< Revelation 11 >
1 Then was giuen me a reede, like vnto a rod, and the Angel stoode by, saying, Rise and mete the Temple of God, and the altar, and them that worship therein.
Ndipo nikapewa mwanzi uliokuwa kama ufito wa kupimia, nikaambiwa, “Nenda ukapime hekalu la Mungu pamoja na madhabahu, nawe uwahesabu wale waabuduo humo.
2 But the court which is without the temple cast out, and mete it not: for it is giuen vnto the Gentiles, and the holy citie shall they treade vnder foote, two and fourtie moneths.
Lakini usiupime ua wa nje wa Hekalu, uache, kwa sababu ua huo wamepewa watu wa Mataifa. Hao wataukanyagakanyaga mji mtakatifu kwa muda wa miezi arobaini na miwili.
3 But I wil giue power vnto my two witnesses, and they shall prophecie a thousande two hundreth and threescore dayes, clothed in sackcloth.
Nami nitawapa mashahidi wangu wawili uwezo, nao watoe unabii kwa muda wa siku 1,260, wakiwa wamevaa nguo za gunia.”
4 These are two oliue trees, and two candlestickes, standing before the God of the earth.
Hawa ndio ile mizeituni miwili na vile vinara viwili vya taa visimamavyo mbele za Bwana Mungu wa dunia yote.
5 And if any man wil hurt them, fire proceedeth out of their mouthes, and deuoureth their enemies: for if any man would hurt the, thus must he be killed.
Kama mtu yeyote akitaka kuwadhuru, moto hutoka vinywani mwao na kuwateketeza adui zao. Hivi ndivyo impasavyo kufa mtu yeyote atakayetaka kuwadhuru.
6 These haue power to shut heauen, that it raine not in the dayes of their prophecying, and haue power ouer waters to turne them into blood, and to smite the earth with all maner plagues, as often as they will.
Watu hawa wanao uwezo wa kufunga anga ili mvua isinyeshe wakati wote watakapokuwa wanatoa unabii wao. Nao watakuwa na uwezo wa kuyabadili maji kuwa damu na kuipiga dunia kwa kila aina ya mapigo mara kwa mara kama watakavyo.
7 And when they haue finished their testimonie, the beast that commeth out of the bottomlesse pit, shall make warre against them, and shall ouercome them, and kill them. (Abyssos )
Basi watakapokuwa wamemaliza ushuhuda wao, yule mnyama atokaye katika lile Shimo atapigana nao vita, atawashinda na kuwaua. (Abyssos )
8 And their corpses shall lie in the streetes of the great citie, which spiritually is called Sodom and Egypt, where our Lord also was crucified.
Maiti zao zitabaki katika barabara ya mji mkubwa, ambao kwa fumbo unaitwa Sodoma na Misri, ambapo pia Bwana wao alisulubiwa.
9 And they of the people and kinreds, and tongues, and Gentiles shall see their corpses three dayes and an halfe, and shall not suffer their carkeises to be put in graues.
Kwa muda wa siku tatu na nusu, watu wa kila kabila, jamaa, lugha na taifa wataziangalia hizo maiti zao na hawataruhusu wazikwe.
10 And they that dwell vpon the earth, shall reioyce ouer them and be glad, and shall sende giftes one to an other: for these two Prophets vexed them that dwelt on the earth.
Watu waishio duniani watazitazama kwa furaha maiti za hao manabii wawili na kushangilia kwa kupeana zawadi kwa sababu hao manabii waliwatesa watu waishio duniani.
11 But after three dayes and an halfe, the spirit of life comming from God, shall enter into them, and they shall stande vp vpon their feete: and great feare shall come vpon them which sawe them.
Lakini baada ya zile siku tatu na nusu, pumzi ya uhai kutoka kwa Mungu ikawaingia, nao wakasimama kwa miguu yao na wote waliowaona wakaingiwa na hofu kuu.
12 And they shall heare a great voyce from heauen, saying vnto them, Come vp hither. And they shall ascend vp to heauen in a cloude, and their enemies shall see them.
Kisha wale manabii wawili wakasikia sauti kuu kutoka mbinguni ikiwaambia, “Njooni huku juu!” Nao wakapaa mbinguni katika wingu, wakati adui zao wakiwa wanawatazama.
13 And the same houre shall there bee a great earthquake, and the tenth part of the citie shall fall, and in the earthquake shalbe slaine in nomber seuen thousande: and the remnant were sore feared, and gaue glorie to the God of heauen.
Saa iyo hiyo, kukatokea tetemeko kubwa la nchi na sehemu ya kumi ya mji ikaanguka. Watu elfu saba wakauawa katika tetemeko hilo, nao walionusurika wakaogopa sana, wakamtukuza Mungu wa mbinguni.
14 The second woe is past, and beholde, the third woe will come anon.
Ole ya pili imekwisha kupita, tazama ole ya tatu inakuja upesi.
15 And the seuenth Angell blewe the trumpet, and there were great voyces in heauen, saying, The kingdomes of this worlde are our Lordes, and his Christes, and he shall reigne for euermore. (aiōn )
Yule malaika wa saba akaipiga tarumbeta yake, pakawa na sauti kubwa mbinguni iliyosema: “Ufalme wa ulimwengu umekuwa ufalme wa Bwana wetu na wa Kristo wake, naye atatawala milele na milele.” (aiōn )
16 Then the foure and twentie Elders, which sate before God on their seates, fell vpon their faces, and worshipped God,
Nao wale wazee ishirini na wanne, waliokuwa wameketi mbele za Mungu, kwenye viti vyao vya enzi, wakaanguka kifudifudi, wakamwabudu Mungu,
17 Saying, We giue thee thankes, Lord God almightie, Which art, and Which wast, and Which art to come: for thou hast receiued thy great might, and hast obteined thy kingdome.
wakisema: “Tunakushukuru, Bwana Mungu Mwenyezi, uliyeko na uliyekuwako, kwa kuwa umetwaa uweza wako mkuu na ukaanza kutawala.
18 And the Gentiles were angrie, and thy wrath is come, and the time of the dead, that they shoulde be iudged, and that thou shouldest giue reward vnto thy seruants the Prophets, and to the Saintes, and to them that feare thy Name, to small and great, and shouldest destroy them, which destroy the earth.
Mataifa walikasirika nao wakati wa ghadhabu yako umewadia. Wakati umewadia wa kuwahukumu waliokufa na kuwapa thawabu watumishi wako manabii na watakatifu wako pamoja na wale wote wanaoliheshimu Jina lako, wakubwa kwa wadogo: na kuwaangamiza wale wanaoiangamiza dunia.”
19 Then the Temple of God was opened in heauen, and there was seene in his Temple the Arke of his couenant: and there were lightnings, and voyces, and thundrings, and earthquake, and much haile.
Ndipo hekalu la Mungu lililoko mbinguni likafunguliwa, na sanduku la agano lake likaonekana humo ndani. Kukatokea mianga ya umeme wa radi, ngurumo, sauti za radi, tetemeko la nchi na mvua kubwa ya mawe.