< John 6 >
1 After these things Jesus went away beyond the sea of Galilee, [or] of Tiberias,
Baada ya hayo, Yesu alivuka ziwa Galilaya (au Ziwa Tiberia).
2 and a great crowd followed him, because they saw the signs which he wrought upon the sick.
Umati mkubwa wa watu ulimfuata kwa sababu watu hao walikuwa wameona ishara alizokuwa akifanya kwa kuwaponya wagonjwa.
3 And Jesus went up into the mountain, and there sat with his disciples:
Yesu alipanda mlimani, akaketi pamoja na wanafunzi wake.
4 but the passover, the feast of the Jews, was near.
Sikukuu ya Wayahudi iitwayo Pasaka ilikuwa imekaribia.
5 Jesus then, lifting up his eyes and seeing that a great crowd is coming to him, says to Philip, Whence shall we buy loaves that these may eat?
Basi, Yesu na alipotazama na kuona umati wa watu ukija kwake, alimwambia Filipo, “Tununue wapi mikate ili watu hawa wapate kula?”
6 But this he said trying him, for he knew what he was going to do.
(Alisema hivyo kwa kumjaribu Filipo, kwani alijua mwenyewe atakalofanya.)
7 Philip answered him, Loaves for two hundred denarii are not sufficient for them, that each may have some little [portion].
Filipo akamjibu, “Mikate ya denari mia mbili za fedha haiwatoshi watu hawa hata kama ila mmoja atapata kipande kidogo tu!”
8 One of his disciples, Andrew, Simon Peter's brother, says to him,
Mmoja wa wanafunzi wake aitwaye Andrea, nduguye Simoni Petro, akamwambia,
9 There is a little boy here who has five barley loaves and two small fishes; but this, what is it for so many?
“Yupo hapa mtoto mmoja aliye na mikate mitano ya shayiri na samaki wawili; lakini hivi vyatosha nini kwa watu wengi kama hawa?”
10 [And] Jesus said, Make the men sit down. Now there was much grass in the place: the men therefore sat down, in number about five thousand.
Yesu akasema, “Waketisheni watu.” Palikuwa na nyasi tele mahali hapo. Basi, watu wakaketi, jumla yapata wanaume elfu tano.
11 And Jesus took the loaves, and having given thanks, distributed [them] to those that were set down; and in like manner of the small fishes as much as they would.
Yesu akaitwaa ile mikate, akamshukuru Mungu, akawagawia watu waliokuwa wameketi; akafanya vivyo hivyo na wale samaki, kila mtu akapata kadiri alivyotaka.
12 And when they had been filled, he says to his disciples, Gather together the fragments which are over and above, that nothing may be lost.
Watu waliposhiba Yesu akawaambia wanafunzi wake, “Kusanyeni vipande vilivyobaki visipotee.”
13 They gathered [them] therefore together, and filled twelve hand-baskets full of fragments of the five barley loaves, which were over and above to those that had eaten.
Basi, wakakusanya vipande vya mikate ya shayiri walivyobakiza wale watu waliokula, wakajaza vikapu kumi na viwili.
14 The men therefore, having seen the sign which Jesus had done, said, This is truly the prophet which is coming into the world.
Watu walipoiona ishara hiyo aliyoifanya Yesu, wakasema, “Hakika huyu ndiye nabii anayekuja ulimwenguni.”
15 Jesus therefore knowing that they were going to come and seize him, that they might make [him] king, departed again to the mountain himself alone.
Yesu akajua ya kuwa watu walitaka kumchukua wamfanye mfalme, akaondoka tena, akaenda mlimani peke yake.
16 But when evening was come, his disciples went down to the sea,
Ilipokuwa jioni wanafunzi wake waliteremka hadi ziwani,
17 and having gone on board ship, they went over the sea to Capernaum. And it had already become dark, and Jesus had not come to them,
wakapanda mashua ili wavuke kwenda Kafarnaumu. Giza lilikuwa limeingia, na Yesu alikuwa hajawafikia bado.
18 and the sea was agitated by a strong wind blowing.
Ziwa likaanza kuchafuka kwa sababu upepo mkali ulikuwa unavuma.
19 Having rowed then about twenty-five or thirty stadia, they see Jesus walking on the sea and coming near the ship; and they were frightened.
Wanafunzi walipokuwa wamekwenda umbali wa kilomita tano au sita, walimwona Yesu akitembea juu ya maji, anakaribia mashua; wakaogopa sana.
20 But he says to them, It is I: be not afraid.
Yesu akawaambia, “Ni mimi, msiogope!”
21 They were willing therefore to receive him into the ship; and immediately the ship was at the land to which they went.
Walifurahi kumchukua Yesu katika mashua; na mara mashua ikawasili nchi kavu walipokuwa wanakwenda.
22 On the morrow the crowd which stood on the other side of the sea, having seen that there was no other little ship there except that into which his disciples had got, and that Jesus had not gone with his disciples into the ship, but [that] his disciples had gone away alone;
Kesho yake umati wa watu wale waliobaki upande wa pili wa ziwa walitambua kwamba kulikuwa na mashua moja tu pale, na Yesu hakuingia katika mashua pamoja na wanafunzi wake, ila wanafunzi hao walikuwa wamekwenda zao peke yao.
23 (but other little ships out of Tiberias came near to the place where they ate bread after the Lord had given thanks; )
Mashua nyingine kutoka Tiberia zilifika mahali hapo watu walipokula ile mikate, Bwana alipokwisha mshukuru Mungu.
24 when therefore the crowd saw that Jesus was not there, nor his disciples, they got into the ships, and came to Capernaum, seeking Jesus.
Basi, hao watu walipogundua kwamba Yesu na wanafunzi wake hawakuwapo mahali hapo, walipanda mashua, wakaenda Kafarnaumu wakimtafuta.
25 And having found him the other side of the sea, they said to him, Rabbi, when art thou arrived here?
Wale watu walipomkuta Yesu ng'ambo ya pili wa ziwa walimwuliza, “Mwalimu, ulifika lini hapa?”
26 Jesus answered them and said, Verily, verily, I say to you, Ye seek me not because ye have seen signs, but because ye have eaten of the loaves and been filled.
Yesu akawajibu, “Kweli nawaambieni, mnanitafuta si kwa kuwa mmeona ishara, bali kwa sababu mlikula ile mikate mkashiba.
27 Work not [for] the food which perishes, but [for] the food which abides unto life eternal, which the Son of man shall give to you; for him has the Father sealed, [even] God. (aiōnios )
Msikishughulikie chakula kiharibikacho; kishugulikieni chakula kidumucho kwa ajili ya uzima wa milele. Mwana wa Mtu ambaye Baba amemthibitisha atawapeni chakula hicho.” (aiōnios )
28 They said therefore to him, What should we do that we may work the works of God?
Wao wakamwuliza, “Tufanye nini ili tuweze kuzitenda kazi za Mungu?”
29 Jesus answered and said to them, This is the work of God, that ye believe on him whom he has sent.
Yesu akawajibu, “Hii ndiyo kazi anayotaka Mungu muifanye: kumwamini yule aliyemtuma.”
30 They said therefore to him, What sign then doest thou that we may see and believe thee? what dost thou work?
Hapo wakamwambia, “Utafanya ishara gani ili tuione tupate kukuamini? Utafanya kitu gani?
31 Our fathers ate the manna in the wilderness, as it is written, He gave them bread out of heaven to eat.
Wazee wetu walikula mana kule jangwani, kama yasemavyo Maandiko: Aliwalisha mkate kutoka mbinguni.”
32 Jesus therefore said to them, Verily, verily, I say to you, [It is] not Moses that has given you the bread out of heaven; but my Father gives you the true bread out of heaven.
Yesu akawaambia, “Kweli nawaambieni, Mose hakuwapeni mkate kutoka mbinguni; Baba yangu ndiye awapaye ninyi mkate halisi kutoka mbinguni.
33 For the bread of God is he who comes down out of heaven and gives life to the world.
Maana mkate wa Mungu ni yule ashukaye kutoka mbinguni na aupaye ulimwengu uzima.”
34 They said therefore to him, Lord, ever give to us this bread.
Basi, wakamwambia, “Mheshimiwa, tupe daima mkate huo.”
35 [And] Jesus said to them, I am the bread of life: he that comes to me shall never hunger, and he that believes on me shall never thirst at any time.
Yesu akawaambia, “Mimi ndimi mkate wa uzima. Anayekuja kwangu hataona njaa; anayeniamini hataona kiu kamwe.
36 But I have said to you, that ye have also seen me and do not believe.
Lakini niliwaambieni kwamba ingawa mmeniona hamniamini.
37 All that the Father gives me shall come to me, and him that comes to me I will not at all cast out.
Wote anaonipa Baba watakuja kwangu; nami sitamtupa nje yeyote anayekuja kwangu,
38 For I am come down from heaven, not that I should do my will, but the will of him that has sent me.
kwani nimeshuka kutoka mbinguni si kwa ajili ya kufanya matakwa yangu, ila kutimiza matakwa ya yule aliyenituma.
39 And this is the will of him that has sent me, that of all that he has given me I should lose nothing, but should raise it up in the last day.
Na matakwa ya yule aliyenituma ndiyo haya: nisimpoteze hata mmoja kati ya wale alionipa, ila niwafufue wote Siku ya mwisho.
40 For this is the will of my Father, that every one who sees the Son, and believes on him, should have life eternal; and I will raise him up at the last day. (aiōnios )
Maana anachotaka Baba yangu ndicho hiki: kila amwonaye Mwana na kumwamini awe na uzima wa milele; nami nitamfufua Siku ya mwisho.” (aiōnios )
41 The Jews therefore murmured about him, because he said, I am the bread which has come down out of heaven.
Basi, Wayahudi wakaanza kunung'unika kwa kuwa alisema: “Mimi ni mkate ulioshuka kutoka mbinguni.”
42 And they said, Is not this Jesus the son of Joseph, whose father and mother we have known? how then does he say, I am come down out of heaven?
Wakasema, “Je, huyu si mwana wa Yosefu? Tunawajua baba yake na mama yake! Basi, anawezaje kusema kwamba ameshuka kutoka mbinguni?”
43 Jesus therefore answered and said to them, Murmur not among yourselves.
Yesu akawaambia, “Acheni kunung'unika ninyi kwa ninyi.
44 No one can come to me except the Father who has sent me draw him, and I will raise him up in the last day.
Hakuna mtu awezaye kuja kwangu, Baba aliyenituma asipomvuta kwangu; nami nitamfufua mtu huyo Siku ya mwisho.
45 It is written in the prophets, And they shall be all taught of God. Every one that has heard from the Father [himself], and has learned [of him], comes to me;
Manabii wameandika: Watu wote watafundishwa na Mungu. Kila mtu anayemsikia Baba na kujifunza kutoka kwake, huja kwangu.
46 not that any one has seen the Father, except he who is of God, he has seen the Father.
Hii haina maana kwamba yupo mtu aliyemwona Baba, isipokuwa yule aliyetoka kwa Mungu; huyo ndiye aliyemwona Baba.
47 Verily, verily, I say to you, He that believes [on me] has life eternal. (aiōnios )
Kweli, nawaambieni, anayeamini anao uzima wa milele. (aiōnios )
48 I am the bread of life.
Mimi ni mkate wa uzima.
49 Your fathers ate the manna in the wilderness and died.
Wazee wenu walikula mana kule jangwani, lakini walikufa.
50 This is the bread which comes down out of heaven, that one may eat of it and not die.
Huu ndio mkate kutoka mbinguni; mkate ambao anayekula hatakufa.
51 I am the living bread which has come down out of heaven: if any one shall have eaten of this bread he shall live for ever; but the bread withal which I shall give is my flesh, which I will give for the life of the world. (aiōn )
Mimi ni mkate hai ulioshuka kutoka mbinguni. Mtu yeyote akila mkate huu ataishi milele. Na mkate nitakaompa ni mwili wangu ninaoutoa kwa ajili ya uzima wa ulimwengu.” (aiōn )
52 The Jews therefore contended among themselves, saying, How can he give us this flesh to eat?
Ndipo Wayahudi wakaanza kubishana kati yao:
53 Jesus therefore said to them, Verily, verily, I say unto you, Unless ye shall have eaten the flesh of the Son of man, and drunk his blood, ye have no life in yourselves.
Yesu akawaambia, “Kweli nawaambieni, msipokula mwili wa Mwana wa Mtu na kunywa damu yake, hamtakuwa na uzima ndani yenu.
54 He that eats my flesh and drinks my blood has life eternal, and I will raise him up at the last day: (aiōnios )
Anayekula mwili wangu na kunywa damu yangu anao uzima wa milele nami nitamfufua siku ya mwisho. (aiōnios )
55 for my flesh is truly food and my blood is truly drink.
Maana mwili wangu ni chakula cha kweli, na damu yangu ni kinywaji cha kweli.
56 He that eats my flesh and drinks my blood dwells in me and I in him.
Aulaye mwili wangu na kunywa damu yangu, akaa ndani yangu, nami nakaa ndani yake.
57 As the living Father has sent me and I live on account of the Father, he also who eats me shall live also on account of me.
Baba aliye hai alinituma, nami naishi kwa sababu yake; vivyo hivyo anilaye mimi ataishi pia kwa sababu yangu.
58 This is the bread which has come down out of heaven. Not as the fathers ate and died: he that eats this bread shall live for ever. (aiōn )
Basi, huu ndio mkate ulioshuka kutoka mbinguni; si kama mana waliyokula babu zetu, wakafa. Aulaye mkate huu ataishi milele.” (aiōn )
59 These things he said in [the] synagogue, teaching in Capernaum.
Yesu alisema hayo alipokuwa akifundisha katika sunagogi kule Kafarnaumu.
60 Many therefore of his disciples having heard [it] said, This word is hard; who can hear it?
Basi, wengi wa wafuasi wake waliposikia hayo, wakasema, “Haya ni mambo magumu! Nani awezaye kuyasikiliza?”
61 But Jesus, knowing in himself that his disciples murmur concerning this, said to them, Does this offend you?
Yesu alijua bila kuambiwa na mtu kwamba wanafunzi wake walikuwa wananung'unika juu ya jambo hilo, akawauliza, “Je, jambo hili linawafanya muwe na mashaka?
62 If then ye see the Son of man ascending up where he was before?
Itakuwaje basi, mtakapomwona Mwana wa Mtu akipanda kwenda kule alikokuwa kwanza?
63 It is the Spirit which quickens, the flesh profits nothing: the words which I have spoken unto you are spirit and are life.
Roho ndiye atiaye uzima; binadamu peke yake hawezi. Maneno niliyowaambieni ni Roho, ni uzima.
64 But there are some of you who do not believe. For Jesus knew from the beginning who they were who did not believe, and who would deliver him up.
Hata hivyo, wako baadhi yenu wasioamini.” (Yesu alisema hivyo kwani alijua tangu mwanzo ni kina nani wasioamini, na pia ni nani atakayemsaliti.)
65 And he said, Therefore said I unto you, that no one can come to me unless it be given to him from the Father.
Kisha akasema, “Ndiyo maana niliwaambieni kwamba hakuna awezaye kuja kwangu asipowezeshwa na Baba yangu.”
66 From that [time] many of his disciples went away back and walked no more with him.
Kutokana na hayo, wengi wa wafuasi wake walirudi nyuma wasiandamane naye tena.
67 Jesus therefore said to the twelve, Will ye also go away?
Basi, Yesu akawauliza wale kumi na wawili, “Je, nanyi pia mwataka kwenda zenu?”
68 Simon Peter answered him, Lord, to whom shall we go? thou hast words of life eternal; (aiōnios )
Simoni Petro akamjibu, “Bwana, tutakwenda kwa nani? Wewe unayo maneno yaletayo uzima wa milele. (aiōnios )
69 and we have believed and known that thou art the holy one of God.
Sisi tunaamini, na tunajua kwamba wewe ndiwe yule Mtakatifu wa Mungu.”
70 Jesus answered them, Have not I chosen you the twelve? and of you one is a devil.
Yesu akawaambia, “Je, sikuwachagua ninyi kumi na wawili? Hata hivyo, mmoja wenu ni Ibilisi!”
71 Now he spoke of Judas [the son] of Simon, Iscariote, for he [it was who] should deliver him up, being one of the twelve.
Yesu alisema hayo juu ya Yuda, mwana wa Simoni Iskarioti; maana huyu alikuwa ndiye atakayemsaliti, ingawa alikuwa mmoja wa wale kumi na wawili.