< Romans 5 >

1 Having been declared righteous, then, by faith, we have peace toward God through our Lord Jesus Christ,
Sasa, kwa vile tumekubaliwa kuwa wadilifu kwa imani, basi, tunayo amani na Mungu kwa ajili ya Bwana wetu Yesu Kristo.
2 through whom also we have the access by faith into this grace in which we have stood, and we boast on the hope of the glory of God.
Kwa imani yetu, yeye ametuleta katika hali hii ya neema ya Mungu ambamo sasa tunaishi. Basi, tunajivunia tumaini tulilo nalo la kushiriki utukufu wa Mungu.
3 And not only [so], but we also boast in the tribulations, knowing that the tribulation works endurance;
Naam, si hayo tu, bali tunafurahi pia katika taabu tukijua kwamba taabu huleta saburi,
4 and the endurance, experience; and the experience, hope;
nayo saburi huleta uthabiti, na uthabiti huleta tumaini.
5 and the hope does not make ashamed, because the love of God has been poured forth in our hearts through the Holy Spirit that has been given to us.
Tumaini hilo haliwezi kutuhadaa, maana Mungu amekwisha miminia mioyoni mwetu upendo wake kwa njia ya Roho Mtakatifu aliyetujalia.
6 For in our being still ailing, Christ in due time died for the impious;
Tulipokuwa bado wanyonge, Kristo, wakati ulipotimia, alikufa kwa ajili yetu sisi waovu.
7 for scarcely for a righteous man will anyone die, for the good man perhaps someone also dares to die;
Si rahisi mtu kufa kwa ajili ya mtu mwadilifu; labda mtu anaweza kuthubutu kufa kwa ajili ya mtu mwema.
8 and God commends His own love to us, that, in our being still sinners, Christ died for us;
Lakini Mungu amethibitisha kwamba anatupenda, maana wakati tulipokuwa bado wenye dhambi, Kristo alikufa kwa ajili yetu.
9 much more, then, having been declared righteous now in His blood, we will be saved through Him from the wrath;
Kwa kuwa sasa tumekubaliwa kuwa waadilifu kwa damu ya Kristo, ni dhahiri zaidi kwamba atatuokoa katika ghadhabu ya Mungu.
10 for if, being enemies, we have been reconciled to God through the death of His Son, much more, having been reconciled, we will be saved in His life.
Maana, tulipokuwa bado adui zake, Mungu alitupatanisha naye kwa kifo cha Mwanae. Na kwa vile sasa tumepatanishwa naye, ni dhahiri zaidi kwamba tutaokolewa kwa uzima wa Kristo.
11 And not only [so], but we are also boasting in God, through our Lord Jesus Christ, through whom we now received the reconciliation;
Wala si hayo tu, ila tunafurahi pia katika Mungu kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo ambaye ametupatanisha na Mungu.
12 because of this, even as through one man sin entered into the world, and through sin—death; and thus to all men death passed through, for that all sinned;
Kwa njia ya mtu mmoja dhambi iliingia ulimwenguni, nayo ikasababisha kifo. Hivyo kifo kimeenea katika jumuiya yote ya binadamu, kwa maana wote wametenda dhambi.
13 for until law sin was in the world: and sin is not reckoned when there is not law;
Kabla ya Sheria kuwako, dhambi ilikuwako ulimwenguni; lakini dhambi haiwekwi katika kumbukumbu bila sheria.
14 but death reigned from Adam until Moses, even on those having not sinned in the likeness of Adam’s transgression, who is a type of Him who is coming.
Lakini tangu wakati wa Adamu mpaka wakati wa Mose, kifo kiliwatawala hata wale ambao hawakutenda dhambi kama ile ya Adamu, ya kumwasi Mungu. Adamu alikuwa kielelezo cha yule ambaye atakuja baadaye.
15 But not as the offense so also [is] the free gift; for if by the offense of the one the many died, much more the grace of God, and the free gift in grace of the one man Jesus Christ, abound to the many;
Lakini ipo tofauti: neema ya Mungu si kama dhambi ya Adamu. Maana, ingawa dhambi ya mtu mmoja ilisababisha kifo kwa wote, kwa fadhili ya mtu mmoja, yaani Yesu Kristo, Mungu amewazidishia wote neema na zawadi zake.
16 and not as through one who sinned [is] the free gift, for the judgment indeed [is] of one to condemnation, but the gift [is] of many offenses to a declaration of “Righteous,”
Kuna tofauti baina ya zawadi ya Mungu, na dhambi ya mtu yule mmoja. Maana, baada ya kosa la mtu mmoja, Mungu alitoa hukumu; lakini baada ya makosa ya watu wengi, Mungu aliwapa zawadi yake kwa kuwasamehe.
17 for if by the offense of the one death reigned through the one, much more those who are receiving the abundance of grace and of the free gift of righteousness, in life will reign through the one—Jesus Christ.
Kweli, kwa dhambi ya mtu mmoja kifo kilianza kutawala kwa sababu ya huyo mtu mmoja; lakini, ni dhahiri zaidi kwamba alichokifanya yule mtu mmoja, yaani Yesu Kristo, ni bora zaidi. Wote wanaopokea neema na zawadi hiyo ya kukubaliwa kuwa waadilifu, watatawala katika uzima kwa njia ya huyo mmoja, yaani Yesu Kristo.
18 So, then, as through one offense to all men [it is] to condemnation, so also through one declaration of “Righteous” [it is] to all men to justification of life;
Basi, kama vile kosa la mtu mmoja lilivyoleta hukumu kwa binadamu wote, kadhalika kitendo kimoja kiadilifu kinawapa uhuru na uzima.
19 for as through the disobedience of the one man, the many were constituted sinners: so also through the obedience of the One, will the many be constituted righteous.
Na kama kwa kutotii kwa mtu mmoja watu wengi walifanywa wenye dhambi, kadhalika kutii kwa mtu mmoja kutawafanya wengi wakubaliwe kuwa waadilifu.
20 And law came in, that the offense might abound, and where sin abounded, grace hyper-abounded,
Sheria ilitokea, ikasababisha kuongezeka kwa uhalifu; lakini pale dhambi ilipoongezeka, neema iliongezeka zaidi.
21 that even as sin reigned in death, so also grace may reign, through righteousness, to continuous life, through Jesus Christ our Lord. (aiōnios g166)
Kama vile dhambi ilivyotawala kwa kifo, kadhalika neema inatawala kwa njia ya uadilifu, na kuleta uzima wa milele kwa njia ya Yesu Kristo Bwana wetu. (aiōnios g166)

< Romans 5 >