< Psalms 17 >
1 A Prayer of David. Hear the right, O LORD, attend unto my cry; give ear unto my prayer from lips without deceit.
Sala ya Daudi. Sikia, Ee Bwana, kusihi kwangu kwa haki, sikiliza kilio changu. Tega sikio kwa ombi langu, halitoki kwenye midomo ya udanganyifu.
2 Let my judgment come forth from Thy presence; let Thine eyes behold equity.
Hukumu yangu na itoke kwako, macho yako na yaone yale yaliyo haki.
3 Thou hast tried my heart, Thou hast visited it in the night; Thou hast tested me, and Thou findest not that I had a thought which should not pass my mouth.
Ingawa unauchunguza moyo wangu na kunikagua usiku, ingawa umenijaribu, hutaona chochote. Nimeamua kwamba kinywa changu hakitatenda dhambi.
4 As for the doings of men, by the word of Thy lips I have kept me from the ways of the violent.
Kuhusu matendo ya wanadamu: kwa neno la midomo yako, nimejiepusha na njia za wenye jeuri.
5 My steps have held fast to Thy paths, my feet have not slipped.
Hatua zangu zimeshikamana na njia zako; nyayo zangu hazikuteleza.
6 As for me, I call upon Thee, for Thou wilt answer me, O God; incline Thine ear unto me, hear my speech.
Ee Mungu, ninakuita, kwa kuwa utanijibu, nitegee sikio lako na usikie ombi langu.
7 Make passing great Thy mercies, O Thou that savest by Thy right hand from assailants them that take refuge in Thee.
Uonyeshe ajabu ya upendo wako mkuu, wewe uokoaye kwa mkono wako wa kuume wale wanaokukimbilia kutokana na adui zao.
8 Keep me as the apple of the eye, hide me in the shadow of Thy wings,
Nilinde kama mboni ya jicho lako, unifiche chini ya kivuli cha mbawa zako
9 From the wicked that oppress, my deadly enemies, that compass me about.
kutokana na waovu wanaonishambulia, kutokana na adui wauaji wanaonizunguka.
10 Their gross heart they have shut tight, with their mouth they speak proudly.
Huifunga mioyo yao iliyo migumu, vinywa vyao hunena kwa majivuno.
11 At our every step they have now encompassed us; they set their eyes to cast us down to the earth.
Wamenifuatia nyayo zangu, sasa wamenizingira, wakiwa macho, waniangushe chini.
12 He is like a lion that is eager to tear in pieces, and like a young lion lurking in secret places.
Wamefanana na simba mwenye njaa awindaye, kama simba mkubwa anyemeleaye mafichoni.
13 Arise, O LORD, confront him, cast him down; deliver my soul from the wicked, by Thy sword;
Inuka, Ee Bwana, pambana nao, uwaangushe, niokoe kutokana na waovu kwa upanga wako.
14 From men, by Thy hand, O LORD, from men of the world, whose portion is in this life, and whose belly Thou fillest with Thy treasure; who have children in plenty, and leave their abundance to their babes.
Ee Bwana, mkono wako uniokoe na watu wa jinsi hii, kutokana na watu wa ulimwengu huu ambao fungu lao liko katika maisha haya. Na wapate adhabu ya kuwatosha. Watoto wao na wapate zaidi ya hayo, hukumu na iendelee kwa watoto wa watoto wao.
15 As for me, I shall behold Thy face in righteousness; I shall be satisfied, when I awake, with Thy likeness.
Na mimi katika haki nitauona uso wako, niamkapo, nitaridhika kwa kuona sura yako.