< Psalms 38 >
1 A Psalm of David, for remembrance. O LORD, do not rebuke me in Your anger or discipline me in Your wrath.
Zaburi ya Daudi. Maombi. Ee Bwana, usinikemee katika hasira yako, wala kuniadhibu katika ghadhabu yako.
2 For Your arrows have pierced me deeply, and Your hand has pressed down on me.
Kwa kuwa mishale yako imenichoma, na mkono wako umenishukia.
3 There is no soundness in my body because of Your anger; there is no rest in my bones because of my sin.
Hakuna afya mwilini mwangu kwa sababu ya ghadhabu yako, mifupa yangu haina uzima kwa sababu ya dhambi zangu.
4 For my iniquities have overwhelmed me; they are a burden too heavy to bear.
Maovu yangu yamenifunika kama mzigo usiochukulika.
5 My wounds are foul and festering because of my sinful folly.
Majeraha yangu yameoza na yananuka, kwa sababu ya upumbavu wa dhambi zangu.
6 I am bent and brought low; all day long I go about mourning.
Nimeinamishwa chini na kushushwa sana, mchana kutwa nazunguka nikiomboleza.
7 For my loins are full of burning pain, and no soundness remains in my body.
Viuno vyangu vimejaa maumivu yaunguzayo, hakuna afya mwilini mwangu.
8 I am numb and badly crushed; I groan in anguish of heart.
Nimedhoofika na kupondwa kabisa, nasononeka kwa maumivu makuu ya moyoni.
9 O Lord, my every desire is before You; my groaning is not hidden from You.
Ee Bwana, yote ninayoyaonea shauku yako wazi mbele zako, kutamani kwangu sana hakufichiki mbele zako.
10 My heart pounds, my strength fails, and even the light of my eyes has faded.
Moyo wangu unapigapiga, nguvu zangu zimeniishia; hata macho yangu yametiwa giza.
11 My beloved and friends shun my disease, and my kinsmen stand at a distance.
Rafiki na wenzangu wananikwepa kwa sababu ya majeraha yangu; majirani zangu wanakaa mbali nami.
12 Those who seek my life lay snares; those who wish me harm speak destruction, plotting deceit all day long.
Wale wanaotafuta uhai wangu wanatega mitego yao, wale ambao wangetaka kunidhuru huongea juu ya maangamizi yangu; hufanya shauri la hila mchana kutwa.
13 But like a deaf man, I do not hear; and like a mute man, I do not open my mouth.
Mimi ni kama mtu kiziwi, asiyeweza kusikia, ni kama bubu, asiyeweza kufungua kinywa chake,
14 I am like a man who cannot hear, whose mouth offers no reply.
nimekuwa kama mtu asiyesikia, ambaye kinywa chake hakiwezi kutoa jibu.
15 I wait for You, O LORD; You will answer, O Lord my God.
Ee Bwana, ninakungojea wewe, Ee Bwana Mungu wangu, utajibu.
16 For I said, “Let them not gloat over me— those who taunt me when my foot slips.”
Kwa kuwa nilisema, “Usiwaache wafurahie, wala wasijitukuze juu yangu mguu wangu unapoteleza.”
17 For I am ready to fall, and my pain is ever with me.
Kwa maana ninakaribia kuanguka, na maumivu yangu yananiandama siku zote.
18 Yes, I confess my iniquity; I am troubled by my sin.
Naungama uovu wangu, ninataabishwa na dhambi yangu.
19 Many are my enemies without cause, and many hate me without reason.
Wengi ni wale ambao ni adui zangu hodari, wale wanaonichukia bila sababu ni wengi.
20 Those who repay my good with evil attack me for pursuing the good.
Wanaolipa maovu kwa wema wangu hunisingizia ninapofuata lililo jema.
21 Do not forsake me, O LORD; be not far from me, O my God.
Ee Bwana, usiniache, usiwe mbali nami, Ee Mungu wangu.
22 Come quickly to help me, O Lord my Savior.
Ee Bwana Mwokozi wangu, uje upesi kunisaidia.