< 2 Corinthians 12 >
1 It is not expedient for me no doubt to reioyce: for I will come to visions and reuelations of the Lord.
Ni lazima nijivune, lakini hakuna kinachoongezwa na hilo. Bali nitaendelea kwenye maono na mafunuo kutoka kwa Bwana.
2 I know a man in Christ aboue fourteene yeeres agone, (whether he were in the body, I can not tell, or out of the body, I can not tell: God knoweth) which was taken vp into the thirde heauen.
Namjua mtu mmoja katika Kristo ambaye miaka kumi na minne iliyopita ambaye—ikiwa katika mwili, au nje ya mwili, mimi sijui, Mungu anajua—alinyakuliwa juu katika mbingu ya tatu.
3 And I knowe such a man (whether in the body, or out of the body, I can not tell: God knoweth)
Na ninajua kwamba mtu huyu—ikiwa katika mwili, au nje ya mwili, mimi sijui, Mungu anajua—
4 How that he was taken vp into Paradise, and heard words which cannot be spoken, which are not possible for man to vtter.
alichukuliwa juu hadi paradiso na kusikia mambo matakatifu sana kwa mtu yeyote kuyasema.
5 Of such a man will I reioyce: of my selfe will I not reioyce, except it bee of mine infirmities.
Kwa niaba ya mtu kama huyo nitajivuna. lakini kwa niaba yangu mwenyewe sitajivuna. Isipokuwa kuhusu udhaifu wangu.
6 For though I woulde reioyce, I should not be a foole, for I will say the trueth: but I refraine, lest any man should thinke of me aboue that hee seeth in me, or that he heareth of me.
Kama nikitaka kujivuna, nisingekuwa mpumbavu, kwa kuwa ningekuwa ninazungumza ukweli. Lakini nitaacha kujivuna, ili kwamba asiwepo yeyote atakayenifikiria zaidi ya hayo kuliko kinachoonekana ndani yangu au kusikika kutoka kwangu.
7 And lest I should be exalted out of measure through the aboundance of reuelations, there was giuen vnto me a pricke in the flesh, the messenger of Satan to buffet mee, because I should not be exalted out of measure.
Sitajivuna pia kwa sababu ya hayo mafunuo ya aina ya ajabu. Kwa hiyo, hivyo sitajawa na kiburi, mwiba uliwekwa ndani ya mwili wangu, mjumbe wa shetani kunishambulia mimi, ili nisigeuke kuwa mwenye majivuno.
8 For this thing I besought the Lord thrise, that it might depart from me.
Mara tatu nilimsihi Bwana kuhusu hili, ili yeye kuundoa kutoka kwangu.
9 And he said vnto me, My grace is sufficient for thee: for my power is made perfect through weakenesse. Very gladly therefore will I reioyce rather in mine infirmities, that the power of Christ may dwell in me.
Naye akaniambia, “Neema yangu inatosha kwa ajili yako, kwa kuwa nguvu hufanywa kamili katika udhaifu. Hivyo, ningetamani zaidi kujivuna zaidi kuhusu udhaifu wangu, ili kwamba uwezo wa Kristo uweze kukaa juu yangu.
10 Therefore I take pleasure in infirmities, in reproches, in necessities, in persecutions, in anguish for Christes sake: for when I am weake, then am I strong.
Kwa hiyo ninatosheka kwa ajili ya Kristo, katika udhaifu, katika matukano, katika shida, katika mateso, katika hali ya masikitiko. Kwa kuwa wakati nikiwa dhaifu, kisha nina nguvu.
11 I was a foole to boast my selfe: yee haue compelled mee: for I ought to haue bene commended of you: for in nothing was I inferiour vnto the very chiefe Apostles, though I bee nothing.
Mimi nimekuwa mpumbavu! ninyi mlinilazimisha kwa hili, kwa kuwa ningekuwa nimesifiwa na ninyi. Kwa kuwa sikuwa duni kabisa kwa hao waitwao mitume—bora, hata kama mimi si kitu.
12 The signes of an Apostle were wrought among you with all patience, with signes, and wonders, and great workes.
Ishara za kweli za mtume zilifanyika katikati yenu kwa uvumilivu, ishara na maajabu na matendo makuu.
13 For what is it, wherein yee were inferiours vnto other Churches, except that I haue not bene slouthfull to your hinderance? forgiue me this wrong.
Kwa namna gani mlikuwa wa muhimu wa chini kuliko makanisa yaliyobaki, isipokuwa kwamba sikuwa mzigo kwenu? Mnisamehe kwa kosa hili!
14 Behold, the thirde time I am ready to come vnto you, and yet will I not be slouthfull to your hinderance: for I seeke not yours, but you: for the children ought not to laye vp for the fathers, but the fathers for the children.
Tazama! mimi niko tayari kuja kwenu kwa mara ya tatu. Sitakuwa mzigo kwenu, kwa kuwa sitaki kitu kilicho chenu. Nawataka ninyi. Kwa kuwa watoto hawapaswi kuweka akiba kwa ajili ya wazazi. Badala yake, wazazi wanapaswa kuweka akiba kwa ajili ya watoto.
15 And I will most gladly bestow, and will be bestowed for your soules: though the more I loue you, the lesse I am loued.
Nitafurahi zaidi kutumia na kutumiwa kwa ajili ya nafsi zenu. Kama ninawapenda zaidi, natakiwa kupendwa kidogo?
16 But bee it that I charged you not: yet for as much as I was craftie, I tooke you with guile.
Lakini kama ilivyo, sikuwalemea mzigo ninyi. Lakini kwa kuwa mimi ni mwerevu sana, mimi ni yule aliyewashika ninyi kwa nimekuwa ambaye aliyewapata kwa udanganyifu.
17 Did I pill you by any of them whom I sent vnto you?
Je, nilichukua kwa kujifanyia faida kwa yeyote niliyemtuma kwenu?
18 I haue desired Titus, and with him I haue sent a brother: did Titus pill you of any thing? walked we not in the selfe same spirit? walked we not in the same steppes?
Nilimsihi Tito kuja kwenu, na nilituma ndugu mwingine pamoja naye. Je, Tito aliwafanyia faida ninyi? Je, hatukutembea katika njia ile ile? Je, hatukutembea katika nyayo zile zile?
19 Againe, thinke yee that wee excuse our selues vnto you? we speake before God in Christ. But wee doe all thinges, dearely beloued, for your edifying.
Mnadhani kwa muda huu wote tumekuwa tukijitetea sisi wenyewe kwenu? Mbele za Mungu, na katika Kristo, tumekuwa tukisema kila kitu kwa ajili ya kuwaimarisha ninyi.
20 For I feare least when I come, I shall not finde you such as I would: and that I shalbe found vnto you such as ye woulde not, and least there be strife, enuying, wrath, contentions, backebitings, whisperings, swellings and discord.
Kwa kuwa nina hofu kwamba nitakapokuja naweza nisiwapate ninyi kama ninavyotamani. Nina hofu kwamba mnaweza msinipate mimi kama mnavyotamani. Nahofia kwamba kunaweza kuwa na majadiliano, wivu, milipuko ya hasira, tamaa ya ubinafsi, umbeya, kiburi, na ugomvi.
21 I feare least when I come againe, my God abase me among you, and I shall bewaile many of them which haue sinned already, and haue not repented of the vncleannesse, and fornication, and wantonnesse which they haue committed.
Nina hofu kwamba nitakaporudi tena, Mungu wangu anaweza kuninyenyekeza mbele yenu. Nina hofu kwamba ninaweza kuhuzunishwa na wengi ambao wamefanya dhambi kabla ya sasa, na ambao hawakutubu uchafu, na uasherati na mambo ya tamaa wanayoyatenda.