< Psalms 145 >
1 A Psalm of praise. Of David. I will exalt You, my God and King; I will bless Your name forever and ever.
Wimbo wa Sifa. Wa Daudi. Nitakutukuza wewe, Mungu wangu Mfalme, nitalisifu jina lako milele na milele.
2 Every day I will bless You, and I will praise Your name forever and ever.
Kila siku nitakusifu na kulitukuza jina lako milele na milele.
3 Great is the LORD and greatly to be praised; His greatness is unsearchable.
Bwana ni mkuu, anayestahili kusifiwa sana, ukuu wake haupimiki.
4 One generation will commend Your works to the next, and will proclaim Your mighty acts—
Kizazi kimoja kitasifia kazi zako kwa kizazi kingine, watasimulia matendo yako makuu.
5 the glorious splendor of Your majesty. And I will meditate on Your wondrous works.
Watasema juu ya utukufu wa fahari ya ukuu wako, nami nitatafakari juu ya kazi zako za ajabu.
6 They will proclaim the power of Your awesome deeds, and I will declare Your greatness.
Watasimulia uwezo wa kazi zako za kutisha, nami nitatangaza matendo yako makuu.
7 They will extol the fame of Your abundant goodness and sing joyfully of Your righteousness.
Wataadhimisha wema wako mwingi, na wataimba kwa shangwe juu ya haki yako.
8 The LORD is gracious and compassionate, slow to anger and abounding in loving devotion.
Bwana ni mwenye neema na mwingi wa huruma, si mwepesi wa hasira, bali ni mwingi wa upendo.
9 The LORD is good to all; His compassion rests on all He has made.
Bwana ni mwema kwa wote, ana huruma kwa vyote alivyovifanya.
10 All You have made will give You thanks, O LORD, and Your saints will bless You.
Ee Bwana, vyote ulivyovifanya vitakusifu, watakatifu wako watakutukuza.
11 They will tell of the glory of Your kingdom and speak of Your might,
Watasimulia utukufu wa ufalme wako na kusema juu ya ukuu wako,
12 to make known to men Your mighty acts and the glorious splendor of Your kingdom.
ili watu wote wajue matendo yako makuu na utukufu wa fahari ya ufalme wako.
13 Your kingdom is an everlasting kingdom, and Your dominion endures through all generations. The LORD is faithful in all His words and kind in all His actions.
Ufalme wako ni ufalme wa milele, mamlaka yako hudumu vizazi vyote. Bwana ni mwaminifu kwa ahadi zake zote na mwenye upendo kwa vyote alivyovifanya.
14 The LORD upholds all who fall and lifts up all who are bowed down.
Bwana huwategemeza wote waangukao, na huwainua wote waliolemewa na mizigo yao.
15 The eyes of all look to You, and You give them their food in season.
Macho yao wote yanakutazama wewe, nawe huwapa chakula chao wakati wake.
16 You open Your hand and satisfy the desire of every living thing.
Waufumbua mkono wako, watosheleza haja ya kila kitu kilicho hai.
17 The LORD is righteous in all His ways and kind in all His deeds.
Bwana ni mwenye haki katika njia zake zote, na mwenye upendo kwa vyote alivyovifanya.
18 The LORD is near to all who call on Him, to all who call out to Him in truth.
Bwana yu karibu na wote wamwitao, karibu na wote wamwitao kwa uaminifu.
19 He fulfills the desires of those who fear Him; He hears their cry and saves them.
Huwatimizia wamchao matakwa yao, husikia kilio chao na kuwaokoa.
20 The LORD preserves all who love Him, but all the wicked He will destroy.
Bwana huwalinda wote wampendao, bali waovu wote atawaangamiza.
21 My mouth will declare the praise of the LORD; let every creature bless His holy name forever and ever.
Kinywa changu kitazinena sifa za Bwana. Kila kiumbe na kilisifu jina lake takatifu milele na milele.