< John 18 >

1 When Jesus had spoken these things, he went out with his disciples beyond the brook Kedron, where was a garden, which he and his disciples entered.
Yesu alipokwisha sema hayo, alikwenda ng'ambo ya kijito Kedroni, pamoja na wanafunzi wake. Mahali hapo palikuwa na bustani, naye Yesu akaingia humo pamoja na wanafunzi wake.
2 And Judas, who delivered him up, also knew the place, because Jesus often went thither with his disciples.
Yuda, aliyemsaliti Yesu, alipajua mahali hapo kwani mara nyingi Yesu alikutana na wanafunzi wake huko.
3 Judas, then, having received the band of soldiers and attendants from the chief priests and Pharisees, came thither with torches and lamps and weapons.
Basi, Yuda alichukua kikosi cha askari na walinzi kutoka kwa makuhani wakuu na Mafarisayo, akaja nao bustanini wakiwa na taa, mienge na silaha.
4 Then Jesus, knowing all things that were coming upon him, went forth, and said to them: Whom do you seek?
Yesu, hali akijua yote yatakayompata, akatokea, akawauliza, “Mnamtafuta nani?”
5 They answered him: Jesus the Nazarene. Jesus said to them: I am he. Judas, also, who delivered him up, was standing among them.
Nao wakamjibu, “Yesu wa Nazareti!” Yesu akawaambia, “Mimi ndiye.” Msaliti Yuda alikuwa amesimama hapo pamoja nao.
6 Then, when he said to them, I am he, they went backward, and fell to the ground.
Basi, Yesu alipowaambia: “Mimi ndiye”, wakarudi nyuma, wakaanguka chini.
7 Then he asked them again: Whom do you seek? They said: Jesus the Nazarene.
Yesu akawauliza tena, “Mnamtafuta nani?” Wakamjibu, “Yesu wa Nazareti!”
8 Jesus answered: I have told you that I am he. If, then, you seek me, let these go away.
Yesu akawaambia, “Nimekwisha waambieni kwamba mimi ndiye. Basi, kama mnanitafuta mimi, waacheni hawa waende zao.”
9 This he said, that the word might be fulfilled which he had spoken: Of those whom thou hast given me; I have lost none.
(Alisema hayo ili yapate kutimia yale aliyosema: “Wale ulionipa sikumpoteza hata mmoja.”)
10 Then Simon Peter, who had a sword, drew it, and struck the servant of the chief priest, and cut off his right ear. The name of the servant was Malchus.
Simoni Petro alikuwa na upanga; basi, akauchomoa, akamkata sikio la kulia mtumishi wa Kuhani Mkuu. Mtumishi huyo aliitwa Malko.
11 Then Jesus said to Peter: Put up your sword into its scabbard. Shall I not drink the cup that my Father has given me?
Basi, Yesu akamwambia Petro, “Rudisha upanga wako alani. Je, nisinywe kikombe alichonipa Baba?”
12 Then the band of soldiers, and the officer, and the attendants of the Jews, took Jesus and bound him,
Kile kikosi cha askari, mkuu wake na walinzi wa Wayahudi walimkamata Yesu, wakamfunga
13 and led him first to Annas; for he was the father-in-law of Caiaphas, who was chief priest that year.
na kumpeleka kwanza kwa Anasi; Anasi alikuwa baba mkwe wa Kayafa ambaye alikuwa Kuhani Mkuu mwaka huo.
14 It was Caiaphas who had given counsel to the Jews, that it was profitable that one man should die for the people.
Huyo Kayafa ndiye aliyekuwa amewashauri Wayahudi kwamba ni afadhali mtu mmoja afe kwa ajili ya taifa.
15 And Simon Peter followed Jesus, and so did another disciple. And that other disciple was acquainted with the chief priest, and he went in with Jesus into the palace of the chief priest.
Simoni Petro pamoja na mwanafunzi mwingine walimfuata Yesu. Huyo mwanafunzi mwingine alikuwa anajulikana kwa Kuhani Mkuu, hivyo aliingia pamoja na Yesu ndani ya ukumbi wa Kuhani Mkuu.
16 But Peter stood without near the door. Then the other disciple, who was acquainted with the chief priest, went out and spoke to the door-keeper, and brought Peter in.
Lakini Petro alikuwa amesimama nje, karibu na mlango. Basi, huyo mwanafunzi mwingine aliyekuwa anajulikana kwa Kuhani Mkuu alitoka nje akasema na mjakazi, mngoja mlango, akamwingiza Petro ndani.
17 Then the maid-servant who kept the door said to Peter: Are you not also one of the disciples of this man? He said: I am not.
Huyo msichana mngoja mlango akamwuliza Petro, “Je, nawe pia ni mmoja wa wanafunzi wa mtu huyu?” Petro akamwambia, “Si mimi!”
18 And the servants and the attendants, having made a fire of coals, for it was cold, were standing and warming themselves. And Peter stood with them, and warmed himself.
Watumishi na walinzi walikuwa wamewasha moto kwa sababu kulikuwa na baridi, wakawa wanaota moto. Naye Petro alikuwa amesimama pamoja nao akiota moto.
19 Then the chief priest questioned Jesus concerning his disciples and his teaching.
Basi, Kuhani akamwuliza Yesu juu ya wanafunzi wake na mafundisho yake.
20 Jesus answered him: I have spoken openly to the world; I always taught in the synagogue, and in the temple, where the Jews come together, and in secret I have spoken nothing.
Yesu akamjibu, “Nimesema na kila mtu daima hadharani. Kila mara nimefundisha katika masunagogi na Hekaluni, mahali wakutanikiapo Wayahudi wote; na wala sijasema chochote kwa siri.
21 Why do you ask me? Ask those who have heard, what things I said to them. Behold, they know what I have said.
Kwa nini waniuliza mimi? Waulize wale waliosikia nini niliwaambia. Wao wanajua nilivyosema.”
22 When he had spoken thus, one of the attendants, who was standing by, struck Jesus with his open hand, saying: Do you answer the chief priest thus?
Alipokwisha sema hayo mlinzi mmoja aliyekuwa amesimama hapo akampiga kofi akisema, “Je, ndivyo unavyomjibu Kuhani Mkuu?”
23 Jesus answered him: If I have spoken evil, testify of the evil; but if well, why do you strike me?
Yesu akamjibu, “Kama nimesema vibaya, onyesha huo ubaya; lakini ikiwa nimesema vema, mbona wanipiga?”
24 Then Annas sent him bound to Caiaphas the chief priest.
Basi, Anasi akampeleka Yesu akiwa amefungwa, kwa Kuhani Mkuu Kayafa.
25 And Simon Peter was standing and warming himself. Then they said to him: Are not you also one of his disciples? He denied, and said: I am not.
Petro alikuwa hapo akiota moto. Basi, wakamwuliza, “Je, nawe pia si mmoja wa wanafunzi wake?” Yeye akakana na kusema, “Si mimi!”
26 One of the servants of the chief priest, who was a kinsman of him whose ear Peter had cut off, said: Did I not see you in the garden with him?
Mmoja wa watumishi wa Kuhani Mkuu, jamaa wa yule aliyekatwa sikio na Petro, akamwuliza, “Je, mimi sikukuona wewe bustanini pamoja naye?”
27 Then Peter denied again. And immediately the cock crew.
Petro akakana tena; mara jogoo akawika.
28 Then they led Jesus from Caiaphas to the governor’s palace. It was the morning hour. And, in order that they might not be denied, but that they might eat the passover, they did not go into the governor’s palace.
Basi, walimchukua Yesu kutoka kwa Kayafa, wakampeleka ikulu. Ilikuwa alfajiri, nao ili waweze kula Pasaka, hawakuingia ndani ya ikulu wasije wakatiwa najisi.
29 Then Pilate came out to them, and said: What accusation do you bring against this man?
Kwa hiyo, Pilato aliwaendea nje, akasema, “Mna mashtaka gani juu ya mtu huyu?”
30 They answered and said to him: If this man were not an evil-doer, we would not have delivered him to you.
Wakamjibu, “Kama huyu hangalikuwa mwovu hatungalimleta kwako.”
31 Then Pilate said to them: Take him yourselves, and judge him according to your law. Then the Jews said to him: It is not lawful for us to put any one to death;
Pilato akawaambia, “Haya, mchukueni ninyi wenyewe, mkamhukumu kufuatana na Sheria yenu.” Wayahudi wakamjibu, “Sisi hatuna mamlaka ya kumwua mtu yeyote.”
32 that the word of Jesus might be fulfilled, which he spoke, signifying by what death he was about to die.
(Ilifanyika hivyo yapate kutimia maneno aliyosema Yesu kuonyesha atakufa kifo gani.)
33 Then Pilate again entered the governor’s palace, and called Jesus, and said to him: Are you the king of the Jews?
Pilato akaingia tena ndani ya ikulu, akamwita Yesu na kumwuliza: “Ati wewe ndiye Mfalme wa Wayahudi?”
34 Jesus answered him: Do you say this of yourself, or did others speak to you of me?
Yesu akamjibu, “Je, hayo ni maneno yako au wengine wamekwambia habari zangu?”
35 Pilate answered: Am I a Jew? Your own nation, and the chief priests have delivered you to me; what have you done?
Pilato akamjibu, “Je, ni Myahudi mimi? Taifa lako na makuhani wamekuleta kwangu. Umefanya nini?”
36 Jesus answered: My kingdom is not of this world; if my kingdom were of this world, then would my servants fight, that I might not be delivered up to the Jews. But now my kingdom is not hence.
Yesu akamjibu, “Ufalme wangu si wa ulimwengu huu. Kama ufalme wangu ungekuwa wa ulimwengu huu watumishi wangu wangenipigania nisitiwe mikononi mwa Wayahudi. Lakini sasa ufalme wangu si wa hapa.”
37 Then Pilate said to him: You are a king, then? Jesus answered; You say that I am a king. For this purpose was I born, and for this purpose I came into the world, that I might testify to the truth. Every one that is of the truth, hears my voice.
Hapo Pilato akamwambia, “Basi, wewe ni Mfalme?” Yesu akajibu, “Wewe umesema kwamba mimi ni Mfalme. Mimi nimezaliwa kwa ajili hiyo; na kwa ajili hiyo nimekuja ulimwenguni kuwaambia watu juu ya ukweli. Kila mtu wa ukweli hunisikiliza.”
38 Pilate said to him: What is truth? And when he had said this, he again came out to the Jews, and said to them: I find no fault in him.
Pilato akamwambia, “Ukweli ni kitu gani?” Pilato alipokwisha sema hayo, aliwaendea tena Wayahudi nje, akawaambia, “Mimi sioni hatia yoyote kwake.
39 But you have a custom, that I release to you one during the passover. Are you willing, then, that I should release to you the king of the Jews?
Lakini, mnayo desturi kwamba mimi niwafungulie mfungwa mmoja wakati wa Pasaka. Basi, mwataka niwafungulieni Mfalme wa Wayahudi?”
40 They all, then, cried out, saying: Not this man, but Barabbas. Now Barabbas was a robber.
Hapo wakapiga kelele: “La! Si huyu ila Baraba!” Naye Baraba alikuwa mnyang'anyi.

< John 18 >