< Exodus 36 >
1 “So Bezalel, Oholiab, and every skilled person are to carry out everything commanded by the LORD, who has given them skill and ability to know how to perform all the work of constructing the sanctuary.”
Hivyo Bezaleli na Oholiabu na kila mtu mwenye ustadi ambaye Yahweh aliye mpa ustadi na uwezo kujua jinsi ya kufanya kazi katika ujenzi wa sehemu takatifu wafanye kazi kadiri ya yote Yahweh aliyo amuru.”
2 Then Moses summoned Bezalel, Oholiab, and every skilled person whom the LORD had gifted—everyone whose heart stirred him to come and do the work.
Musa akamuita Bezaleli, Oholiabu, na kila mtu mwenye ujuzi ambaye Yahweh kampa ujuzi, na ambaye moyoni mwake ulichochewa kuja na kufanya kazi.
3 They received from Moses all the contributions that the Israelites had brought to carry out the service of constructing the sanctuary. Meanwhile, the people continued to bring freewill offerings morning after morning,
Walipokea kutoka kwa Musa sadaka zote ambazo Waisraeli walizo leta kwa ujenzi ya sehemu takatifu. Watu walikuwa bado wanaleta sadaka za hiari kila asubui kwa Musa.
4 so that all the skilled craftsmen who were doing all the work on the sanctuary left their work
Hivyo watu wote walikuwa na ujuzi walikuwa wakifanya kazi sehemu takatifu walikuja kutoka kwenye kazi walikuwa wakifanya.
5 and said to Moses, “The people are bringing more than enough for doing the work the LORD has commanded us to do.”
Wachonga mawe walimwabia Musa, “Watu wanaleta zaidi sana ya yanayo itajika kufanya kazi Yahweh aliyo tuamuru.”
6 After Moses had given an order, they sent a proclamation throughout the camp: “No man or woman should make anything else as an offering for the sanctuary.” So the people were restrained from bringing more,
Hivyo Musa akaamuru mtu yeyote asilete tena kwa ujenzi wa sehemu takatifu. Kisha watu wakaacha kuleta hivi vitu.
7 since what they already had was more than enough to perform all the work.
Walikuwa na zaidi ya vitu vya ujenzi.
8 All the skilled craftsmen among the workmen made the ten curtains for the tabernacle. They were made of finely spun linen, as well as blue, purple, and scarlet yarn, with cherubim skillfully worked into them.
Hivyo wachonga mawe miongoni mwao wakajenga lile hema la kuabudia kwa mapazia kumi yaliyo jengwa kitamba kizuri na buluu, zambarau, na sufu nyekundu kwa aina ya kerubi. Hii ni kazi ya Bezaleli, mjenzi mwenye ujuzi sana.
9 Each curtain was twenty-eight cubits long and four cubits wide; all the curtains were the same size.
Urefu wa kila pazia ulikuwa mikono ishirini na nane, nao upana wa kila kitambaa ulikuwa mikono minne. Vitambaa vyote hivyo vilikuwa na kipimo kimoja.
10 And he joined five of the curtains together, and the other five he joined as well.
Bezaleli akaunganisha vitambaa vitano pamoja, na vile vitambaa vingine vitano akaviunganisha pamoja.
11 He made loops of blue material on the edge of the end curtain in the first set, and also on the end curtain in the second set.
Kisha akafanya vitanzi vya uzi wa bluu kwenye upindo wa kitambaa kilicho mahali pa kuungania. Akafanya vivyo hivyo kwenye upindo wa kitambaa cha nje kabisa kilicho mahali pale pengine pa kuungania.
12 He made fifty loops on one curtain and fifty loops on the end curtain of the second set, so that the loops lined up opposite one another.
Akafanya vitanzi hamsini kwenye kitambaa kimoja, akafanya vitanzi hamsini kwenye mwisho wa kitambaa kilichokuwa mahali pale pengine pa kuungania, vitanzi hivyo vikiwa vinaelekeana.
13 He also made fifty gold clasps to join the curtains together, so that the tabernacle was a unit.
Mwishowe akafanya kulabu hamsini za dhahabu na kuviunganisha vitambaa hivyo pamoja kwa kulabu hizo, hivi kwamba hiyo ikawa maskani moja.
14 He then made curtains of goat hair for the tent over the tabernacle—eleven curtains in all.
Bezaleli akafanya vitambaa vya mahema vya manyoya ya mbuzi kwa ajili ya hema lililo juu ya maskani. Vitambaa kumi na moja ndivyo alivyofanyiza.
15 Each of the eleven curtains was the same size—thirty cubits long and four cubits wide.
Urefu wa kila kitambaa ulikuwa mikono thelathini, nao upana wa kila kitambaa ulikuwa mikono minne. Vitambaa hivyo kumi na moja vilikuwa na kipimo kimoja.
16 He joined five of the curtains into one set and the other six into another.
Kisha akaunganisha vitambaa vitano pamoja na vile vitambaa vingine sita pamoja.
17 He made fifty loops along the edge of the end curtain in the first set, and fifty loops along the edge of the corresponding curtain in the second set.
Kisha akafanya vitanzi hamsini kwenye upindo wa kitambaa cha nje kabisa kilicho mahali pa kuungania, naye akafanya vitanzi hamsini kwenye upindo wa kile kitambaa kingine kilichoungana nacho.
18 He also made fifty bronze clasps to join the tent together as a unit.
Bezaleli akafanya kulabu hamsini za shaba kwa ajili ya kuliunganisha hilo hema pamoja liwe kipande kimoja.
19 Additionally, he made for the tent a covering of ram skins dyed red, and over that a covering of fine leather.
Naye akafanya kifuniko cha hema kutokana na ngozi za kondoo dume zilizotiwa rangi nyekundu na kifuniko kutokana na ngozi za sili, upande wa juu.
20 Next, he constructed upright frames of acacia wood for the tabernacle.
Bezaleli akafanya viunzi vya mbao vya hema ya kukutani kutokana na mbao za mshita.
21 Each frame was ten cubits long and a cubit and a half wide.
Urefu wa kiunzi ulikuwa mikono kumi, nao upana wa kila kiunzi ulikuwa mkono mmoja na nusu.
22 Two tenons were connected to each other for each frame. He made all the frames of the tabernacle in this way.
Kila kiunzi kilikuwa na ndimi mbili zilizounganishwa. Hivyo ndivyo alivyofanya viunzi vyote vya maskani.
23 He constructed twenty frames for the south side of the tabernacle,
Basi akafanya viunzi vya maskani, viunzi ishirini kwa ajili ya upande kuelekea kusini.
24 with forty silver bases to put under the twenty frames—two bases for each frame, one under each tenon.
Bezaleli akafanya vikalio arobaini vya fedha viwe chini ya vile viunzi ishirini, vikalio viwili chini ya kiunzi kimoja pamoja na ndimi zake mbili na vikalio vingine viwili chini ya kiunzi kingine pamoja na ndimi zake mbili.
25 For the second side of the tabernacle, the north side, he made twenty frames
Na kwa ajili ya ule upande mwingine wa maskani, upande wa kaskazini, akafanya viunzi ishirini
26 and forty silver bases—two bases under each frame.
na vikalio vyake arobaini vya fedha. Vikalio viwili chini ya kiunzi kimoja na vikalio viwili chini ya kiunzi kingine
27 He made six frames for the rear of the tabernacle, the west side,
Na kwa ajili ya zile pande za nyuma za maskani kuelekea magharibi akafanya viunzi sita.
28 and two frames for the two back corners of the tabernacle,
Naye akafanya viunzi viwili vya pembeni ya maskani kwenye pande zake mbili za nyuma
29 coupled together from bottom to top and fitted into a single ring. He made both corners in this way.
Hizi zilikuwa pacha upande wa chini, lakini juu ya kila moja kwenye pete ya kwanza. Hivyo ndivyo alivyoifanya yote miwili, ile miimo ya pembeni.
30 So there were eight frames and sixteen silver bases—two under each frame.
Basi vikajumlika kuwa viunzi vinane na vikalio vyake kumi na sita vya fedha, vikalio viwili kando ya vikalio viwili chini ya kila kiunzi.
31 He also made five crossbars of acacia wood for the frames on one side of the tabernacle,
Bezaleli akafanya miti ya mshita, mitano kwa ajili ya viunzi vya upande mmoja wa maskani,
32 five for those on the other side, and five for those on the rear side of the tabernacle, to the west.
na miti mitano kwa ajili ya viunzi vya upande ule mwingine wa maskani na miti mitano kwa ajili ya viunzi vya maskani kwa ajili ya zile pande mbili za nyuma za magharibi.
33 He made the central crossbar to run through the center of the frames, from one end to the other.
Kisha akafanya mti wa katikati upitie katikati ya vile viunzi toka mwisho mmoja mpaka ule mwingine.
34 And he overlaid the frames with gold and made gold rings to hold the crossbars. He also overlaid the crossbars with gold.
Naye akavifunika vile viunzi kwa dhahabu, akafanyiza pete zake za dhahabu ziwe vitegemezo kwa ajili ya ile miti, akaifunika ile miti kwa dhahabu.
35 Next, he made the veil of blue, purple, and scarlet yarn, and finely spun linen, with cherubim skillfully worked into it.
Bezaleli akafanya pazia, la uzi wa bluu na sufu iliyotiwa rangi ya zambarau na kitambaa cha rangi nyekundu ya kochinili na kitani bora kilichosokotwa, kalitia makerubi kwa kazi ya mjenzi.
36 He also made four posts of acacia wood for it and overlaid them with gold, along with gold hooks; and he cast four silver bases for the posts.
Kisha akalifanyia nguzo nne za mshita na kuzifunika kwa dhahabu, vibanio vyake vikiwa vya dhahabu, na kutengeneza vikalio vinne vya fedha kwa ajili yake.
37 For the entrance to the tent, he made a curtain embroidered with blue, purple, and scarlet yarn, and finely spun linen,
Naye akafanya kisitiri kwa ajili ya mwingilio wa hema kutokana na uzi wa bluu na sufu iliyotiwa rangi ya zambarau na kitambaa chenye rangi nyekundu ya kochinili na kitani bora kilichosokotwa, kazi ya mfumaji.
38 together with five posts and their hooks. He overlaid the tops of the posts and their bands with gold, and their five bases were bronze.
Pia akafanya na nguzo zake tano na vibanio vyake. Naye akavifunika vilele vyake na viungo vyake kwa dhahabu, lakini vile vikalio vyake vitano vilikuwa vya shaba.