< 1 Samuel 27 >
1 And David says to his heart, “Now I am consumed by the hand of Saul one day; there is nothing better for me than that I diligently escape to the land of the Philistines, and Saul has been despairing of me—of seeking me anymore in all the border of Israel, and I have escaped out of his hand.”
Daudi alisema moyoni mwake, “Basi, siku moja nitaangamia kwa mkono wa Sauli; hakuna jambo zuri kwangu kuliko kutoroka hadi nchi ya Wafilisti; Sauli atakata tamaa asinitafute tena ndani ya mipaka yote ya Israeli; kwa njia hii nitaponyoka kutoka mkono wake.”
2 And David rises, and passes over, he and six hundred men who [are] with him, to Achish son of Maoch king of Gath;
Daudi akaondoka na kuvuka, akiwa pamoja na watu mia sita hadi kwa Akishi mwana wa Maoki, mfalme wa Gathi.
3 and David dwells with Achish in Gath, he and his men, each one with his household, [even] David and his two wives, Ahinoam the Jezreelitess, and Abigail wife of Nabal the Carmelitess.
Daudi akaishi na Akishi huko Gathi pamoja na watu wake, na kila mtu na familia yake, na Daudi akiwa na wake zake wawili, Ahinoamu Myezreeli, na Abigaili Mkarmeli aliyekuwa mke wa Nabali.
4 And it is declared to Saul that David has fled to Gath, and he has not added to seek him anymore.
Sauli akaambiwa kuwa Daudi amekimbilia Gathi, hivyo hakumtafuta tena.
5 And David says to Achish, “Now if I have found grace in your eyes, they give a place to me in one of the cities of the field, and I dwell there, indeed, why does your servant dwell in the royal city with you?”
Daudi akamwambia Akishi, “Kama nimepata kibali machoni pako, wanipatie mahali katika mojawapo ya miji ya nchi, ili nikae huko: kwa nini mtumishi wako akae pamoja na wewe katika mji wa kifalme?”
6 And Achish gives Ziklag to him in that day, therefore Ziklag has been for the kings of Judah until this day.
Hivyo siku hiyo Akishi akampa Daudi Ziklagi; ndiyo sababu mji wa Ziklagi ni mali ya wafalme wa Yuda hadi leo.
7 And the number of the days which David has dwelt in the field of the Philistines [is one year] of days and four months;
Idadi ya siku ambazo Daudi aliishi katika nchi ya Wafilisti ulikuwa mwaka mmoja na miezi minne.
8 and David and his men go up, and they push toward the Geshurite, and the Gerizite, and the Amalekite (for they are inhabitants of the land from of old), as you come to Shur and to the land of Egypt,
Daudi na watu wake walizipiga sehemu mbalimbali, wakiteka nyara Wageshuri, Wagirizi, na Waamaleki; kwa maana mataifa hayo ndio walikuwa wakaaji wa nchi, kwa uelekeo wa kwenda Shuri hadi kufika nchi ya Misri. Walikuwa wamekaa katika nchi hiyo toka nyakati za zamani.
9 and David has struck the land, and does not keep alive man and woman, and has taken sheep, and oxen, and donkeys, and camels, and garments, and turns back, and comes to Achish.
Daudi aliipiga nchi na hakumwacha mwanaume wala mwanamke akiwa hai; akatwaa kondoo, ng'ombe, punda, ngamia, na nguo; kisha alirudi na kufika tena kwa Akishi.
10 And Achish says, “To where have you pushed today?” And David says, “Against the south of Judah, and against the south of the Jerahmeelite, and to the south of the Kenite.”
Ndipo Akishi humuuliza, “Je, leo umefanya mashambulizi dhidi ya nani?” Daudi humjibu, “Nimefanya dhidi ya kusini mwa Yuda,” au dhidi ya kusini mwa Wayerameeli,” au “dhidi ya kusini mwa Wakeni.”
11 David keeps alive neither man nor woman, to bring in [word] to Gath, saying, “Lest they declare [it] against us, saying, Thus David has done, and thus [is] his custom all the days that he has dwelt in the fields of the Philistines.”
Daudi asingemwacha mwanaume wala mwanamke akiwa hai awalete hadi Gathi, akisema, “ili wasije kututeta, 'Daudi amefanya hivi na vile.”' Hivi ndivyo alivyofanya kwa kipindi chote alichokaa katika nchi ya Wafilisti.
12 And Achish believes in David, saying, “He has made himself utterly abhorred among his people in Israel, and has been for a perpetual servant to me.”
Akishi alimwamini Daudi, akisema, “Amesababisha watu wake Israeli wamchukie kabisa; kwa hiyo atakuwa mtumishi wangu milele.”