< Numbers 28 >

1 The Lord also said to Moses:
Bwana akamwambia Mose,
2 Command the children of Israel, and thou shalt say to them: Offer ye my oblation and my bread, and burnt sacrifice of most sweet odour, in their due seasons.
“Wape Waisraeli agizo hili na uwaambie: ‘Hakikisheni kwamba mnaniletea mimi kwa wakati uliowekwa chakula kwa ajili ya sadaka za kuteketezwa kwa moto, kama harufu nzuri ya kupendeza.’
3 These are the sacrifices which you shall offer: Two lambs of a year old without blemish every day for the perpetual holocaust:
Waambie: ‘Hii ni sadaka ya kuteketezwa kwa moto mnayomtolea Bwana: wana-kondoo wawili wa mwaka mmoja wasio na dosari, kama sadaka ya kawaida ya kuteketezwa kila siku.
4 One you shall offer in the morning, and the other in the evening:
Andaa mwana-kondoo mmoja asubuhi na mwingine jioni,
5 And the tenth part of an ephi of flour, which shall be tempered with the purest oil, of the measure of the fourth part of a hin.
kila mmoja atolewe pamoja na sadaka ya nafaka sehemu ya kumi ya efa ya unga laini uliochanganywa pamoja na robo ya hini ya mafuta ya zeituni.
6 It is the continual holocaust which you offered in mount Sinai for a most sweet. odour of a sacrifice by fire to the Lord.
Hii ni sadaka ya kawaida ya kuteketezwa iliyoanzishwa katika Mlima Sinai kama harufu nzuri ya kupendeza, sadaka iliyotolewa kwa Bwana kwa moto.
7 And for a libation you shall offer of wine the fourth part of a hin for every lamb in the sanctuary of the Lord.
Sadaka ya kinywaji itakayotolewa pamoja na kila mwana-kondoo ni robo ya hini ya kinywaji kilichochachuka. Mimina sadaka ya kinywaji kwa Bwana mahali patakatifu.
8 And you shall offer the other lamb in like manner ill the evening according to all the rites of the morning sacrifice, and of the libations thereof, an oblation of most sweet odour to the Lord.
Andaa yule mwana-kondoo wa pili jioni, pamoja na sadaka ya nafaka na sadaka ya kinywaji kama ulivyofanya kwa ile sadaka nyingine ya asubuhi. Hii ni sadaka iliyotolewa kwa kuteketezwa kwa moto, harufu nzuri ya kumpendeza Bwana.
9 And on the sabbath day you shall offer two lambs of a year old without blemish, and two tenths of flour tempered with oil in sacrifice, and the libations,
“‘Siku ya Sabato, utatoa sadaka ya wana-kondoo wawili wa mwaka mmoja wasiokuwa na dosari pamoja na sadaka yake ya kinywaji na sadaka ya nafaka yenye uzito wa sehemu mbili za kumi za efa za unga laini uliochanganywa na mafuta.
10 Which regularly are poured out every sabbath for the perpetual holocaust.
Hii ni sadaka ya kuteketezwa itakayotolewa kwa ajili ya kila Sabato, pamoja na sadaka ya kawaida ya kuteketezwa na sadaka yake ya kinywaji.
11 And on the first day of the month you shall offer a holocaust to the Lord, two calves of the herd, one ram, and seven lambs of a year old, without blemish,
“‘Siku ya kwanza ya kila mwezi, mtamletea Bwana sadaka ya kuteketezwa ya fahali wawili wachanga, kondoo dume mmoja na wana-kondoo saba wa mwaka mmoja, wote wasiokuwa na dosari.
12 And three tenths of flour tempered with oil in sacrifice for every calf: and two tenths of flour tempered with oil for every ram:
Pamoja na kila fahali, kutakuwa na sadaka ya nafaka ya unga laini sehemu tatu za kumi za efa, uliochanganywa na mafuta, pamoja na kondoo dume mmoja, sadaka ya nafaka ya unga laini uliochanganywa na mafuta;
13 And the tenth of a tenth of flour tempered with oil in sacrifice for every lamb. It is a holocaust of most sweet odour and an offering by fire to the Lord.
pamoja na kila mwana-kondoo, sadaka ya nafaka yenye uzito wa sehemu ya kumi ya efa ya unga laini uliochanganywa na mafuta. Hii ni kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa, harufu nzuri, sadaka ya kuteketezwa iliyotolewa kwa moto kwa Bwana.
14 And these shall be the libations of wine that are to be poured out for every victim: Half a hin for every calf, a third for a ram, and a fourth for a lamb. This shall be the holocaust for every month, as they succeed one another in the course of the year.
Pamoja na kila fahali kutakuwa na sadaka ya kinywaji nusu ya hini ya divai; pamoja na kila kondoo dume, theluthi moja ya hini, na pamoja na kila mwana-kondoo robo hini. Hii ni sadaka ya kuteketezwa ya kila mwezi itakayotolewa kila mwandamo wa mwezi kwa mwaka.
15 A buck goat also shall be offered to the Lord for a sin offering over and above the perpetual holocaust with its libations.
Zaidi ya sadaka ya kawaida ya kuteketezwa pamoja na sadaka yake ya kinywaji, mbuzi mmoja dume atatolewa kwa Bwana kama sadaka ya dhambi.
16 And in the first month, on the fourteenth day of the month, shall be the phase of the Lord,
“‘Katika siku ya kumi na nne ya mwezi wa kwanza, itafanyika Pasaka ya Bwana.
17 And on the fifteenth day the solemn feast: seven days shall they eat unleavened bread.
Katika siku ya kumi na tano ya mwezi huo itakuwa sikukuu; kwa siku saba mtakula mikate isiyotiwa chachu.
18 And the first day of them shall be venerable and holy: you shall not do any servile work therein.
Katika siku ya kwanza mtakuwa na kusanyiko takatifu, msifanye kazi za kawaida.
19 And you shall offer a burnt sacrifice a holocaust to the Lord, two calves of the herd, one ram, seven lambs of a year old, without blemish:
Leteni mbele za Bwana sadaka ya kuteketezwa, sadaka ya kuteketezwa ya mafahali wawili wachanga, kondoo dume mmoja na wana-kondoo dume saba wenye umri wa mwaka mmoja, wote wasio na dosari.
20 And for the sacrifices of every one three tenths of flour which shall be tempered with oil to every calf, and two tenths to every ram,
Pamoja na kila fahali, andaa sadaka ya nafaka sehemu tatu za kumi za efa za unga laini uliochanganywa na mafuta; pamoja na kondoo dume, andaa sehemu mbili za kumi za efa;
21 And the tenth of a tenth, to every lamb, that is to say, to all the seven lambs:
pia pamoja na kila mmoja wa wale wana-kondoo saba, andaa sehemu ya kumi ya efa.
22 And one buck goat for sin, to make atonement for you,
Pia mtoe beberu mmoja kama sadaka ya dhambi ambaye atafanya upatanisho kwa ajili yenu.
23 Besides the morning holocaust which you shall always offer.
Andaa hizi licha ya zile sadaka za kawaida za kuteketezwa za kila asubuhi.
24 So shall you do every day of the seven days for the food of the fire, and for a most sweet odour to the Lord, which shall rise from the holocaust, and from the libations of each.
Kwa njia hii andaa chakula cha sadaka ya kuteketezwa kila siku, kwa siku saba kama harufu nzuri impendezayo Bwana. Hii itaandaliwa licha ya ile sadaka ya kawaida ya kuteketezwa ya kila siku pamoja na sadaka yake ya kinywaji.
25 The seventh day also shall be most solemn and holy unto you: you shall do no servile work therein.
Siku ya saba mwe na kusanyiko takatifu na msifanye kazi zenu za kawaida.
26 The day also of firstfruits, when after the weeks are accomplished, you shall offer new fruits to the Lord, shall be venerable and holy: you shall do no servile work therein.
“‘Siku ya malimbuko, mnapomletea Bwana sadaka ya nafaka mpya wakati wa Sikukuu ya Majuma, mwe na kusanyiko takatifu na msifanye kazi zenu za kawaida.
27 And you shall offer a holocaust for a most sweet odour to the Lord, two calves of the herd, one ram, and seven lambs of a year old, without blemish:
Mlete sadaka ya kuteketezwa ya mafahali wawili wachanga, kondoo dume mmoja, na pia wana-kondoo saba wenye umri wa mwaka mmoja, kama harufu nzuri ya kumpendeza Bwana.
28 And in the sacrifices of them three tenths of flour tempered with oil to every calf, two to every ram,
Pamoja na kila fahali itatolewa sadaka ya nafaka ya unga laini sehemu tatu za kumi za efa uliochanganywa na mafuta; pamoja na kondoo dume, andaa sehemu mbili za kumi za efa za unga laini;
29 The tenth of a tenth to every lamb, which in all are seven lambs: a buck goat also,
na sehemu ya kumi ya efa ya unga laini kwa kila mmoja wa wana-kondoo saba.
30 Which is slain for expiation: besides the perpetual holocaust and the libations thereof.
Ongeza beberu mmoja kwa kufanya upatanisho kwa ajili yenu.
31 You shall offer them all without blemish with their libations.
Andaa hizi sadaka pamoja na sadaka zake za vinywaji, kuwa nyongeza ya sadaka za kawaida za kuteketezwa, pamoja na sadaka yake ya nafaka. Hakikisha kuwa wanyama hao hawana dosari.

< Numbers 28 >