< Hebrews 13 >

1 Continue in brotherly love.
Basi upendo wa ndugu na uendelee.
2 Do not neglect to show hospitality to strangers, for by so doing some people have entertained angels without knowing it.
Msisahau kuwakaribisha wageni, maana kwa kufanya hivi, baadhi wamewakaribisha malaika pasipo kujua.
3 Remember those in prison as if you were bound with them, and those who are mistreated as if you were suffering with them.
Kumbuka wote waliomo gerezani, kana kwamba mulikuwa nao kule pamoja nao, na kama miili yenu ilitendewa kama wao.
4 Marriage should be honored by all and the marriage bed kept undefiled, for God will judge the sexually immoral and adulterers.
Basi ndoa na iheshimiwe na wote na basi kitanda cha ndoa kifanywe kuwa safi, kwa maana Mungu atawahukumu waasherati na wazinzi.
5 Keep your lives free from the love of money and be content with what you have, for God has said: “Never will I leave you, never will I forsake you.”
Basi njia zenu za maisha ziwe huru katika upendo wa pesa. Muwe wanoridhika na vitu mulivyonavyo, kwani Mungu mwenyewe alisema, “Sitawaacha ninyi kamwe, wala kuwatelekeza ninyi.”
6 So we say with confidence: “The Lord is my helper; I will not be afraid. What can man do to me?”
Basi tulidhikeni ili tusema kwa ujasiri, “Bawa ni msaidizi wangu; Sitaogopa. Mwanadamu aweza kunifanya nini?”
7 Remember your leaders who spoke the word of God to you. Consider the outcome of their way of life and imitate their faith.
Wafikirieni wale walio waongoza, wale waliongea neno la Mungu kwenu, na kumbukeni matokeo ya mienendo yao; igeni imani zao.
8 Jesus Christ is the same yesterday and today and forever. (aiōn g165)
Yesu Kristo ni yeye jana, leo, na ata milele. (aiōn g165)
9 Do not be carried away by all kinds of strange teachings, for it is good for the heart to be strengthened by grace and not by foods of no value to those devoted to them.
Usije ukaongozwa na mafundisho mbalimbali ya kigeni kwani ni vizuri kwamba moyo ujengwe kwa neema, na siyo kwa sheria kuhusu chakula hayo hayatawasaidia wale wanaoishi kwa hayo.
10 We have an altar from which those who serve at the tabernacle have no right to eat.
Tunayo madhabau ambayo wale wanaotumika ndani ya hekalu hawana haki ya kula.
11 Although the high priest brings the blood of animals into the Holy Place as a sacrifice for sin, the bodies are burned outside the camp.
Kwa kuwa damu za wanyama, zilizotolewa dhabihu kwa ajili ya dhambi, ililetwa na kuhani mkuu ndani ya sehemu takatifu, lakini miili yao ilichomwa nje ya kambi.
12 And so Jesus also suffered outside the city gate, to sanctify the people by His own blood.
Kwa hiyo Yesu naye aliteseka nje ya lango la mji, hili kwamba kuweka wakfu watu kwa Mungu kupitia damu yake.
13 Therefore let us go to Him outside the camp, bearing the disgrace He bore.
Na kwa hiyo twendeni kwake nje ya kambi, tukizibeba fadheha zake.
14 For here we do not have a permanent city, but we are looking for the city that is to come.
Kwani hatuna makao ya kudumu katika mji huu. Badala yake tutafute mji ambao unakuja.
15 Through Jesus, therefore, let us continually offer to God a sacrifice of praise, the fruit of lips that confess His name.
Kupitia Yesu mnapaswa mara kwa mara kujitoa sadaka ya kumtukuza Mungu, kumsifu kwamba tunda la midomo yetu likili jina lake.
16 And do not neglect to do good and to share with others, for with such sacrifices God is pleased.
Na usisahau kufanya mazuri na kusadiana ninyi kwa ninyi, kwa kuwa ni kwa sadaka kama hiyo ndiyo Mungu hupendezwa sana.
17 Obey your leaders and submit to them, for they watch over your souls as those who must give an account. To this end, allow them to lead with joy and not with grief, for that would be of no advantage to you.
Tiini na kujishusha kwa viongozi wenu, kwani wanaendelea kuwalinda kwa ajili ya nafsi zenu, kama wale watakaotoa hesabu. Tiini ili kwamba viongozi wenu waweze kuwatunza kwa furaha, na sio kwa huzuni, ambayo haitawasaidia.
18 Pray for us; we are convinced that we have a clear conscience and desire to live honorably in every way.
Tuombeni, kwani tuna uhakikwa kwamba tuna dhamira njema, tunatamani kuishi maisha ya heshima katika mambo yote.
19 And I especially urge you to pray that I may be restored to you soon.
Na nyote ninawatia moyo zaidi mfanye hivi, ili kwamba niweze kurudi kwenu hivi karibuni.
20 Now may the God of peace, who through the blood of the eternal covenant brought back from the dead our Lord Jesus, that great Shepherd of the sheep, (aiōnios g166)
Sasa Mungu wa amani, ambaye aliwaleta tena kutoka kwa wafu mchungaji mkuu wa kondoo, Bwana wetu Yesu, kwa damu ya agano la milele, (aiōnios g166)
21 equip you with every good thing to do His will. And may He accomplish in us what is pleasing in His sight through Jesus Christ, to whom be glory forever and ever. Amen. (aiōn g165)
Atawapa uwezo kwa kila jambo zuri kufanya mapenzi yake, akifanya kazi ndani yetu iliyo njema ya kupendeza machoni pake, kupitia Yesu Kristo, kwake uwe utukufu milele na milele. Amina. (aiōn g165)
22 I urge you, brothers, to bear with my word of exhortation, for I have only written to you briefly.
Sasa ninakutia moyo, ndugu, kuchukualiana na neno la kutia moyo ambalo kwa ufupi nililiandika kwenu.
23 Be aware that our brother Timothy has been released. If he arrives soon, I will come with him to see you.
Fahamu kwamba ndugu yetu Timotheo ameshaachiwa huru, ambaye pamoja naye nitawaona kama atakuja hivi karibuni.
24 Greet all your leaders and all the saints. Those from Italy send you greetings.
Salimia viongozi wako wote na waumini wote. Wale wanaotoka Italia wanakusalimia.
25 Grace be with all of you.
Na neema iwe nanyi nyote.

< Hebrews 13 >