< Jonah 4 >

1 But it displeased Jonah exceedingly, and he was angry.
Lakini Yona alichukizwa sana akakasirika.
2 And he prayed unto the LORD, and said: 'I pray Thee, O LORD, was not this my saying, when I was yet in mine own country? Therefore I fled beforehand unto Tarshish; for I knew that Thou art a gracious God, and compassionate, long-suffering, and abundant in mercy, and repentest Thee of the evil.
Akamwomba Bwana, “Ee Bwana, hili si lile nililolisema nilipokuwa ningali nyumbani? Hii ndiyo sababu niliharikisha kukimbilia Tarshishi. Nikifahamu kuwa wewe ni Mungu mwenye neema na huruma, si mwepesi wa hasira na umejaa upendo, ni Mungu ambaye hughairi katika kupeleka maafa.
3 Therefore now, O LORD, take, I beseech Thee, my life from me; for it is better for me to die than to live.'
Sasa, Ee Bwana, niondolee uhai wangu, kwa kuwa ni afadhali mimi nife kuliko kuishi.”
4 And the LORD said: 'Art thou greatly angry?'
Lakini Bwana akamjibu, “Je unayo haki yoyote kukasirika?”
5 Then Jonah went out of the city, and sat on the east side of the city, and there made him a booth, and sat under it in the shadow, till he might see what would become of the city.
Yona akatoka nje akaketi mahali upande wa mashariki wa mji. Hapo akajitengenezea kibanda, akaketi kwenye kivuli chake na kungojea ni nini kitakachotokea katika mji.
6 And the LORD God prepared a gourd, and made it to come up over Jonah, that it might be a shadow over his head, to deliver him from his evil. So Jonah was exceeding glad because of the gourd.
Ndipo Bwana, Mungu akaweka tayari mzabibu na kuufanya uote, kumpa Yona kivuli kilichomfunika kichwa ili kuondoa taabu yake, naye Yona akafurahi sana kwa ajili ya ule mzabibu.
7 But God prepared a worm when the morning rose the next day, and it smote the gourd, that it withered.
Lakini kesho yake asubuhi na mapema Mungu akaamuru buu, autafune mzabibu huo nao ukanyauka.
8 And it came to pass, when the sun arose, that God prepared a vehement east wind; and the sun beat upon the head of Jonah, that he fainted, and requested for himself that he might die, and said: 'It is better for me to die than to live.'
Wakati jua lilipochomoza, Mungu akautuma upepo wa hari wa mashariki, nalo jua likawaka juu ya kichwa cha Yona mpaka akazimia. Akatamani kufa, naye akasema, “Ni afadhali mimi nife kuliko kuishi.”
9 And God said to Jonah: 'Art thou greatly angry for the gourd?' And he said: 'I am greatly angry, even unto death.'
Lakini Mungu alimwambia Yona, “Je, unayo haki kukasirika kuhusu mzabibu huo?” Akasema, “Ndiyo, ninayo haki. Nimekasirika kiasi cha kufa.”
10 And the LORD said: 'Thou hast had pity on the gourd, for which thou hast not laboured, neither madest it grow, which came up in a night, and perished in a night;
Lakini Bwana akamwambia, “Wewe unakasirika kwa ajili ya mzabibu huu, nawe hukuusababisha kuota wala kuutunza. Uliota usiku mmoja, nao ukafa usiku mmoja.
11 and should not I have pity on Nineveh, that great city, wherein are more than sixscore thousand persons that cannot discern between their right hand and their left hand, and also much cattle?'
Lakini Ninawi ina zaidi ya watu 120,000 ambao hawawezi kupambanua kulia au kushoto, pamoja na ngʼombe wengi. Je, hainipasi kufikiri juu ya mji ule mkubwa?”

< Jonah 4 >