< Habakkuk 3 >
1 This is a prayer of Habakkuk the prophet, according to Shigionoth:
Maombi ya Habakuki nabii:
2 O LORD, I have heard the report of You; I stand in awe, O LORD, of Your deeds. Revive them in these years; make them known in these years. In Your wrath, remember mercy!
Yahwe, nimesikia taarifa zako, na mimi naogopa. Yahwe, fufua kazi yako katikati wakati; katikati ya muda huu; fanya hiyo ijulikane; kumbuka kuwa na rehema katika ghadhabu yako.
3 God came from Teman, and the Holy One from Mount Paran. (Selah) His glory covered the heavens, and His praise filled the earth.
Mungu alikuja kutoka Temani, na yule Mtakatifu kutoka Parani. (Sela) Utukufu wake umezifunika mbingu, na dunia ilikuwa imejaa utukufu wake.
4 His radiance was like the sunlight; rays flashed from His hand, where His power is hidden.
Miali miwili ya mikono yake ilikuwa iking'aa kama mwanga, ambapo uweza wake ulifichwa.
5 Plague went before Him, and fever followed in His steps.
Ugonjwa wa kuua ulitangulia mbele yake, na adha iliifuta miguu yake.
6 He stood and measured the earth; He looked and startled the nations; the ancient mountains crumbled; the perpetual hills collapsed. His ways are everlasting.
Yeye alisimama na akaipima nchi; aliangalia na aliyatikisa mataifa. Hata milima ya milele iliharibiwa kabisa, na vilima vya milele vilianguka chini. Njia yake ni ya milele.
7 I saw the tents of Cushan in distress; the curtains of Midian were trembling.
Niliona mahema ya Wakushi katika mateso, na vitambaa vya mahema katika Midiani vinatetema.
8 Were You angry at the rivers, O LORD? Was Your wrath against the streams? Did You rage against the sea when You rode on Your horses, on Your chariots of salvation?
Yahwe alikuwa na hasira pale mtoni? Ghadhabu yako ilikuwa dhidi ya mito, au hasira yako dhidi ya bahari, unapopanda juu ya farasi wenye mikokoteni na wa ushindi wako?
9 You brandished Your bow; You called for many arrows. (Selah) You split the earth with rivers.
Umeleta upinde wako bila mfuniko; unaweka mishale kwenye upinde wako! (Sela) uliigawa nchi na mito.
10 The mountains saw You and quaked; torrents of water swept by. The deep roared with its voice and lifted its hands on high.
Milima ilikuona wewe na kugeuka kwa huzuni. Maji yaliyomwagwa chini yalipita juu yao; kina cha bahari kilipaza sauti. Mawimbi yake yakainuka juu.
11 Sun and moon stood still in their places at the flash of Your flying arrows, at the brightness of Your shining spear.
Jua na mwezi vilisimama imara juu mahali pake katika mwanga wa mishale yako na ilipaa, pale katika uangavu wa mwanga wa mikuki yako.
12 You marched across the earth with fury; You threshed the nations in wrath.
Umetembea juu ya nchi kwa uchungu. Katika ghadhabu umepukuchua mataifa.
13 You went forth for the salvation of Your people, to save Your anointed. You crushed the head of the house of the wicked and stripped him from head to toe.
Ulikwenda nje kwaajili ya wokovu wa watu wako, Kwaajili ya wokovu wa mteule wako. Wewe pondaponda kichwa cha nyumba ya mwovu kuweka wazi msingi wa shingo. (Sela)
14 With his own spear You pierced his head, when his warriors stormed out to scatter us, gloating as though ready to secretly devour the weak.
Umekichoma kichwa cha wapiganaji wake kwa mshale wake mwenyewe sababu walikuja kama upepo kututawanya sisi, wivu wao ulikuwa kama mtu ambaye anamteketeza masikini katika mahali pamaficho.
15 You trampled the sea with Your horses, churning the great waters.
Umesafiri juu ya bahari kwa farasi wako, na kuyapita maji makuu.
16 I heard and trembled within; my lips quivered at the sound. Decay entered my bones; I trembled where I stood. Yet I must wait patiently for the day of distress to come upon the people who invade us.
Nilisikia, na ndani yangu nilitetemeka! midomo yangu ilitetemesha sauti. Uozo unakuja katika mifupa yangu, na chini yangu mwenyewe nilitetemeka kama nasubiri kwaajili ya siku ya kuhuzunisha ifike juu ya watu waliotushambulia sisi.
17 Though the fig tree does not bud and no fruit is on the vines, though the olive crop fails and the fields produce no food, though the sheep are cut off from the fold and no cattle are in the stalls,
Ingawa mtini hauchipui na hauzai kutokana na mzababibu; na ingawa kuzaa kwa mti wa mzaituni hakuridhishi na mashamba hayatoi chakula; na ingawa kundi mifugo limetoweka na hakuna ng'ombe katika zizi, hiki ndicho nitakacho kifanya.
18 yet I will exult in the LORD; I will rejoice in the God of my salvation!
Bado, nitafurahia katika Yahwe. Nitakuwa nafuraha kwa sababu ya Mungu wa wokovu wangu.
19 GOD the Lord is my strength; He makes my feet like those of a deer; He makes me walk upon the heights!
Bwana Yahwe ni nguvu yangu na anaifanya miguu yangu kama ya kulungu. Ananifanya mimi niende mbele mahali pangu pa juu. - kufuata maelekezo ya muziki, katika vyombo vyangu vya nyuzi.