< 1 Corinthians 3 >
1 And I, brothers, was not able to speak to you as to spiritual, but as to fleshly—as to babies in Christ;
Na mimi, kaka na dada zangu, sikusema nanyi kama watu kiroho, lakini kama na watu wa kimwili. Kama na watoto wadogo katika Kristo.
2 with milk I fed you, and not with meat, for you were not yet able, but not even yet are you now able,
Niliwanywesha maziwa na si nyama, kwa kuwa hamkuwa tayari kwa kula nyama. Na hata sasa hamjawa tayari.
3 for yet you are fleshly, for where [there is] among you envying, and strife, and divisions, are you not fleshly, and walk in the manner of men?
Kwa kuwa ninyi bado ni wa mwilini. Kwa kuwa wivu na majivuno yanaonekana miongoni mwenu. Je, hamuishi kulingana na mwili, na je, hamtembei kama kawaida ya kibinadamu?
4 For when one may say, “I, indeed, am of Paul,” and another, “I—of Apollos,” are you not fleshly?
Kwa kuwa mmoja husema, “Namfuata Paulo” Mwingine husema “Namfuata Apolo,” hamuishi kama wanadamu?
5 Who, then, is Paul, and who Apollos, but servants through whom you believed, and to each as the LORD gave?
Apolo ni nani? na Paulo ni nani? Watumishi wa yule mliyemwamini, kwa kila ambaye Bwana alimpa jukumu.
6 I planted, Apollos watered, but God was giving growth;
Mimi nilipanda, Apolo akatia maji, lakini Mungu akakuza.
7 so that neither is he who is planting anything, nor he who is watering, but He who is giving growth—God;
Kwa hiyo, si aliye panda wala aliyetia maji ana chochote. Lakini ni Mungu anayekuza.
8 and he who is planting and he who is watering are one, and each will receive his own reward according to his own labor,
Sasa apandaye na atiaye maji wote ni sawa, na kila mmoja atapokea ujira wake kulingana na kazi yake.
9 for we are fellow-workmen of God; you are God’s tillage, God’s building.
Kwa kuwa sisi tu watendakazi wa Mungu, ninyi ni bustani ya Mungu, jengo la Mungu.
10 According to the grace of God that was given to me, as a wise master-builder, I have laid a foundation, and another builds on [it],
Kutokana na neema ya Mungu niliyopewa kama mjenzi mkuu, niliuweka msingi, na mwingine anajenga juu yake. Lakini mtu awe makini jinsi ajengavyo juu yake.
11 for no one is able to lay another foundation except that which is laid, which is Jesus the Christ;
Kwa kuwa hakuna mwingine awezaye kujenga msingi mwingine zaidi ya uliojengwa, ambao ni Yesu Kristo.
12 and if anyone builds on this foundation gold, silver, precious stones, wood, hay, straw—
Sasa, kama mmoja wenu ajenga juu yake kwa dhahabu, fedha, mawe ya thamani, miti, nyasi, au majani,
13 the work will become visible of each, for the day will declare [it], because it is revealed in fire, and the work of each, what kind it is, the fire will prove;
kazi yake itafunuliwa, kwa mwanga wa mchana utaidhihirisha. Kwa kuwa itadhihirishwa na moto. Moto utajaribu ubora wa kazi wa kila mmoja alichofanya.
14 if the work of anyone remains that he built on [it], he will receive a wage;
Kama chochote mtu alichojenga kitabaki, yeye atapokea zawadi.
15 if the work of any is burned up, he will suffer loss, but himself will be saved, but so as through fire.
Lakini kama kazi ya mtu ikiteketea kwa moto, atapata hasara. Lakini yeye mwenyewe ataokolewa, kama vile kuepuka katika moto.
16 Have you not known that you are a temple of God, and the Spirit of God dwells in you?
Hamjui kuwa ninyi ni hekalu la Mungu na kwamba Roho wa Mungu anakaa ndani yenu?
17 If anyone ruins the temple of God, God will ruin him; for the temple of God is holy, which you are.
Kama mtu akiliharibu hekalu la Mungu, Mungu atamharibu mtu yule. Kwa kuwa hekalu la Mungu ni takatifu, na hivyo na ninyi.
18 Let no one deceive himself; if anyone seems to be wise among you in this age—let him become a fool, that he may become wise, (aiōn )
Mtu asijidanganye mwenyewe, kama yeyote miongoni mwenu anadhani ana hekima katika nyakati hizi, awe kama “mjinga” ndipo atakuwa na hekima. (aiōn )
19 for the wisdom of this world is foolishness with God, for it has been written: “Who is taking the wise in their craftiness”;
Kwa kuwa hekima ya dunia hii ni ujinga mbele za Mungu, Kwa kuwa imeandikwa, “Huwanasa wenye hekima kwa hila zao”
20 and again, “The LORD knows the reasonings of the wise, that they are vain.”
Na tena “Bwana anajua mawazo ya wenye busara ni ubatili.”
21 So then, let no one glory in men, for all things are yours,
Hivyo mtu asijivunie wanadamu! Kwa kuwa vitu vyote ni vyenu.
22 whether Paul, or Apollos, or Cephas, or the world, or life, or death, or things present, or things about to be—all are yours,
Kama ni Paulo, au Apolo, au Kefa, au dunia, au maisha, au kifo, au vitu vilivyopo, au vitakavyokuwepo. Vyote ni vyenu,
23 and you [are] Christ’s, and Christ [is] God’s.
na ninyi ni wa Kristo na Kristo ni wa Mungu.