< Genesis 21 >
1 And the Lord visited Sara, as he had promised: and fulfilled what he had spoken.
Wakati huu Bwana akamrehemu Sara kama alivyokuwa amesema, naye Bwana akamtendea Sara kile alichokuwa ameahidi.
2 And she conceived and bore a son in her old age, at the time that God had foretold her.
Sara akapata mimba, akamzalia Abrahamu mwana katika uzee wake, majira yale ya Mungu aliomwahidi.
3 And Abraham called the name of his son, whom Sara bore him, Isaac.
Abrahamu akamwita Isaki yule mwana ambaye Sara alimzalia.
4 And he circumcised him the eighth day, as God had commanded him,
Isaki alipokuwa na umri wa siku nane, Abrahamu akamtahiri, kama Mungu alivyomwamuru.
5 When he was a hundred years old: for at this age of his father was Isaac born.
Abrahamu alikuwa na miaka 100 wakati Isaki mwanawe alipozaliwa.
6 And Sara said: God hath made a laughter for me: whosoever shall hear of it will laugh with me.
Sara akasema, “Mungu ameniletea kicheko, kila mmoja atakayesikia jambo hili atacheka pamoja nami.”
7 And again she said: Who would believe that Abraham should hear that Sara gave suck to a son, whom she bore to him in his old age.
Akaongeza kusema, “Nani angemwambia Abrahamu kuwa Sara angenyonyesha watoto? Tena nimemzalia mwana katika uzee wake.”
8 And the child grew and was weaned: and Abraham made a great feast on the day of his weaning.
Mtoto akakua, akaachishwa kunyonya. Siku hiyo Isaki alipoachishwa kunyonya, Abrahamu alifanya sherehe kubwa.
9 And when Sara had seen the son of Agar the Egyptian playing with Isaac her son, she said to Abraham:
Lakini Sara aliona kuwa mwana ambaye Hagari, Mmisri, aliyemzalia Abrahamu alikuwa anadhihaki,
10 Cast out this bondwoman, and her son: for the son of the bondwoman shall not be heir with my son Isaac.
Sara akamwambia Abrahamu, “Mwondoe mwanamke huyo mtumwa pamoja na mwanawe, kwa kuwa mwana wa mwanamke mtumwa kamwe hatarithi pamoja na mwanangu Isaki.”
11 Abraham took this grievously for his son.
Jambo hili lilimhuzunisha sana Abrahamu kwa sababu lilimhusu mwanawe.
12 And God said to him: Let it not seem grievous to thee for the boy, and for thy bondwoman: in all that Sara hath said to thee, hearken to her voice: for in Isaac shall thy seed be called.
Lakini Mungu akamwambia, “Usihuzunike hivyo kwa sababu ya kijana na mtumishi wako wa kike. Sikiliza lolote Sara analokuambia, kwa sababu uzao wako utahesabiwa kupitia kwake Isaki.
13 But I will make the son also of the bondwoman a great nation, because he is thy seed.
Nitamfanya huyu mwana wa mtumishi wako wa kike kuwa taifa pia, kwa sababu naye ni uzao wako.”
14 So Abraham rose up in the morning, and taking bread and a bottle of water, put it upon her shoulder, and delivered the boy, and sent her away. And she departed, and wandered in the wilderness of Bersabee.
Kesho yake asubuhi na mapema, Abrahamu akachukua chakula na kiriba cha maji, akampa Hagari. Akaviweka mabegani mwa Hagari, akamwondoa pamoja na kijana. Hagari akashika njia, akatangatanga katika jangwa la Beer-Sheba.
15 And when the water in the bottle was spent, she cast the boy under one of the trees that were there.
Maji yalipokwisha kwenye kiriba, akamwacha kijana chini ya mojawapo ya vichaka.
16 And she went her way, and sat over against him a great way off as far as a bow can carry, for she said: I will not see the boy die: and sitting over against, she lifted up her voice and wept.
Kisha akajiendea zake akaketi karibu, umbali wa kutupa mshale, akawaza, “Siwezi kumwangalia kijana akifa.” Ikawa alipokuwa ameketi pale karibu, akaanza kulia kwa huzuni.
17 And God heard the voice of the boy: and an angel of God called to Agar from heaven, saying: What art thou doing, Agar? fear not: for God hath heard the voice of the boy, from the place wherein he is.
Mungu akamsikia kijana akilia, malaika wa Mungu akamwita Hagari kutoka mbinguni na kumwambia, “Kuna nini Hagari? Usiogope, Mungu amesikia kijana analia akiwa amelala pale.
18 Arise, take up the boy, and hold him by the hand: for I will make him a great nation.
Mwinue kijana na umshike mkono, kwa maana nitamfanya kuwa taifa kubwa.”
19 And God opened her eyes: and she saw a well of water, and went and filled the bottle, and gave the boy to drink.
Ndipo Mungu akamfumbua Hagari macho yake naye akaona kisima cha maji. Hivyo akaenda akajaza kiriba maji na kumpa kijana anywe.
20 And God was with him: and he grew, and dwelt in the wilderness, and became a young man, an archer.
Mungu akawa pamoja na huyu kijana alipokuwa akiendelea kukua. Aliishi jangwani na akawa mpiga upinde.
21 And he dwelt in the wilderness of Pharan, and his mother took a wife for him out of the land of Egypt.
Alipokuwa akiishi katika Jangwa la Parani, mama yake akampatia mke kutoka Misri.
22 At the same time Abimelech, and Phicol the general of his army said to Abraham: God is with thee in all that thou dost.
Wakati huo Abimeleki na Fikoli mkuu wa majeshi yake wakamwambia Abrahamu, “Mungu yu pamoja nawe katika kila kitu unachofanya.
23 Swear therefore by God, that thou wilt not hurt me, nor my posterity, nor my stock: but according to the kindness that I have done to thee, thou shalt do to me, and to the land wherein thou hast lived a stranger.
Sasa niapie hapa mbele za Mungu kwamba hutanitenda hila mimi, watoto wangu wala wazao wangu. Nitendee mimi na nchi ambayo unaishi kama mgeni wema ule ule ambao nimekutendea.”
24 And Abraham said: I will swear.
Abrahamu akasema, “Ninaapa hivyo.”
25 And he reproved Abimelech for a well of water, which his servants had taken away by force.
Ndipo Abrahamu akalalamika kwa Abimeleki kuhusu kisima cha maji ambacho watumishi wa Abimeleki walikuwa wamekinyangʼanya.
26 And Abimelech answered: I knew not who did this thing: and thou didst not tell me, and I heard not of it till today.
Lakini Abimeleki akasema, “Sijui ni nani ambaye amefanya hili. Hukuniambia, leo tu ndipo ninasikia habari zake.”
27 And Abraham took sheep and oxen and gave them to Abimelech: and both of them made a league.
Hivyo Abrahamu akaleta kondoo na ngʼombe, akampa Abimeleki, nao watu hawa wawili wakafanya mapatano.
28 And Abraham set apart seven ewe lambs of the flock.
Abrahamu akatenga kondoo wa kike saba kutoka kwenye kundi,
29 And Abimelech said to him: What mean these seven ewe lambs which thou hast set apart?
Abimeleki akamuuliza Abrahamu, “Ni nini maana ya hawa kondoo wa kike saba uliowatenga peke yao?”
30 But he said: Thou shalt take seven ewe lambs at my hand: that they may be a testimony for me, that I dug this well.
Abrahamu akamjibu, “Upokee hawa kondoo wa kike saba kutoka mkononi mwangu kama ushahidi kuwa nilichimba kisima hiki.”
31 Therefore that place was called Bersabee: because there both of them did swear.
Hivyo mahali pale pakaitwa Beer-Sheba, kwa sababu watu wawili waliapiana hapo.
32 And they made a league for the well of oath.
Baada ya mapatano kufanyika huko Beer-Sheba, Abimeleki na Fikoli mkuu wa majeshi yake wakarudi katika nchi ya Wafilisti.
33 And Abimelech, and Phicol the general of his army arose and returned to the land of the Palestines. But Abraham planted a grove in Bersabee, and there called upon the name of the Lord God eternal.
Abrahamu akapanda mti wa mkwaju huko Beer-Sheba, na hapo akaliitia jina la Bwana, Mungu wa milele.
34 And he was a sojourner in the land of the Palestines many days.
Naye Abrahamu akakaa katika nchi ya Wafilisti kwa muda mrefu.