< Matthew 16 >

1 Then the Pharisees and Sadducees came to him, and in order to test him, asked him to show them a sign from heaven.
Mafarisayo na Masadukayo wakamjia Yesu na kumjaribu kwa kumwomba awaonyeshe ishara kutoka mbinguni.
2 In answer he said. "In the evening you say, ‘It will be fine weather, for the sky is red as fire’;
Yesu akawajibu, “Ifikapo jioni, mnasema, ‘Hali ya hewa itakuwa nzuri, kwa kuwa anga ni nyekundu.’
3 and at dawn you say, ‘It will storm today, for the sky is red and lowering.’ You know how to discern the look of the sky, but the signs of the times you cannot read.
Nanyi wakati wa asubuhi mnasema, ‘Leo kutakuwa na dhoruba, kwa sababu anga ni nyekundu na mawingu yametanda.’ Mnajua jinsi ya kupambanua kule kuonekana kwa anga, lakini hamwezi kupambanua dalili za nyakati.
4 A wicked and faithless generation is seeking a sign, but no sign shall be given it but the sign of Jonah." So he left them and went away.
Kizazi kiovu na cha uzinzi kinatafuta ishara, lakini hakitapewa ishara yoyote isipokuwa ishara ya Yona.” Yesu akawaacha, akaenda zake.
5 When his disciples reached the other side of the lake, they had forgotten to bring bread.
Wanafunzi wake walipofika ngʼambo ya bahari, walikuwa wamesahau kuchukua mikate.
6 Presently Jesus said to them, "Take heed and beware of the leaven of the Pharisees."
Yesu akawaambia, “Jihadharini. Jilindeni na chachu ya Mafarisayo na ya Masadukayo.”
7 And they began discussing it among themselves, saying, "It is because we did not bring any bread."
Wakajadiliana wao kwa wao, wakisema, “Ni kwa sababu hatukuleta mikate.”
8 When Jesus knew it he said. "Weaklings in faith! Why are you arguing among yourselves, because you have no bread?
Yesu, akifahamu majadiliano yao, akauliza, “Enyi wa imani haba! Mbona mnajadiliana miongoni mwenu kuhusu kutokuwa na mikate?
9 "Do you not remember the five loaves for the five thousand, and how many large basketfuls you took up?
Je, bado hamwelewi? Je, hamkumbuki ile mikate mitano iliyolisha watu 5,000 na idadi ya vikapu vingapi vya mabaki mlivyokusanya?
10 "Nor the seven loaves for the four thousand, and how many large basketfuls you took up?
Au ile mikate saba iliyolisha watu 4,000 na idadi ya vikapu vingapi vya mabaki mlivyokusanya?
11 "How is it that you do not perceive that I did not speak to you concerning bread? But beware off the leaven of the Pharisees and Sadducees!"
Inakuwaje mnashindwa kuelewa kwamba nilikuwa sisemi nanyi habari za mikate? Jilindeni na chachu ya Mafarisayo na Masadukayo.”
12 Then they realized that he had not told them to beware of the leaven, but of the teaching of the Pharisees and Sadducees.
Ndipo wakaelewa kwamba alikuwa hasemi juu ya chachu ya kutengeneza mikate, bali juu ya mafundisho ya Mafarisayo na Masadukayo.
13 When Jesus came into the neighborhood of Caesarea Philippi, he asked his disciples, "Who do people say that the Son of man is?"
Basi Yesu alipofika katika eneo la Kaisaria-Filipi, akawauliza wanafunzi wake, “Watu husema kwamba mimi Mwana wa Adamu ni nani?”
14 They replied, "Some say ‘Johnthe Baptist’; others, however, say that’He is Elijah’; others, ‘Jeremiah,’ or ‘One of the Prophets.’"
Wakamjibu, “Baadhi husema ni Yohana Mbatizaji; wengine husema ni Eliya; na bado wengine husema ni Yeremia au mmojawapo wa manabii.”
15 "And who do you say that I am?" he asked them.
Akawauliza, “Je, ninyi mnasema mimi ni nani?”
16 So Simon Peter answered, "You are the Christ, the Son of the living God."
Simoni Petro akamjibu, “Wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai.”
17 "Blessed are you, Simon, Son of Jonah," said Jesus; "for flesh and blood have not revealed this to you, but my Father who is in heaven!
Naye Yesu akamwambia, “Heri wewe, Simoni Bar-Yona, kwa maana hili halikufunuliwa kwako na mwanadamu, bali na Baba yangu aliye mbinguni.
18 "Moreover I say to you that you are Petros (a rock), and on this petra (rock) I will build my church, and the gates of Hades shall not prevail against her. (Hadēs g86)
Nami nakuambia, wewe ndiwe Petro na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu, hata malango ya Kuzimu hayataweza kulishinda. (Hadēs g86)
19 "I will give you the keys of the kingdom of heaven; and whatever you bind upon the earth shall be bound in the heavens, and whatever you loose upon earth shall be loosed in the heavens."
Nitakupa funguo za Ufalme wa mbinguni, na lolote utakalolifunga duniani litakuwa limefungwa Mbinguni, nalo lolote utakalofungua duniani litakuwa limefunguliwa mbinguni.”
20 Then he enjoined his disciples to tell no one that he was the Christ.
Kisha akawakataza wanafunzi wake wasimwambie mtu yeyote kwamba yeye ndiye Kristo.
21 After this Jesus the Christ began to show his disciples how he must go to Jerusalem, and suffer many things at the hands of the elders and chief priests and Scribes, and be put to death, and on the third day be raised again.
Tangu wakati huo, Yesu alianza kuwaeleza wanafunzi wake kwamba hana budi kwenda Yerusalemu na kupata mateso mengi mikononi mwa wazee, viongozi wa makuhani, na walimu wa sheria, na kwamba itampasa auawe lakini siku ya tatu kufufuliwa.
22 Then Peter took him aside and began to reprove him, saying. "God forbid, Master! That shall never befall you."
Petro akamchukua kando, akaanza kumkemea akisema, “Haiwezekani, Bwana! Jambo hili kamwe halitakupata!”
23 But he turned and said to Peter. "Get behind me, Satan! You are a stumbling-block to me, because you are not intent on what pleases God, but what pleases men."
Lakini Yesu akageuka na kumwambia Petro, “Rudi nyuma yangu, Shetani! Wewe ni kikwazo kwangu. Moyo wako hauwazi yaliyo ya Mungu, bali ya wanadamu.”
24 Then Jesus said to his disciples. "If any man wishes to come after me, let him renounce self, take up his cross, and follow me.
Ndipo Yesu akawaambia wanafunzi wake, “Mtu yeyote akitaka kunifuata, ni lazima ajikane mwenyewe, auchukue msalaba wake, anifuate.
25 For he who wants to save his life will lose it; but whoever loses his life for my sake will find it.
Kwa maana yeyote anayetaka kuyaokoa maisha yake atayapoteza, lakini yeyote atakayeyapoteza maisha yake kwa ajili yangu atayapata.
26 What will it profit a man to gain the whole world and lose his soul? or what shall a man give in exchange for his soul?
Kwa maana, je, itamfaidi nini mtu kuupata ulimwengu wote, lakini akayapoteza maisha yake? Au mtu atatoa nini badala ya nafsi yake?
27 For the Son of man is about to come in the glory of his Father, and his angels with him, and then will he reward each one in accordance with his actions.
Kwa maana Mwana wa Adamu atakuja katika utukufu wa Baba yake pamoja na malaika zake, naye ndipo atakapomlipa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake.
28 Solemnly I tell you, some of those who are standing here shall not taste death, till they have seen the Son of man coming in his kingdom.
Nawaambia kweli, baadhi yenu hapa hawataonja mauti kabla ya kumwona Mwana wa Adamu akija katika Ufalme wake.”

< Matthew 16 >