< Revelation 3 >
1 And to the angel of the church in Sardis write; These things says he that has the seven Spirits of God, and the seven stars; I know your works, that you have a name that you live, and are dead.
Kwa malaika wa kanisa la Sardi andika: 'Maneno ya yule anayeshikilia zile roho saba za Mungu na nyota saba. “Najua ambacho umefanya. Una sifa ya kuwa hai, lakini u-mfu.
2 Be watchful, and strengthen the things which remain, that are ready to die: for I have not found your works perfect before God.
Amka na kuimarisha yaliyosalia, lakini yako karibu kufa, kwa sababu sikuyaona matendo yako yamekamilika machoni pa Mungu wangu.
3 Remember therefore how you have received and heard, and hold fast, and repent. If therefore you shall not watch, I will come on you as a thief, and you shall not know what hour I will come on you.
Kwa hiyo, kumbuka, yale uliyoyapokea na kusikia. Yatii na kutubu. Lakini usipoamka, nitakuja kama mwivi, na hutajua saa ipi nitakayokuja juu yako.
4 You have a few names even in Sardis which have not defiled their garments; and they shall walk with me in white: for they are worthy.
Lakini kuna majina machache ya watu katika Sardi ambao hawakuchafua nguo zao. Watatembea pamoja nami, wamevaa nguo nyeupe, kwa sababu wanastahili.
5 He that overcomes, the same shall be clothed in white raiment; and I will not blot out his name out of the book of life, but I will confess his name before my Father, and before his angels.
Yeye ashindaye atavikwa mavazi meupe, na kamwe sitalifuta jina lake kutoka katika kitabu cha uzima, na nitalitaja jina lake mbele ya Baba yangu, na mbele ya malaika.
6 He that has an ear, let him hear what the Spirit says to the churches.
Ukiwa na sikio, sikiliza Roho ayaambiavyo makanisa.”
7 And to the angel of the church in Philadelphia write; These things says he that is holy, he that is true, he that has the key of David, he that opens, and no man shuts; and shuts, and no man opens;
“Kwa malaika wa kanisa la Philadefia andika: Maneno ya aliye mtakatifu na kweli - aliye na funguo za Daudi, hufungua na hakuna afungaye, hufunga na hakuna awezaye kufungua.
8 I know your works: behold, I have set before you an open door, and no man can shut it: for you have a little strength, and have kept my word, and have not denied my name.
Najua ambacho umetenda. Tazama, nimekuwekea mbele yako mlango uliofunguliwa ambao hakuna awezaye kuufunga. Najua unazo nguvu kidogo, lakini umelitii neno langu na hujalikana jina langu.
9 Behold, I will make them of the synagogue of Satan, which say they are Jews, and are not, but do lie; behold, I will make them to come and worship before your feet, and to know that I have loved you.
Angalia! Wote walio wa sinagogi la shetani, wale wasemao wao ni Wayahudi na kumbe siyo, badala yake wanadanganya. Nitawafanya waje na kusujudu mbele ya miguu yako, na watajua ya kuwa nilikupenda.
10 Because you have kept the word of my patience, I also will keep you from the hour of temptation, which shall come on all the world, to try them that dwell on the earth.
Kwa kuwa umetunza amri yangu kwa uvumilivu wa uthabiti, nitakulinda pia katika saa yako ya kujaribiwa ambayo inakuja katika ulimwengu wote, kuwajaribu wale wote wanaoishi katika nchi.
11 Behold, I come quickly: hold that fast which you have, that no man take your crown.
Naja upesi. Shikilia sana kile ulichonacho ili asiwepo mtu wa kuitwaa taji yako.
12 Him that overcomes will I make a pillar in the temple of my God, and he shall go no more out: and I will write on him the name of my God, and the name of the city of my God, which is new Jerusalem, which comes down out of heaven from my God: and I will write on him my new name.
Nitamfanya yeye ashindaye kuwa nguzo katika hekalu la Mungu wangu, na hatatoka nje kamwe. Nitaliandika kwake jina la Mungu wangu, jina la mji wa Mungu wangu (Yerusalemu mpya, ushukao chini toka mbinguni kwa Mungu wangu), na jina langu jipya.
13 He that has an ear, let him hear what the Spirit says to the churches.
Yeye aliye na sikio, na asikie ambacho Roho anasema kwa makanisa.'
14 And to the angel of the church of the Laodiceans write; These things says the Amen, the faithful and true witness, the beginning of the creation of God;
“Kwa malaika wa kanisa la Laodikia andika: 'Maneno yake aliye Amina, wakutegemewa na shahidi mwaminifu, mtawala juu ya uumbaji wa Mungu.
15 I know your works, that you are neither cold nor hot: I would you were cold or hot.
Najua ambacho umefanya, na kwamba wewe si baridi wala moto, natamani kwamba ungekuwa wa baridi au moto!
16 So then because you are lukewarm, and neither cold nor hot, I will spew you out of my mouth.
Hivyo, kwa sababu wewe ni vuguvugu, si moto wala baridi, nitakutapika utoke kinywani mwangu.
17 Because you say, I am rich, and increased with goods, and have need of nothing; and know not that you are wretched, and miserable, and poor, and blind, and naked:
Kwa kuwa unasema, “Mimi ni tajiri, nimekuwa na mali nyingi, na sihitaji chochote.” Lakini hujui kwamba wewe ni duni sana, wakuhuzunikiwa, maskini, kipofu na uchi.
18 I counsel you to buy of me gold tried in the fire, that you may be rich; and white raiment, that you may be clothed, and that the shame of your nakedness do not appear; and anoint your eyes with eye salve, that you may see.
Sikiliza ushauri kwangu: Nunua kwangu dhahabu iliyosafishwa kwa moto ili upate kuwa tajiri, na nguo nyeupe za kumetameta ili ujivike mwenyewe na usioneshe aibu ya uchi wako, na mafuta ya kupaka katika macho yako upate kuona.
19 As many as I love, I rebuke and chasten: be zealous therefore, and repent.
Kila nimpendaye, namwelekeza na kuwafundisha namna iwapasavyo kuishi; kwa hiyo, kuwa mkweli na kutubu.
20 Behold, I stand at the door, and knock: if any man hear my voice, and open the door, I will come in to him, and will sup with him, and he with me.
Tazama nasimama katika mlango na kubisha. Yeyote asikiaye sauti yangu na kufungua mlango, nitakuja na kuingia nyumbani kwake, na kula chakula naye na yeye pamoja nami.
21 To him that overcomes will I grant to sit with me in my throne, even as I also overcame, and am set down with my Father in his throne.
Yeye ashindaye, nitampa haki ya kukaa chini pamoja nami juu ya kiti changu cha enzi, kama vile mimi nilivyoshinda na kukaa chini pamoja na Baba yangu juu ya kiti chake cha enzi.
22 He that has an ear, let him hear what the Spirit says to the churches.
Yeye aliye na sikio, na asikilize ambacho Roho ayaambia makanisa.”