< Song of Solomon 4 >
1 How beautiful you are, my darling— how very beautiful! Your eyes are like doves behind your veil. Your hair is like a flock of goats streaming down Mount Gilead.
Tazama jinsi ulivyo mzuri, mpenzi wangu! Ee, jinsi ulivyo mzuri! Macho yako nyuma ya shela yako ni kama ya hua. Nywele zako ni kama kundi la mbuzi zikishuka kutoka Mlima Gileadi.
2 Your teeth are like a flock of newly shorn sheep coming up from the washing; each has its twin, and not one of them is lost.
Meno yako ni kama kundi la kondoo waliokatwa manyoya sasa hivi, watokao kuogeshwa. Kila mmoja ana pacha lake, hakuna hata mmoja aliye peke yake.
3 Your lips are like a scarlet ribbon, and your mouth is lovely. Your brow behind your veil is like a slice of pomegranate.
Midomo yako ni kama uzi mwekundu, kinywa chako kinapendeza. Mashavu yako nyuma ya shela yako ni kama vipande viwili vya komamanga.
4 Your neck is like the tower of David, built with rows of stones; on it hang a thousand shields, all of them shields of warriors.
Shingo yako ni kama mnara wa Daudi, uliojengwa kwa madaha, juu yake zimetundikwa ngao elfu, zote ni ngao za mashujaa.
5 Your breasts are like two fawns, twins of a gazelle grazing among the lilies.
Matiti yako mawili ni kama wana-paa wawili, kama wana-paa mapacha wajilishao katikati ya yungiyungi.
6 Before the day breaks and the shadows flee, I will make my way to the mountain of myrrh and to the hill of frankincense.
Hata kupambazuke na vivuli vikimbie, nitakwenda kwenye mlima wa manemane na kwenye kilima cha uvumba.
7 You are altogether beautiful, my darling; in you there is no flaw.
Wewe ni mzuri kote, mpenzi wangu, hakuna hitilafu ndani yako.
8 Come with me from Lebanon, my bride, come with me from Lebanon! Descend from the peak of Amana, from the summits of Senir and Hermon, from the dens of the lions, from the mountains of the leopards.
Enda nami kutoka Lebanoni, bibi arusi wangu, enda nami kutoka Lebanoni. Shuka kutoka ncha ya Amana, kutoka juu ya Seniri, kilele cha Hermoni, kutoka mapango ya simba na kutoka mlima wapendapo kukaa chui.
9 You have captured my heart, my sister, my bride; you have stolen my heart with one glance of your eyes, with one jewel of your neck.
Umeiba moyo wangu, dada yangu, bibi arusi wangu; umeiba moyo wangu kwa mtazamo mmoja wa macho yako, kwa kito kimoja cha mkufu wako.
10 How delightful is your love, my sister, my bride! Your love is much better than wine, and the fragrance of your perfume than all spices.
Tazama jinsi pendo lako linavyofurahisha, dada yangu, bibi arusi wangu! Pendo lako linafurahisha aje zaidi ya divai, na harufu ya manukato yako zaidi ya kikolezo chochote!
11 Your lips, my bride, drip sweetness like the honeycomb; honey and milk are under your tongue, and the fragrance of your garments is like the aroma of Lebanon.
Midomo yako inadondosha utamu kama sega la asali, bibi arusi wangu; maziwa na asali viko chini ya ulimi wako. Harufu nzuri ya mavazi yako ni kama ile ya Lebanoni.
12 My sister, my bride, you are a garden locked up, a spring enclosed, a fountain sealed.
Wewe ni bustani iliyofungwa, dada yangu, bibi arusi wangu; wewe ni chanzo cha maji kilichozungushiwa kabisa, chemchemi yangu peke yangu.
13 Your branches are an orchard of pomegranates with the choicest of fruits, with henna and nard,
Mimea yako ni bustani ya mikomamanga yenye matunda mazuri sana, yenye hina na nardo,
14 with nard and saffron, with calamus and cinnamon, with every kind of frankincense tree, with myrrh and aloes, with all the finest spices.
nardo na zafarani, mchai na mdalasini, pamoja na kila aina ya mti wa uvumba, manemane na udi, na aina zote za vikolezo bora kuliko vyote.
15 You are a garden spring, a well of fresh water flowing down from Lebanon.
Wewe ni chemchemi ya bustani, kisima cha maji yatiririkayo, yakitiririka kutoka Lebanoni.
16 Awake, O north wind, and come, O south wind. Breathe on my garden and spread the fragrance of its spices. Let my beloved come into his garden and taste its choicest fruits.
Amka, upepo wa kaskazini, na uje, upepo wa kusini! Vuma juu ya bustani yangu, ili harufu yake nzuri iweze kuenea mpaka ngʼambo. Mpendwa wangu na aje bustanini mwake na kuonja matunda mazuri sana.