonekane kwamba yametendwa kwa utiifu wa Mungu.
22 After these things, Jesus came with his disciples into the land of Judea. He stayed there with them, and was baptizing.
Baada ya haya, Yesu pamoja na wanafunzi walienda katika nchi ya Yudea. Huko alitumia muda pamoja nao na alikuwa akibatiza.
23 Now John also was baptizing in Aenon near Salim, because there was much water there. They came, and were baptized.
Sasa Yohana pia alikuwa akibatiza huko Ainea karibu na Salim maana kulikuwa na maji mengi pale. Watu walikuwa wakija kwake na kubatizwa,
24 For John was not yet thrown into prison.
kwa kuwa Yohana alikuwa hajatupwa gerezani.
25 Now a dispute arose between John's disciples with a Jew about purification.
Kisha palitokea mabishano kati ya wanafunzi wa Yohana na Myahudi kuhusu sikukuuu za utakaso.
26 And they came to John, and said to him, "Rabbi, he who was with you beyond the Jordan, to whom you have testified, look, he is baptizing, and everyone is coming to him."
Wakaenda kwa Yohana wakamwambia, “Rabi, yeye uliyekuwa naye ng'ambo ya Mto Yorodani, yeye uliyeshuhudia habari zake, tazama, anabatiza na wote wanaenda wanamfuata.”
27 John answered, "No one can receive anything, unless it has been given to him from heaven.
Yohana akajibu mtu hawezi kupokea kitu chochote isipokuwa kama amepewa kutoka mbinguni.
28 You yourselves bear me witness that I said, 'I am not the Christ,' but, 'I have been sent before him.'
Ninyi wenyewe mwashuhudia kuwa nalisema kuwa, 'mimi sio Kristo', badala yake nilisema, 'nimetumwa mbele yake.'
29 He who has the bride is the bridegroom; but the friend of the bridegroom, who stands and hears him, rejoices greatly because of the bridegroom's voice. So this joy of mine is now complete.
Yeye aliye na bibi arusi ni bwana harusi. Sasa rafiki wa bwana arusi, asimamaye na kusikiliza hufurahia sana kwa sababu ya sauti ya bwana arusi. Hii sasa ni furaha yangu iliyotimilika.
30 He must increase, but I must decrease.
Anapaswa kuzidi, nami napaswa kupungua.
31 He who comes from above is above all. He who is from the earth belongs to the earth, and speaks of the earth. He who comes from heaven is above all.
Yeye atokaye juu, yu juu ya yote. Yeye aliye wa ulimwengu anatoka ulimwenguni na huongea mambo ya ki ulimwengu. Yeye atokaye mbinguni yuko juu ya yote.
32 What he has seen and heard, of that he testifies; and no one receives his witness.
Yeye hushuhudia yale aliyoyaona na kuyasikia, lakini hakuna apokeaye ushuhuda wake.
33 He who has received his witness has set his seal to this, that God is true.
Yeye aliye pokea ushuhuda wake amehakikisha kuwa Mungu ni mkweli.
34 For he whom God has sent speaks the words of God; for he does not give the Spirit by measure.
Kwa sababu yeye aliyetumwa na Mungu huongea maneno ya Mungu. Kwa kuwa hampi Roho kwa kipimo.
35 The Father loves the Son, and has given all things into his hand.
Baba humpenda Mwana na amempa vitu vyote mikononi mwake.
36 Whoever believes in the Son has everlasting life, but whoever refuses to believe in the Son won't see life, but the wrath of God remains on him." (aiōnios )
Yeye amwaminiye Mwana anao uzima wa milele, lakini kwa yeye asiye mtii Mwana hatauona uzima, bali ghadhabu ya Mungu hushikamana juu yake. (aiōnios )