< Mark 15 >

1 And forthwith in the morning, the chief priests, with the elders and scribes, and the whole Sanhedrin, having held a consultation, and having bound Jesus, led him away, and delivered him to Pilate.
Kulipopambazuka, makuhani wakuu walifanya shauri pamoja na wazee, walimu wa Sheria na Baraza lote, wakamfunga Yesu pingu, wakampeleka na kumkabidhi kwa Pilato.
2 And Pilate asked him: Are you the King of the Jews? And he answering, said: You say it.
Pilato akamwuliza Yesu, “Je, wewe ni mfalme wa Wayahudi?” Yesu akajibu, “Wewe umesema.”
3 And the chief priests accused him of many things.
Makuhani wakuu wakamshtaki Yesu mambo mengi.
4 Pilate again asked him, saying: Do you make no answer? See, how many things they testify against you.
Pilato akamwuliza tena Yesu, “Je, hujibu neno? Tazama wanavyotoa mashtaka mengi juu yako.”
5 But Jesus gave no further answer; so that Pilate was astonished.
Lakini Yesu hakujibu neno, hata pilato akashangaa.
6 Now it was his custom to release to them, at the feast, one prisoner, whomever they desired.
Kila wakati wa sikukuu ya Pasaka, Pilato alikuwa na desturi ya kuwafungulia mfungwa mmoja waliyemtaka.
7 And there was one called Barabbas, lying bound with his fellow-insurgents, who had committed murder in the insurrection.
Basi, kulikuwa na mtu mmoja aitwaye Baraba, ambaye alikuwa amefungwa pamoja na waasi wengine kwa kusababisha uasi na mauaji.
8 And the multitude cried out, and began to ask him to do as he had always done for them.
Watu wengi wakamwendea Pilato wakamwomba awafanyie kama kawaida yake.
9 But Pilate answered them, saying: Do you wish me to release to you the King of the Jews?
Pilato akawauliza, “Je, mwataka niwafungulieni Mfalme wa Wayahudi?”
10 For he knew that, through envy, the chief priests had delivered him up.
Alisema hivyo kwa sababu alijua wazi kwamba makuhani wakuu walimkabidhi Yesu kwake kwa sababu ya wivu.
11 But the chief priests instigated the multitude, that he should rather release Barabbas to them.
Lakini makuhani wakuu wakawachochea watu wamwombe Pilato awafungulie Baraba.
12 And Pilate answered and said again to them: What, then, do you wish me to do with him whom you call the King of the Jews?
Pilato akawauliza tena, “Basi, sasa mwataka nifanye nini na mtu huyu mnayemwita Mfalme wa Wayahudi?”
13 They again cried out: Crucify him.
Watu wote wakapaaza sauti tena: “Msulubishe!”
14 But Pilate said to them: Why, what evil has he done? But they cried vehemently: Crucify him.
Lakini Pilato akawauliza, “Kwa nini! Amefanya kosa gani?” Lakini wao wakazidi kupaaza sauti, “Msulubishe!”
15 And Pilate, willing to gratify the multitude, released to them Barabbas; and delivered Jesus, after he had scourged him, to be crucified.
Pilato alitaka kuuridhisha huo umati wa watu; basi, akamwachilia Baraba kutoka gerezani. Akaamuru Yesu apigwe viboko, kisha akamtoa asulubiwe.
16 And the soldiers led him away within the court, which is the governor’s house, and called together the whole band.
Kisha askari walimpeleka Yesu ndani ukumbini, katika ikulu, wakakusanya kikosi kizima cha askari.
17 And they clothed him in purple; and having plaited a crown of thorn branches, they put it on him,
Wakamvika vazi la rangi ya zambarau, wakasokota taji ya miiba, wakamwekea kichwani.
18 and began to salute him: Hail, King of the Jews!
Wakaanza kumsalimu, “Shikamoo Mfalme wa Wayahudi!”
19 And they struck him on the head with a reed, and spit upon him, and bowing their knees, did him homage.
Wakampiga kichwani kwa mwanzi, wakamtemea mate; wakampigia magoti na kumsujudia.
20 And when they had derided him, they took off the purple from him, and put his own clothes on him, and led him out to crucify him.
Baada ya kumdhihaki, walimvua lile joho, wakamvika nguo zake, kisha wakampeleka kumsulubisha.
21 And they compelled one Simon, a Cyrenian, (the father of Alexander and Rufus, ) who was passing by, coming in from the country, to bear his cross.
Walipokuwa njiani, walikutana na mtu mmoja aitwaye Simoni, mwenyeji wa Kurene. Yeye alikuwa baba wa Aleksanda na Rufo, na wakati huo alikuwa akitoka shambani. Basi, wakamlazimisha auchukue msalaba wa Yesu.
22 And they brought him to the place Golgotha, which is, when translated, the place of a skull.
Kisha wakampeleka Yesu mpaka mahali palipoitwa Golgotha, maana yake, “Mahali pa Fuvu la Kichwa.”
23 And they gave him wine mingled with myrrh, to drink: but he did not receive it.
Wakampa divai iliyochanganywa na manemane, lakini yeye akaikataa.
24 And when they had crucified him, they divided his clothes among themselves, casting lots for them, what each one should take.
Basi, wakamsulubisha, wakagawana mavazi yake kwa kuyapigia kura waamue nani angepata nini.
25 And it was the third hour, and they crucified him.
Ilikuwa saa tatu asubuhi walipomsulubisha.
26 And the superscription containing his accusation was written above him: THE KING OF THE JEWS.
Na mshtaka wake ulikuwa umeandikwa: “Mfalme wa Wayahudi.”
27 And with him they crucified two robbers, one on his right hand, and the other on his left.
Pamoja naye waliwasulubisha wanyang'anyi wawili, mmoja upande wake wa kulia na mwingine upande wake wa kushoto.
28 And the scripture was fulfilled, which says: And he was numbered with transgressors.
Hapo yakatimia Maandiko Matakatifu yanayosema, “Aliwekwa kundi moja na waovu.”
29 And those who passed by reviled him, shaking their heads, and saying: Aha! you that destroy the temple, and build it in three days,
Watu waliokuwa wanapita mahali hapo walimtukana, wakitikisa vichwa vyao na kusema, “Aha! Wewe mwenye kuvunja Hekalu na kulijenga kwa siku tatu!
30 save yourself, and come down from the cross.
Sasa, shuka msalabani ujiokoe mwenyewe!”
31 Likewise the chief priests, with the scribes, speaking in derision one to another, said: He saved others; himself he can not save.
Nao makuhani wakuu pamoja na walimu wa Sheria walimdhihaki wakisema, “Aliwaokoa wengine, lakini kujiokoa mwenyewe hawezi!
32 Let the Christ, the King of Israel, come down now from the cross, that we may see and believe. Those also who were crucified with him, reproached him.
Eti yeye ni Kristo, Mfalme wa Israeli! Basi, na ashuke msalabani ili tuone na kuamini.” Hata watu wale waliosulubiwa pamoja naye walimtukana.
33 And when the sixth hour had come, there was darkness over the whole land, till the ninth hour.
Tangu saa sita mchana mpaka saa tisa kulikuwa giza nchini kote.
34 And at the ninth hour, Jesus cried with a loud voice, saying: Eloi, Eloi, lamma sabachthani? which is, when translated, My God, my God, why hast thou forsaken me?
Saa tisa alasiri Yesu akalia kwa sauti kubwa, “Eloi, Eloi, lema sabakthani?” Maana yake, “Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?”
35 And some of those who stood by, when they heard it, said: Behold, he calls for Elijah.
Baadhi ya watu waliosimama pale waliposikia hivyo, walisema, “Sikiliza! Anamwita Eliya!”
36 And one ran, and filled a sponge with vinegar, and put it on a reed, and gave it to him to drink, saying: Wait; let us see if Elijah is coming to take him down.
Mtu mmoja akakimbia, akachovya sifongo katika siki, akaiweka juu ya mwanzi, akampa anywe akisema, “Hebu tuone kama Eliya atakuja kumteremsha msalabani!”
37 But Jesus, having cried with a loud voice, gave up his spirit.
Yesu akapaaza sauti kubwa, akakata roho.
38 And the vail of the temple was rent in two, from the top to the bottom.
Basi, pazia la Hekalu likapasuka vipande viwili toka juu mpaka chini.
39 And when the centurion that was standing opposite him, saw that he thus cried out, and gave up his spirit, he said: Truly, this man was the Son of God.
Jemadari mmoja aliyekuwa amesimama mbele yake aliona jinsi Yesu alivyolia kwa sauti na kukata roho, akasema, “Kweli mtu huyu alikuwa Mwana wa Mungu!”
40 And there were, at a distance, women also, looking on; among whom were Mary Magdalene, and Mary the mother of James the younger and of Joses, and Salome;
Walikuwako pia wanawake waliotazama kwa mbali, miongoni mwao akiwa Maria toka mji wa Magdala, Salome, na Maria mama wa kina Yakobo mdogo na Yose.
41 who also, when he was in Galilee, followed him, and ministered to him; and many other women, who had come up with him to Jerusalem.
Hawa walimfuata Yesu alipokuwa Galilaya na kumtumikia. Kulikuwa na wanawake wengine wengi waliokuja Yerusalemu pamoja naye.
42 And when the evening had come, because it was the preparation, which is the eve of the sabbath,
Wakati wa jioni ulikuwa umekwisha fika. Hiyo ilikuwa siku ya Maandalio, yaani siku inayotangulia Sabato.
43 Joseph of Arimathea, an honorable counselor, who was himself looking for the kingdom of God, came, and went in boldly to Pilate, and asked for the body of Jesus.
Hapo akaja Yosefu mwenyeji wa Armathaya, mjumbe wa Baraza Kuu, aliyeheshimika sana. Yeye pia alikuwa anatazamia kuja kwa Ufalme wa Mungu. Basi, alimwendea Pilato bila uoga, akaomba apewe mwili wa Yesu.
44 But Pilate was astonished that he was already dead; and having called the centurion to him, he inquired of him whether he had been any while dead.
Pilato alishangaa kusikia kwamba Yesu alikuwa amekwisha kufa. Basi, akamwita jemadari, akamwuliza kama Yesu alikuwa amekufa kitambo.
45 And having learned the fact from the centurion, he gave the body to Joseph.
Pilato alipoarifiwa na huyo jemadari kwamba Yesu alikuwa amekwisha kufa, akamruhusu Yosefu auchukue mwili wake.
46 And he bought fine linen, and took him down, and wrapped him in the linen, and laid him in a sepulcher that had been hewed out of a rock: and he rolled a stone to the door of the sepulcher.
Hapo Yosefu akanunua sanda ya kitani, akauteremsha chini huo mwili, akauzungushia sanda. Akauweka katika kaburi lililokuwa limechongwa mwambani, kisha akavingirisha jiwe kubwa mbele ya mlango.
47 And Mary Magdalene and Mary the mother of Joses saw where he was laid.
Nao Maria Magdalene na Maria mama yake Yose walipaona hapo alipolazwa.

< Mark 15 >