< James 5 >

1 Come now, you who are rich, weep and wail over the misery to come upon you.
Njoni sasa, enyi mlio matajiri, lieni kwa sauti ya juu kwa sababu ya taabu inayokuja juu yenu.
2 Your riches have rotted and moths have eaten your clothes.
Utajiri wenu umeharibiwa na mavazi yenu yametafunwa na wadudu waharibifu.
3 Your gold and silver are corroded. Their corrosion will testify against you and consume your flesh like fire. You have hoarded treasure in the last days.
Dhahabu zenu na fedha zenu zimekosa thamani, na uharibifu wake utashuhudia dhidi yenu na kuangamiza miili yenu kama moto. Mmejiwekea hazina yenu katika siku za mwisho.
4 Look, the wages you withheld from the workmen who mowed your fields are crying out against you. The cries of the harvesters have reached the ears of the Lord of Hosts.
Tazameni, malipo ya watendakazi-wale ambao hamjawalipa kwa kuvuna katika mashamba yenu- wanalia! Na kilio cha wale waliovuna mazao yenu kimeyafikia masikio ya Bwana wa Majeshi.
5 You have lived on earth in luxury and self-indulgence. You have fattened your hearts in the day of slaughter.
Mmeishi kwa anasa duniani na kujifurahisha ninyi wenyewe. Mmejinenepesha mioyo yenu kwa siku ya machinjo.
6 You have condemned and murdered the righteous, who did not resist you.
Mmemhukumu na kumuua mwenye haki asiyeweza kuwapinga.
7 Be patient, then, brothers, until the Lord’s coming. See how the farmer awaits the precious fruit of the soil—how patient he is for the fall and spring rains.
Kwa hiyo vumilieni, ndugu, mpaka ujio wa Bwana, kama mkulima husubiri mavuno ya thamani toka katika nchi, akisubiri kwa uvumilivu kwa ajili yake, mpaka mvua za kwanza na zile za mwisho zikinyesha.
8 You, too, be patient and strengthen your hearts, because the Lord’s coming is near.
Pia ninyi muwe wavumilivu; kazeni mioyo yenu, kwa sababu kuja kwake Bwana ni karibu.
9 Do not complain about one another, brothers, so that you will not be judged. Look, the Judge is standing at the door!
Ndugu, msinung'unikiane ninyi kwa ninyi, kusudi msije mkahukumiwa. Tazama, hakimu anasimama mlangoni.
10 Brothers, as an example of patience in affliction, take the prophets who spoke in the name of the Lord.
Kwa mfano, ndugu, angalieni mateso na uvumilivu wa manabii walionena katika jina la Bwana.
11 See how blessed we consider those who have persevered. You have heard of Job’s perseverance and have seen the outcome from the Lord. The Lord is full of compassion and mercy.
Tazama, twawaita wale wanaovumilia, “heri.” Mmesikia uvumilivu wa Ayubu, na mnalijua kusudi la Bwana kwa ajili ya Ayubu, ni kwa jinsi gani Bwana amejaa huruma na rehema.
12 Above all, my brothers, do not swear, not by heaven or earth or by any other oath. Simply let your “Yes” be yes, and your “No,” no, so that you will not fall under judgment.
Zaidi ya yote, ndugu zangu, msiape, aidha kwa mbingu ama kwa nchi, au kwa kiapo cha aina nyingine. Bali hebu “ndiyo” yenu na imaanishe “ndiyo” na “hapana” yenu na imaanishe “hapana,” ili kwamba msije kuangukia chini ya hukumu.
13 Is any one of you suffering? He should pray. Is anyone cheerful? He should sing praises.
Kuna yeyote miongoni mwenu ana mateso? Lazima aombe. Je, mtu yeyote ni mwenye kuchangamka? Na aimbe sifa.
14 Is any one of you sick? He should call the elders of the church to pray over him and anoint him with oil in the name of the Lord.
Je, kuna yeyote miongoni mwenu aliye mgonjwa? Na awaite wazee wa kanisa, nao wazee wa kanisa waombe juu yake, wakimpaka mafuta katika jina la Bwana,
15 And the prayer offered in faith will restore the one who is sick. The Lord will raise him up. If he has sinned, he will be forgiven.
na maombi ya imani yatamponya mgonjwa, na Bwana atamwinua. Na kama atakuwa ametenda dhambi, Mungu atamsamehe.
16 Therefore confess your sins to each other and pray for each other so that you may be healed. The prayer of a righteous man has great power to prevail.
Kwa hiyo ungameni dhambi zenu ninyi kwa ninyi, na kuombeana kila mmoja na mwenzake, ili muweze kuponywa. Maombi ya mwenye haki huzaa matokeo makubwa.
17 Elijah was a man just like us. He prayed earnestly that it would not rain, and it did not rain on the land for three and a half years.
Eliya alikuwa mtu mwenye hisia kama zetu, aliomba kwa juhudi kwamba mvua isinyeshe, na haikunyesha katika nchi kwa muda wa miaka mitatu na miezi sita.
18 Again he prayed, and the heavens gave rain, and the earth yielded its crops.
Na Eliya aliomba tena, na mbingu zilimwaga mvua juu ya nchi na nchi ikatoa mavuno.
19 My brothers, if one of you should wander from the truth and someone should bring him back,
Ndugu zangu, kama yeyote miongoni mwenu anapotoka kutoka kwenye ukweli, lakini mtu mwingine akamrejesha,
20 consider this: Whoever turns a sinner from the error of his way will save his soul from death and cover over a multitude of sins.
hebu na ajue kuwa yeyote amwongozaye mwenye dhambi kuondoka katika njia yake ya ukosaji ataponya nafsi yake kutoka katika mauti na atafunika wingi wa dhambi.

< James 5 >