< Numbers 2 >

1 Then the LORD said to Moses and Aaron:
Bwana aliwaambia Mose na Aroni:
2 “The Israelites are to camp around the Tent of Meeting at a distance from it, each man under his standard, with the banners of his family.
“Waisraeli watapiga kambi zao kuzunguka Hema la Kukutania kwa umbali fulani kutoka kwenye hema, kila mwanaume chini ya alama yake pamoja na bendera ya jamaa yake.”
3 On the east side, toward the sunrise, the divisions of Judah are to camp under their standard: The leader of the descendants of Judah is Nahshon son of Amminadab,
Kwa upande wa mashariki kuelekea mawio ya jua, kambi ya makundi ya Yuda watapiga kambi chini ya alama yao. Kiongozi wa watu wa Yuda ni Nashoni mwana wa Aminadabu.
4 and his division numbers 74,600.
Kundi lake lina watu 74,600.
5 The tribe of Issachar will camp next to it. The leader of the Issacharites is Nethanel son of Zuar,
Kabila la Isakari watapiga kambi karibu na Yuda. Kiongozi wa watu wa Isakari ni Nethaneli mwana wa Suari.
6 and his division numbers 54,400.
Kundi lake lina watu 54,400.
7 Next will be the tribe of Zebulun. The leader of the Zebulunites is Eliab son of Helon,
Kabila la Zabuloni litafuata. Kiongozi wa watu wa Zabuloni ni Eliabu mwana wa Heloni.
8 and his division numbers 57,400.
Kundi lake lina watu 57,400.
9 The total number of men in the divisions of the camp of Judah is 186,400; they shall set out first.
Wanaume wote walio katika kambi ya Yuda, kufuatana na makundi yao, ni 186,400. Wao watatangulia kuondoka.
10 On the south side, the divisions of Reuben are to camp under their standard: The leader of the Reubenites is Elizur son of Shedeur,
Kwa upande wa kusini kutakuwa kambi ya makundi ya Reubeni chini ya alama yao. Kiongozi wa watu wa Reubeni ni Elisuri mwana wa Shedeuri.
11 and his division numbers 46,500.
Kundi lake lina watu 46,500.
12 The tribe of Simeon will camp next to it. The leader of the Simeonites is Shelumiel son of Zurishaddai,
Kabila la Simeoni watapiga kambi karibu na Reubeni. Kiongozi wa watu wa Simeoni ni Shelumieli mwana wa Surishadai.
13 and his division numbers 59,300.
Kundi lake lina watu 59,300.
14 Next will be the tribe of Gad. The leader of the Gadites is Eliasaph son of Deuel,
Kabila la Gadi litafuata. Kiongozi wa watu wa Gadi ni Eliasafu mwana wa Deueli.
15 and his division numbers 45,650.
Kundi lake lina watu 45,650.
16 The total number of men in the divisions of the camp of Reuben is 151,450; they shall set out second.
Wanaume wote walio katika kambi ya Reubeni, kufuatana na makundi yao, ni 151,450. Nao watakuwa nafasi ya pili kuondoka.
17 In the middle of the camps, the Tent of Meeting is to travel with the camp of the Levites. They are to set out in the order they encamped, each in his own place under his standard.
Kisha Hema la Kukutania na kambi ya Walawi vitakuwa katikati ya kambi zote. Wao watasafiri kwa utaratibu ule ule kama walivyopiga kambi, kila mmoja mahali pake mwenyewe chini ya alama yake.
18 On the west side, the divisions of Ephraim are to camp under their standard: The leader of the Ephraimites is Elishama son of Ammihud,
Upande wa magharibi kutakuwepo na kambi ya makundi ya Efraimu chini ya alama yao. Kiongozi wa watu wa Efraimu ni Elishama mwana wa Amihudi.
19 and his division numbers 40,500.
Kundi lake lina watu 40,500.
20 The tribe of Manasseh will be next to it. The leader of the Manassites is Gamaliel son of Pedahzur,
Kabila la Manase litafuata baada ya Efraimu. Kiongozi wa watu wa Manase ni Gamalieli mwana wa Pedasuri.
21 and his division numbers 32,200.
Kundi lake lina watu 32,200.
22 Next will be the tribe of Benjamin. The leader of the Benjamites is Abidan son of Gideoni,
Kabila la Benyamini litafuata baada ya Manase. Kiongozi wa watu wa Benyamini ni Abidani mwana wa Gideoni.
23 and his division numbers 35,400.
Kundi lake lina watu 35,400.
24 The total number of men in the divisions of the camp of Ephraim is 108,100; they shall set out third.
Wanaume wote walio katika kambi ya Efraimu kufuatana na makundi yao ni 108,100. Nao watakuwa nafasi ya tatu kuondoka.
25 On the north side, the divisions of Dan are to camp under their standard: The leader of the Danites is Ahiezer son of Ammishaddai,
Upande wa kaskazini kutakuwa na makundi ya kambi ya Dani, chini ya alama yao. Kiongozi wa watu wa Dani ni Ahiezeri mwana wa Amishadai.
26 and his division numbers 62,700.
Kundi lake lina watu 62,700.
27 The tribe of Asher will camp next to it. The leader of the Asherites is Pagiel son of Ocran,
Kabila la Asheri watapiga kambi karibu na Dani. Kiongozi wa watu wa Asheri ni Pagieli mwana wa Okrani.
28 and his division numbers 41,500.
Kundi lake lina watu 41,500.
29 Next will be the tribe of Naphtali. The leader of the Naphtalites is Ahira son of Enan,
Kabila la Naftali litafuata. Kiongozi wa watu wa Naftali ni Ahira mwana wa Enani.
30 and his division numbers 53,400.
Kundi lake lina watu 53,400.
31 The total number of men in the camp of Dan is 157,600; they shall set out last, under their standards.”
Wanaume wote walio katika kambi ya Dani ni 157,600. Wao watakuwa wa mwisho kuondoka chini ya alama yao.
32 These are the Israelites, numbered according to their families. The total of those counted in the camps, by their divisions, was 603,550.
Hawa ndio Waisraeli, wakiwa wamehesabiwa kufuatana na jamaa zao. Wote walio kambini kwa makundi yao ni watu 603,550.
33 But the Levites were not counted among the other Israelites, as the LORD had commanded Moses.
Hata hivyo, Walawi hawakuhesabiwa pamoja na Waisraeli wengine, kama Bwana alivyomwagiza Mose.
34 So the Israelites did everything the LORD commanded Moses; they camped under their standards in this way and set out in the same way, each man with his clan and his family.
Kwa hiyo Waisraeli wakafanya kila kitu Bwana alichomwamuru Mose. Hivyo ndivyo walivyopiga kambi chini ya alama zao, pia hivyo ndivyo walivyoondoka, kila mmoja akiwa na ukoo wake na jamaa yake.

< Numbers 2 >