< Psalms 54 >

1 Save me, O God, by your name, and judge me by your strength.
Uniokoe, Mungu, kwa jina lako, na kwa nguvu zako unihukumu.
2 Hear my prayer, O God; give ear to the words of my mouth.
Usikie maombi yangu, Mungu; uyategee sikio maneno ya mdomo wangu.
3 For strangers are risen up against me, and oppressors seek after my soul: they have not set God before them. (Selah)
Kwa maana wageni wameinuka dhidi yangu, na watu wasio na huruma wanaitafuta roho yangu; nao hawakumuweka Mungu mbele yao. (Selah)
4 Behold, God is my helper: the Lord is with them that uphold my soul.
Tazama, Mungu ni msaidizi wangu; Bwana ndiye anisaidiaye.
5 He shall reward evil to my enemies: cut them off in your truth.
Naye atawalipizia uovu maadui zangu; katika uaminifu wako, uwaharibu!
6 I will freely sacrifice to you: I will praise your name, O LORD; for it is good.
Nitakutolea dhabihu kwa moyo mkunjufu; nitalishukuru jina lako, Yahwe, kwa maana ni jema.
7 For he has delivered me out of all trouble: and my eye has seen his desire on my enemies.
Kwa kuwa yeye ameniokoa katika kila shida; macho yangu yamewatazama adui zangu yakiwa na ushindi.

< Psalms 54 >