< 2 Chronicles 19 >
1 And Jehoshaphat king of Judah turns back to his house in peace, to Jerusalem,
Mfalme Yehoshafati wa Yuda akarudi salama kwenye jumba lake la kifalme huko Yerusalemu.
2 and Jehu son of Hanani the seer goes out to his presence and says to King Jehoshaphat, “Do you love to give help to the wicked and to those hating YHWH? And for this, wrath [is] against you from before YHWH,
Yehu mwonaji, mwana wa Hanani, akapanda kwenda kuonana naye akamwambia Mfalme Yehoshafati, “Je, utawasaidia waovu na kuwapenda wale wanaomchukia Bwana? Kwa sababu ya jambo hili, ghadhabu ya Bwana iko juu yako.
3 but good things have been found with you, for you have put away the Asheroth out of the land, and have prepared your heart to seek God.”
Hata hivyo, kuna mema yaliyoonekana kwako, kwa kuwa umeondoa katika nchi nguzo za Ashera na umeukaza moyo wako katika kumtafuta Mungu.”
4 And Jehoshaphat dwells in Jerusalem, and he turns back and goes out among the people from Beer-Sheba to the hill-country of Ephraim, and brings them back to YHWH, God of their fathers.
Yehoshafati aliishi huko Yerusalemu, naye akatoka akaenda tena miongoni mwa watu, kuanzia Beer-Sheba hadi nchi ya vilima ya Efraimu na kuwageuza wakamrudia Bwana, Mungu wa baba zao.
5 And he establishes judges in the land, in all the fortified cities of Judah, for every city,
Akawaweka waamuzi katika nchi, kwenye miji yote ya Yuda yenye maboma.
6 and says to the ones judging, “See what you are doing—for you do not judge for man, but for YHWH, who [is] with you in the matter of judgment;
Akawaambia, “Angalieni kwa makini yale mtendayo, kwa kuwa hamkuhukumu kwa ajili ya mwanadamu bali kwa ajili ya Bwana ambaye yu pamoja nanyi kila mtoapo hukumu.
7 and now, let fear of YHWH be on you, observe and do, for there is not perverseness with our God YHWH, and favoring by appearance, and taking of a bribe.”
Basi sasa hofu ya Bwana na iwe juu yenu. Hukumuni kwa uangalifu, kwa kuwa kwa Bwana Mungu wetu hakuna jambo lisilo la haki, upendeleo, wala rushwa.”
8 And also in Jerusalem, Jehoshaphat has appointed of the Levites, and of the priests, and of the heads of the fathers of Israel, for the judgment of YHWH, and for strife; and they return to Jerusalem,
Pia huko Yerusalemu, Yehoshafati akaweka baadhi ya Walawi, makuhani na viongozi wa jamaa za Waisraeli ili kutoa hukumu kwa ajili ya Bwana na kuamua magomvi. Nao waliishi huko Yerusalemu.
9 and he lays a charge on them, saying, “Thus do you do in the fear of YHWH, in faithfulness, and with a perfect heart,
Akawapa maagizo haya: “Ni lazima mtumike kwa uaminifu na kwa moyo wote katika kicho cha Bwana.
10 and any strife that comes to you of your brothers who are dwelling in their cities, between blood and blood, between law and command, statutes, and judgments, then you have warned them and they do not become guilty before YHWH, and wrath has not been on you and on your brothers; thus do you do, and you are not guilty.
Katika kila shauri lifikalo mbele yenu kutoka kwa ndugu zenu wale waishio katika miji, ikiwa ni la umwagaji wa damu au mambo mengine yahusuyo sheria, amri, hukumu au maagizo, inawapasa ninyi kuwaonya kwamba wasiingie katika hatia dhidi ya Bwana, la sivyo ghadhabu yake itakuja juu yenu na ndugu zenu. Tendeni hivyo, nanyi hamtatenda dhambi.
11 And behold, Amariah the head priest [is] over you for every matter of YHWH, and Zebadiah son of Ishmael, the leader of the house of Judah, [is] for every matter of the king, and the Levites [are] officers before you; be strong and do, and YHWH is with the good.”
“Amaria kuhani mkuu atakuwa juu yenu katika jambo lolote linalomhusu Bwana naye Zebadia mwana wa Ishmaeli, kiongozi wa kabila la Yuda, atakuwa juu yenu kwa jambo lolote linalomhusu mfalme, nao Walawi watatumika kama maafisa mbele yenu. Tendeni kwa ujasiri, naye Bwana atakuwa pamoja na wale watendao vyema.”