< Hebrews 5 >
1 Every high priest is appointed from among men to represent them in matters relating to God, to offer gifts and sacrifices for sins.
Kwani kila kuhani mkuu, aliyechaguliwa kutoka miongoni mwa watu, amechaguliwa kusimama badala yao katika vitu vinavyohusiana na Mungu, ili aweze kutoa kwa pamoja zawadi na dhabihu kwa ajili ya dhambi.
2 He is able to deal gently with those who are ignorant and misguided, since he himself is beset by weakness.
Anaweza kujishughulisha kwa upole na wajinga na wabishi kwa kuwa yeye mwenyewe pia amezungukwa na udhaifu.
3 That is why he is obligated to offer sacrifices for his own sins, as well as for the sins of the people.
Kwa sababu ya hili, ana wajibu wa kutoa sadaka kwa ajili ya dhambi zake kama afanyavyo kwa dhambi za watu.
4 No one takes this honor upon himself; he must be called by God, just as Aaron was.
Na hakuna mtu achukuaye heshima hii kwa ajili yake mwenyewe, lakini badala yake, lazima aitwe na Mungu, kama alivyokuwa Haruni.
5 So also Christ did not take upon Himself the glory of becoming a high priest, but He was called by the One who said to Him: “You are My Son; today I have become Your Father.”
Hata Kristo hakujipa heshimu mwenyewe kwa kujifanya mwenyewe kuwa kuhani mkuu. Badala yake, Mungu alisema kwake, “Wewe ni mwanangu, leo nimekuwa Baba yako.”
6 And in another passage God says: “You are a priest forever in the order of Melchizedek.” (aiōn )
Ni kama asemavyo pia sehemu nyingine, “Wewe ni kuhani milele baada ya mfumo wa Melkizedeki.” (aiōn )
7 During the days of Jesus’ earthly life, He offered up prayers and petitions with loud cries and tears to the One who could save Him from death, and He was heard because of His reverence.
Wakati wa kipindi chake katika mwili, aliomba na kuombea, alimwomba Mungu kwa machozi, kwa yeye awezaye kumwokoa kutoka kwenye kifo. Kwa sababu ya unyenyekevu wake kwa Mungu, alisikiwa.
8 Although He was a Son, He learned obedience from what He suffered.
Ijapokuwa alikua mwana, alijifunza kutii kwa mambo yaliyomtesa.
9 And having been made perfect, He became the source of eternal salvation to all who obey Him (aiōnios )
Alikamilishwa na kwa njia hii alifanyika kwa kila mtu amwaminiye kuwa sababu ya wokovu wa milele, (aiōnios )
10 and was designated by God as high priest in the order of Melchizedek.
kwa kutengwa na Mungu kama kuhani Mkuu baada ya zamu ya Melkizedeki.
11 We have much to say about this, but it is hard to explain, because you are dull of hearing.
Tuna mengi ya kusema kuhusu Yesu, lakini ni vigumu kuwaelezea kwa kuwa ninyi ni wavivu wa kusikia.
12 Although by this time you ought to be teachers, you need someone to reteach you the basic principles of God’s word. You need milk, not solid food!
Ijapokuwa kwa kipindi hiki mlipaswa kuwa walimu, bado kuna umuhimu wa mtu kuwafundisha mafundisho ya awali ya kanuni za neno la Mungu. Mnahitaji maziwa na si chakula kigumu.
13 For everyone who lives on milk is still an infant, inexperienced in the message of righteousness.
Kwa kuwa yeyote anywaye maziwa tu hana uzoefu katika ujumbe wa haki, kwa kuwa bado ni mtoto.
14 But solid food is for the mature, who by constant use have trained their senses to distinguish good from evil.
Kwa upande mwingine, chakula kigumu ni cha watu wazima, wale ambao kwa sababu ya uzoefu wao katika kutofautisha haki na ubaya wamefundishwa kutambua jema na ovu.