< Ezekiel 42 >

1 The man took me out through the north gate to the outer courtyard into the rooms on the far side of the Temple courtyard by the northern external wall.
Kisha yule mtu akanituma kwenda ua wa nje upande wa kaskazini, akanileta kwenye vyumba mbele ya ua wa nje na ukuta wa nje kaskazini.
2 The building with the north-facing door was a hundred cubits long and fifty cubits wide.
Hivyo vyumba vilikuwa dhiraa mia moja karibu na mbele yake na dhiraa hamsini upana.
3 It had three floors of open halls on both sides, one facing the twenty-cubit area of the inner courtyard and one facing the pavement of the outer courtyard.
Baadhi ya hivyo vyumba vilielekea ua wa ndani na vilikuwa na dhiraa ishirini kutoka patakatifu. Kulikuwa na vyumba vitatu vinavyolingana, na kingine juu kilichokuwa kimetazama chini kuelekea kingine vilikuwa vimefunguliwa, vilikuwa na pakutokea. Baadhi ya vyumba vilielekea nje kwenye ua wa nje.
4 In front of the rooms was an inside walkway ten cubits wide and a hundred cubits long. Their doors opened to the north.
Njia dhiraa kumi upana dhiraa mia moja urefu kueleikea mbele ya vyumba. Milango ya vyumba ilikuwa mbele kaskazini.
5 The upper rooms were smaller because of the space taken up by the open halls on the lower and middle levels of the building.
Lakini kumbi za juu zilikuwa ndogo, kwa ajili ya njia za kutembea zilichukua kutoka kwazo sehemu kubwa kulikuwa walivyofanya kwenye vyumba vya chini na katikati usawa wa jengo.
6 Since they didn't have pillars like the courtyards, the upper rooms were set farther back than the lower and middle levels.
Kwa kuwa orofa tatu hapakuwa na mihimili, kama zile nyua, ambazo zilikuwa na mihimili. Hivyo usawa wa vyumba vya juu vilikuwa sawa sawa katika kipimo cha kulinganisha na vyumba vya chini na usawa wa katikakati.
7 An external wall ran in front of the rooms for fifty cubits long parallel to the outer courtyard.
Ukuta wa nje karibu na vyumba mbele ya ua wa nje, ua uliokuwa mbele ya vyumba. Huo ukuta ulikuwa dhiraa hamsini urefu.
8 The rooms on the outer courtyard extended for fifty cubits, but those that faced the Temple were a hundred cubits long.
Urefu wa vyumba vya ua wa nje ulikuwa dhiraa hamsini, na vyumba vilivyokuwa vimeelekea patakatifu vilikuwa dhiraa mia moja urefu.
9 Below these rooms was an entrance on the east side coming from the outer courtyard.
Kulikuwa na mahali pa kuingilia kwenye vyumba vidogo zaidi kutoka upande mashariki, kuingia kutoka ua wa nje.
10 Along the wall on the south side of the outer courtyard were rooms next to the courtyard and opposite the building.
Karibu na ukuta wa ua wa nje juu ya upande wa mgaribi pa ua wa ndani, mbele ya patakatifu pa ua wa nje, pia kulikuwa na vyumba na njia ya mbele yao.
11 There was a walkway in front of them, just like the rooms on the north side. These rooms had the same length and width, the same doors, floor plan, and exits.
zilikuwa kama umbo la vyumba kwa upande wa kaskazini. Zilikuwa urefu ule ule na upana na matokeo yale yale na mipangilio na madirisha.
12 Similarly there was an entrance under the rooms on the south side of the building, coming from the east side.
Kwa upande wa kusini kulikuwa na madirisha kwenye vyumba ambavyo vilikuwa kama yale yaliyokuwa upande wa kaskazini. Aya iliyokuwa ndani ilikuwa na mlango kwenye kichwa chake, na njia ilifunguliwa kwenye vyumba tafauti. Upande mashariki kulikuwa na malango wa njia kwenye njia mwishoni.
13 The man told me, “The north and south rooms that face the Temple courtyard are holy rooms where the priests who go before the Lord will eat the most holy offerings. They will place the most holy offerings there because the place is holy, and include the grain offerings, the sin offerings, and the guilt offerings.
Kisha yule mtu akanambia, “Vyumba vya kaskazini na vyumba vya kusini vilivyokuwa mbele ya ua wa nje ni vyumba vitakatifu amabapo makuhani wafanyao kazi karibu sana na Yahwe waweze kula chakula kitakatifu sana. Wataweka vitu vitakatifu sana-sadaka ya chakula, sadaka ya dhambi, na sadaka ya hatia-kwa kuwa hapa ni mahali patakatifu.
14 Once the priests have entered these rooms, they are not to go to the outer courtyard before leaving their priestly clothes, because these are holy. They must change into other clothes before go where the ordinary people are.”
Wakati makuhani watakapoingia hapo, wasitoke nje ya mahali patakatifu kwa ua wa nje, bila kuweka mavazi karibu mahali wahudumupo, kwa kuwa hapa ni patakatifu. Hivyo watavalia mahali pengine nguo kabla ya kwenda karibu na watu.”
15 After the man finished measuring inside of the Temple area, he took me out through the east gate, and he measured the surrounding area as well.
Yule mtu akamaliza kupima ndani ya nyumba na kisha akanichukua nje ya lango lililokuwa limeelekea magharibi na kuzipima sehemu zote zilizokuwa zimepazunguka hapo.
16 Using the measuring rod he measured the east side. It was five hundred cubits long.
Akaupima upande wa mashariki na fimbo ya kupimia-dhiraa mia tano kwa fimbo ya kupimia.
17 He measured the north side. It was five hundred cubits long.
akaupima upande wa kaskazini-dhiraa mia tano na fimbo ya kupimia.
18 He measured the south side. It was five hundred cubits long.
Pia akaupima upande wa kusini dhraa mia tano na fimbo ya kupimia.
19 And he came around and measured the west side. It was five hundred cubits long.
Pia akageuka na kuupima upande wa magharibi dhiraa mia tano kwa fimbo ya kupimia,
20 So he measured all four sides. There was a wall surrounding it, five hundred cubits long and five hundred cubits wide, separating the holy from the common.
Akaipima pande nne. Ilikuwa na ukuta umeizunguka ilikuwa dhiraa mia tano urefu, na dhiraa mia tano upana, kulitenganisha umbo takatifu kutoka ambapo ni pa kawada.

< Ezekiel 42 >