< 1 Peter 4 >
1 Forasmuch then as Christ suffered in the flesh, arm yourselves also with the same mind; for he who has suffered in the flesh has ceased from sin;
Kwa hiyo, kwa kuwa Kristo aliteswa katika mwili wake, ninyi nanyi jivikeni nia iyo hiyo kwa maana mtu aliyekwisha kuteswa katika mwili ameachana na dhambi.
2 that you no longer should live the rest of your time in the flesh for human desires, but for the will of God.
Kwa hivyo, haishi maisha yake yaliyobaki ya kuishi hapa duniani kwa tamaa mbaya za wanadamu, bali anaishi kwa mapenzi ya Mungu.
3 For enough time in the past has been spent doing the will of the unbelievers, and having walked in lewdness, lusts, drunkenness, orgies, carousings, and abominable idolatries.
Maana wakati uliopita mmekwisha kutumia muda wa kutosha katika maisha yenu mkifanya yale ambayo wapagani hupenda kutenda: wakiishi katika uasherati, tamaa mbaya, ulevi, karamu za ulafi, vileo, ngoma mbaya, na ibada chukizo za sanamu.
4 They think it is strange that you do not run with them into the same flood of debauchery, blaspheming:
Wao hushangaa kwamba ninyi hamjiingizi pamoja nao katika huo wingi wa maisha ya ufisadi, nao huwatukana ninyi.
5 who will give account to him who is ready to judge the living and the dead.
Lakini itawapasa wao kutoa hesabu mbele zake yeye aliye tayari kuwahukumu walio hai na waliokufa.
6 For this reason also the Good News was preached to those who are now dead, that they might be judged according to man in the flesh, but might live according to God in the Spirit.
Kwa kuwa hii ndiyo sababu Injili ilihubiriwa hata kwa wale waliokufa, ili wahukumiwe sawasawa na wanadamu wengine katika mwili, lakini katika roho waishi kulingana na Mungu aishivyo.
7 But the end of all things is near. Therefore be serious and disciplined in your prayers.
Mwisho wa mambo yote umekaribia. Kwa hiyo kuweni na akili tulivu na kiasi, mkikesha katika kuomba.
8 Above all things be earnest in your love among yourselves, for love covers a multitude of sins.
Zaidi ya yote, dumuni katika upendo kwa maana upendo husitiri wingi wa dhambi.
9 Be hospitable to one another without grumbling.
Kuweni wakarimu kila mtu na mwenzake pasipo manungʼuniko.
10 As each has received a gift, employ it in serving one another, as good managers of the grace of God in its various forms.
Kila mmoja na atumie kipawa chochote alichopewa kuwahudumia wengine, kama mawakili waaminifu wa neema mbalimbali za Mungu.
11 If anyone speaks, let it be as it were the very words of God. If anyone serves, let it be as of the strength which God supplies, that in all things God may be glorified through Jesus Christ, to whom belong the glory and the dominion forever and ever. Amen. (aiōn )
Yeyote asemaye hana budi kusema kama mtu asemaye maneno ya Mungu mwenyewe. Yeyote ahudumuye hana budi kuhudumu kwa nguvu zile anazopewa na Mungu, ili Mungu apate kutukuzwa katika mambo yote kwa njia ya Yesu Kristo. Utukufu na uweza una yeye milele na milele. Amen. (aiōn )
12 Beloved, do not be astonished at the fiery trial which has come upon you, to test you, as though a strange thing happened to you.
Wapenzi, msione ajabu kwa yale mateso yanayotukia miongoni mwenu, kana kwamba ni kitu kigeni kinachowapata.
13 But because you are partakers of Christ's sufferings, rejoice; that at the revelation of his glory you also may rejoice with exceeding joy.
Bali furahini kuwa mnashiriki katika mateso ya Kristo, ili mpate kufurahi zaidi wakati utukufu wake utakapofunuliwa.
14 If you are insulted for the name of Christ, you are blessed; because the Spirit of glory and of God rests on you. On their part he is blasphemed, but on your part he is glorified.
Kama mkitukanwa kwa ajili ya jina la Kristo, mmebarikiwa, kwa sababu Roho wa utukufu na wa Mungu anakaa juu yenu.
15 For let none of you suffer as a murderer, or a thief, or an evil doer, or a meddler.
Lakini asiwepo mtu yeyote miongoni mwenu anayeteswa kwa kuwa ni muuaji, au mwizi, au mhalifu wa aina yoyote, au anayejishughulisha na mambo ya watu wengine.
16 But if as a Christian, let him not be ashamed, but let him glorify God in this name.
Lakini kama ukiteseka kwa kuwa Mkristo, usihesabu jambo hilo kuwa ni aibu, bali mtukuze Mungu kwa sababu umeitwa kwa jina hilo.
17 For the time has come for judgment to begin with the household of God; and if it begins first with us, what will happen to those who do not obey the Good News of God?
Kwa maana wakati umewadia wa hukumu kuanzia katika nyumba ya Mungu. Basi kama ikianzia kwetu sisi, mwisho wa hao wasiotii Injili ya Mungu utakuwaje?
18 And "If the righteous is delivered with difficulty, where will the ungodly and the sinner appear?"
Basi, “Ikiwa ni vigumu kwa mwenye haki kuokoka, itakuwaje kwa mtu asiyemcha Mungu na mwenye dhambi?”
19 Therefore let them also who suffer according to the will of God in doing good entrust their souls to him, as to a faithful Creator.
Kwa hiyo, wale wanaoteswa kulingana na mapenzi ya Mungu, wajikabidhi kwa Muumba wao aliye mwaminifu, huku wakizidi kutenda mema.