< Ezekiel 35 >

1 And the word of Jehovah came unto me, saying,
Neno la Bwana likanijia kusema:
2 Son of man, set thy face against mount Seir, and prophesy against it,
“Mwanadamu, elekeza uso wako juu ya mlima Seiri, utabiri dhidi yake
3 and say unto it, Thus saith the Lord Jehovah: Behold, I am against thee, mount Seir, and I will stretch out my hand upon thee, and I will make thee a desolation and an astonishment.
na useme: ‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Mimi ni kinyume nawe, ee mlima Seiri, nami nitanyoosha mkono wangu dhidi yako na kukufanya ukiwa na usiyekaliwa na watu wala kulimika.
4 I will lay thy cities waste, and thou shalt be a desolation: and thou shalt know that I [am] Jehovah.
Nitaifanya miji yako kuwa magofu nawe utakuwa ukiwa. Ndipo utakapojua kuwa Mimi ndimi Bwana.
5 Because thou hast had a perpetual hatred, and hast given over the children of Israel to the power of the sword, in the time of their calamity, in the time of the iniquity of the end;
“‘Kwa sababu ulificha moyoni uadui wa siku nyingi nawe ukawatoa Waisraeli wauawe kwa upanga wakati wa maafa yao, wakati adhabu yake ilipofikia kilele chake,
6 therefore, [as] I live, saith the Lord Jehovah, I will certainly appoint thee unto blood, and blood shall pursue thee; since thou hast not hated blood, blood shall pursue thee.
kwa hiyo hakika kama niishivyo, asema Bwana Mwenyezi, nitakutia katika umwagaji damu nao utakufuatia. Kwa kuwa hakuchukia kumwaga damu, kumwaga damu kutakufuatia.
7 And I will make mount Seir a desolation and an astonishment, and cut off from it him that passeth out and him that returneth;
Nitaufanya Mlima Seiri ukiwa na usiokaliwa na watu wala kulimika na kuukatilia mbali na wote wanaokuja na wanaokwenda.
8 and I will fill his mountains with his slain. In thy hills, and in thy valleys, and in all thy water-courses shall they fall that are slain with the sword.
Nitaijaza milima yenu kwa watu wake waliouawa, wale waliouawa kwa upanga wataanguka juu ya vilima vyako na katika mabonde yako na katika makorongo yako yote.
9 I will make thee perpetual desolations, and thy cities shall not be inhabited: and ye shall know that I [am] Jehovah.
Nitakufanya ukiwa milele, watu hawataishi katika miji yako. Ndipo utakapojua kuwa Mimi ndimi Bwana.
10 Because thou hast said, These two nations and these two countries shall be mine, and we will possess it, whereas Jehovah was there:
“‘Kwa sababu umesema, “Mataifa haya mawili na nchi hizi zitakuwa zetu nasi tutazimiliki,” ingawa hata mimi Bwana nilikuwa huko,
11 therefore, [as] I live, saith the Lord Jehovah, I will even do according to thine anger and according to thine envy, as thou hast done out of thy hatred against them; and I will make myself known among them, when I shall judge thee.
kwa hiyo hakika kama niishivyo, asema Bwana Mwenyezi, nitakutenda kwa kadiri ya hasira na wivu uliouonyesha katika chuki yako juu yao nami nitafanya nijulikane miongoni mwao wakati nitakapokuhukumu.
12 And thou shalt know that I Jehovah have heard all thy reproaches, which thou hast uttered against the mountains of Israel, saying, They are laid desolate, they are given us to devour.
Ndipo utakapojua kuwa Mimi Bwana nimesikia mambo yote ya dharau uliyosema dhidi ya milima ya Israeli. Ulisema, “Wamefanyika ukiwa na kutiwa mikononi mwetu tuwararue.”
13 And ye have magnified yourselves against me with your mouth, and have multiplied your words against me: I have heard [them].
Ulijigamba dhidi yangu na kusema maneno dhidi yangu bila kujizuia, nami nikayasikia.
14 Thus saith the Lord Jehovah: When the whole earth rejoiceth, I will make thee a desolation.
Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Wakati dunia yote inashangilia nitakufanya ukiwa.
15 As thou didst rejoice at the inheritance of the house of Israel, because it was desolated, so will I do unto thee: thou shalt be a desolation, O mount Seir, and all Edom, the whole of it: and they shall know that I [am] Jehovah.
Kwa sababu ulishangilia wakati urithi wa nyumba ya Israeli ulipofanyika ukiwa, hivyo ndivyo nitakavyokutendea. Utakuwa ukiwa, ee mlima Seiri, wewe na Edomu yote. Kisha ndipo watajua kuwa Mimi ndimi Bwana.’”

< Ezekiel 35 >