< Leviticus 1 >
1 Then the LORD called to Moses and spoke to him from the Tent of Meeting, saying,
Bwana akamwita Mose na kusema naye kutoka kwenye Hema la Kukutania, akamwambia,
2 “Speak to the Israelites and tell them: When any of you brings an offering to the LORD, you may bring as your offering an animal from the herd or the flock.
“Sema na Waisraeli na uwaambie, ‘Yeyote miongoni mwenu aletapo sadaka ya mnyama kwa Bwana, alete mnyama kama sadaka yake kutoka kundi lake la ngʼombe au la kondoo na mbuzi.
3 If one’s offering is a burnt offering from the herd, he is to present an unblemished male. He must bring it to the entrance to the Tent of Meeting for its acceptance before the LORD.
“‘Kama sadaka hiyo ni ya kuteketezwa kutoka kwenye kundi la ngʼombe, atamtoa ngʼombe dume asiye na dosari. Ni lazima amlete kwenye ingilio la Hema la Kukutania ili aweze kukubalika kwa Bwana.
4 He is to lay his hand on the head of the burnt offering, so it can be accepted on his behalf to make atonement for him.
Ataweka mkono wake juu ya kichwa cha sadaka ya kuteketezwa, nayo itakubaliwa kwa niaba yake ili kufanya upatanisho kwa ajili yake.
5 And he shall slaughter the young bull before the LORD, and Aaron’s sons the priests are to present the blood and sprinkle it on all sides of the altar at the entrance to the Tent of Meeting.
Atamchinja yule fahali mchanga mbele za Bwana, kisha wana wa Aroni walio makuhani wataleta damu na kuinyunyiza pande zote za madhabahu yaliyo penye ingilio la Hema la Kukutania.
6 Next, he is to skin the burnt offering and cut it into pieces.
Ataichuna hiyo sadaka ya kuteketezwa na kuikata vipande vipande.
7 The sons of Aaron the priest shall put a fire on the altar and arrange wood on the fire.
Wana wa Aroni kuhani wataweka moto juu ya madhabahu na kupanga kuni juu ya huo moto.
8 Then Aaron’s sons the priests are to arrange the pieces, including the head and the fat, atop the burning wood on the altar.
Kisha wana wa Aroni walio makuhani watapanga vile vipande vya nyama, pamoja na kichwa na mafuta ya huyo mnyama juu ya zile kuni zinazowaka juu ya madhabahu.
9 The entrails and legs must be washed with water, and the priest shall burn all of it on the altar as a burnt offering, an offering made by fire, a pleasing aroma to the LORD.
Ataziosha sehemu za ndani na miguu yake kwa maji, naye kuhani atavichoma vyote juu ya madhabahu. Hii ni sadaka ya kuteketezwa, sadaka iliyotolewa kwa moto, yenye harufu nzuri ya kumpendeza Bwana.
10 If, however, one’s offering is a burnt offering from the flock—from the sheep or goats—he is to present an unblemished male.
“‘Kama sadaka ni ya kuteketezwa kutoka kwenye kundi la kondoo au mbuzi, atamtoa mnyama dume asiye na dosari.
11 He shall slaughter it on the north side of the altar before the LORD, and Aaron’s sons the priests are to sprinkle its blood against the altar on all sides.
Atamchinjia upande wa kaskazini wa madhabahu mbele za Bwana, nao wana wa Aroni walio makuhani watanyunyizia damu yake pande zote za madhabahu.
12 He is to cut the animal into pieces, and the priest shall arrange them, including the head and fat, atop the burning wood that is on the altar.
Atamkata vipande vipande, naye kuhani atavipanga, pamoja na kichwa na mafuta ya mnyama juu ya zile kuni zinazowaka juu ya madhabahu.
13 The entrails and legs must be washed with water, and the priest shall bring all of it and burn it on the altar; it is a burnt offering, an offering made by fire, a pleasing aroma to the LORD.
Ataosha sehemu za ndani na miguu kwa maji, naye kuhani atavileta vyote na kuvichoma juu ya madhabahu. Hii ni sadaka ya kuteketezwa, sadaka iliyotolewa kwa moto, harufu nzuri ya kumpendeza Bwana.
14 If, instead, one’s offering to the LORD is a burnt offering of birds, he is to present a turtledove or a young pigeon.
“‘Kama sadaka ya kuteketezwa inayotolewa kwa Bwana ni ndege, atamtoa hua au kinda la njiwa.
15 Then the priest shall bring it to the altar, twist off its head, and burn it on the altar; its blood should be drained out on the side of the altar.
Kuhani atamleta kwenye madhabahu, naye atamvunja shingo na kumnyofoa kichwa na kumchoma juu ya madhabahu. Damu yake itachuruzishwa ubavuni mwa madhabahu.
16 And he is to remove the crop with its contents and throw it to the east side of the altar, in the place for ashes.
Ataondoa kifuko cha chakula pamoja na uchafu wake na kuvitupa upande wa mashariki wa madhabahu, mahali pale penye majivu.
17 He shall tear it open by its wings, without dividing the bird completely. And the priest is to burn it on the altar atop the burning wood. It is a burnt offering, an offering made by fire, a pleasing aroma to the LORD.
Atampasua na kumweka wazi katika mabawa yake, lakini asimwachanishe kabisa, kisha kuhani ataichoma juu ya zile kuni zinazowaka juu ya madhabahu. Hii ni sadaka ya kuteketezwa, sadaka iliyotolewa kwa moto, harufu nzuri ya kumpendeza Bwana.