< Exodus 30 >
1 And thou shalt make an altar to burn incense upon: of acacia wood shalt thou make it.
“Tengeneza madhabahu kwa mbao za mshita kwa ajili ya kufukizia uvumba.
2 A cubit shall be the length thereof, and a cubit the breadth thereof; foursquare shall it be; and two cubits shall be the height thereof: the horns thereof shall be of one piece with it.
Madhabahu hayo yawe mraba, urefu na upana wake dhiraa moja, na kimo cha dhiraa mbili, nazo pembe zake zitakuwa kitu kimoja nayo.
3 And thou shalt overlay it with pure gold, the top thereof, and the sides thereof round about, and the horns thereof; and thou shalt make unto it a crown of gold round about.
Funika hayo madhabahu juu na pande zote na pia pembe zake kwa dhahabu safi, na uifanyizie ukingo wa dhahabu kuizunguka.
4 And two golden rings shalt thou make for it under the crown thereof; upon the two ribs thereof, upon the two sides of it shalt thou make them; and they shall be for places for staves wherewith to bear it.
Tengeneza pete mbili za dhahabu kwa ajili ya madhabahu chini ya huo ukingo, ziwe mbili kila upande, za kushikilia hiyo mipiko itumikayo kuibebea madhabahu.
5 And thou shalt make the staves of acacia wood, and overlay them with gold.
Tengeneza mipiko kwa miti ya mshita na uifunike kwa dhahabu.
6 And thou shalt put it before the veil that is by the ark of the testimony, before the mercy-seat that is over the testimony, where I will meet with thee.
Weka hayo madhabahu mbele ya lile pazia lililo mbele ya Sanduku la Ushuhuda, lililo mbele ya kiti cha rehema kilicho juu ya Sanduku la Ushuhuda, mahali ambapo nitakutana nawe.
7 And Aaron shall burn thereon incense of sweet spices: every morning, when he dresseth the lamps, he shall burn it.
“Itampasa Aroni kufukiza uvumba wenye harufu nzuri juu ya madhabahu kila siku asubuhi wakati anapowasha zile taa.
8 And when Aaron lighteth the lamps at even, he shall burn it, a perpetual incense before Jehovah throughout your generations.
Itampasa afukize uvumba tena wakati anapowasha taa wakati wa machweo ili uvumba ufukizwe daima mbele za Bwana kwa vizazi vijavyo.
9 Ye shall offer no strange incense thereon, nor burnt-offering, nor meal-offering; and ye shall pour no drink-offering thereon.
Usifukize uvumba mwingine wowote juu ya madhabahu haya au sadaka nyingine yoyote ya kuteketezwa wala sadaka ya nafaka, wala usimimine sadaka ya kinywaji juu yake.
10 And Aaron shall make atonement upon the horns of it once in the year; with the blood of the sin-offering of atonement once in the year shall he make atonement for it throughout your generations: it is most holy unto Jehovah.
Mara moja kwa mwaka Aroni atafanya upatanisho juu ya pembe za hayo madhabahu. Upatanisho huu wa mwaka lazima ufanywe kwa damu ya sadaka ya upatanisho kwa ajili ya dhambi kwa vizazi vijavyo. Ni takatifu sana kwa Bwana.”
11 And Jehovah spake unto Moses, saying,
Naye Bwana akamwambia Mose,
12 When thou takest the sum of the children of Israel, according to those that are numbered of them, then shall they give every man a ransom for his soul unto Jehovah, when thou numberest them; that there be no plague among them, when thou numberest them.
“Utakapowahesabu Waisraeli, kila mmoja lazima alipe kwa Bwana fidia kwa ajili ya nafsi yake wakati wa kuhesabiwa kwake. Ndipo hakutakuwa na pigo juu yao unapowahesabu.
13 This they shall give, every one that passeth over unto them that are numbered, half a shekel after the shekel of the sanctuary; (the shekel is twenty gerahs), half a shekel for an offering to Jehovah.
Kila mmoja anayekwenda upande wa wale waliokwisha hesabiwa atatoa nusu shekeli, kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, ambayo ina uzito wa gera ishirini. Hii nusu shekeli ni sadaka kwa Bwana.
14 Every one that passeth over unto them that are numbered, from twenty years old and upward, shall give the offering of Jehovah.
Wote wale wanaovuka, wenye umri wa miaka ishirini au zaidi, watatoa sadaka kwa Bwana.
15 The rich shall not give more, and the poor shall not give less, than the half shekel, when they give the offering of Jehovah, to make atonement for your souls.
Matajiri hawatalipa zaidi ya nusu shekeli, nao maskini hawatatoa pungufu wakati mnatoa sadaka kwa Bwana kwa kufanya upatanisho wa nafsi zenu.
16 And thou shalt take the atonement money from the children of Israel, and shalt appoint it for the service of the tent of meeting; that it may be a memorial for the children of Israel before Jehovah, to make atonement for your souls.
Utapokea fedha ya upatanisho kutoka kwa Waisraeli na uzitumie kwa ajili ya huduma ya Hema la Kukutania. Itakuwa ni ukumbusho kwa Waisraeli mbele za Bwana kufanya upatanisho kwa ajili ya nafsi zenu.”
17 And Jehovah spake unto Moses, saying,
Kisha Bwana akamwambia Mose,
18 Thou shalt also make a laver of brass, and the base thereof of brass, whereat to wash. And thou shalt put it between the tent of meeting and the altar, and thou shalt put water therein.
“Tengeneza sinia la shaba lenye kitako cha shaba kwa ajili ya kunawia. Liweke kati ya Hema la Kukutania na madhabahu, kisha uweke maji ndani yake.
19 And Aaron and his sons shall wash their hands and their feet thereat:
Aroni na wanawe watanawa mikono na miguu yao kwa maji yatokayo katika hilo sinia.
20 when they go into the tent of meeting, they shall wash with water, that they die not; or when they come near to the altar to minister, to burn an offering made by fire unto Jehovah.
Wakati wowote wanapoingia katika Hema la Kukutania, watanawa kwa maji ili kwamba wasije wakafa. Pia, wanapokaribia madhabahu ili kuhudumu kwa kuleta sadaka zilizotolewa kwa Bwana kwa moto,
21 So they shall wash their hands and their feet, that they die not: and it shall be a statute for ever to them, even to him and to his seed throughout their generations.
watanawa mikono na miguu yao ili kwamba wasije wakafa. Hii itakuwa ni amri ya kudumu kwa ajili ya Aroni na wazao wake kwa vizazi vijavyo.”
22 Moreover Jehovah spake unto Moses, saying,
Kisha Bwana akamwambia Mose,
23 Take thou also unto thee the chief spices: of flowing myrrh five hundred [shekels], and of sweet cinnamon half so much, even two hundred and fifty, and of sweet calamus two hundred and fifty,
“Chukua vikolezi bora vifuatavyo: shekeli 500 za manemane ya maji, shekeli 250 za mdalasini wenye harufu nzuri, shekeli 250 za miwa yenye harufu nzuri,
24 and of cassia five hundred, after the shekel of the sanctuary, and of olive oil a hin;
shekeli 500 za aina nyingine ya mdalasini, vyote kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, pia hini ya mafuta ya zeituni.
25 and thou shalt make it a holy anointing oil, a perfume compounded after the art of the perfumer: it shall be a holy anointing oil.
Vitengeneze vikolezi hivi kuwa mafuta matakatifu ya upako yenye harufu nzuri, kazi ya mtengeneza manukato. Yatakuwa mafuta matakatifu ya upako.
26 And thou shalt anoint therewith the tent of meeting, and the ark of the testimony,
Kisha yatumie kupaka hilo Hema la Kukutania, Sanduku la Ushuhuda,
27 and the table and all the vessels thereof, and the candlestick and the vessels thereof, and the altar of incense,
meza na vifaa vyake vyote, kinara cha taa na vifaa vyake vyote, madhabahu ya kufukizia uvumba,
28 and the altar of burnt-offering with all the vessels thereof, and the laver and the base thereof.
madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa na vyombo vyake vyote na sinia pamoja na kitako chake.
29 And thou shalt sanctify them, that they may be most holy: whatsoever toucheth them shall be holy.
Utaviweka wakfu ili viwe vitakatifu sana na kila kitakachoigusa kitakuwa kitakatifu.
30 And thou shalt anoint Aaron and his sons, and sanctify them, that they may minister unto me in the priest’s office.
“Mtie Aroni na wanawe mafuta na uwaweke wakfu ili waweze kunitumikia katika kazi ya ukuhani.
31 And thou shalt speak unto the children of Israel, saying, This shall be a holy anointing oil unto me throughout your generations.
Waambie Waisraeli, ‘Haya yatakuwa mafuta matakatifu yangu ya upako kwa vizazi vijavyo.
32 Upon the flesh of man shall it not be poured, neither shall ye make any like it, according to the composition thereof: it is holy, [and] it shall be holy unto you.
Usiyamimine juu ya miili ya wanadamu wala usitengeneze mafuta ya aina nyingine kwa utaratibu huu. Ni mafuta matakatifu na ni lazima myaone kuwa ni matakatifu.
33 Whosoever compoundeth any like it, or whosoever putteth any of it upon a stranger, he shall be cut off from his people.
Mtu yeyote atakayetengeneza manukato kama hayo na yeyote atakayeyamimina juu ya mtu yeyote ambaye si kuhani atakatiliwa mbali na watu wake.’”
34 And Jehovah said unto Moses, Take unto thee sweet spices, stacte, and onycha, and galbanum; sweet spices with pure frankincense: of each shall there be a like weight;
Kisha Bwana akamwambia Mose, “Chukua vikolezi vyenye harufu nzuri vifuatavyo: natafi, shekelethi, kelbena na uvumba safi vyote vikiwa na vipimo sawa,
35 and thou shalt make of it incense, a perfume after the art of the perfumer, seasoned with salt, pure [and] holy:
pia tengeneza mchanganyiko wa uvumba wenye harufu nzuri, kazi ya mtengeneza manukato. Utiwe chumvi ili upate kuwa safi na mtakatifu.
36 and thou shalt beat some of it very small, and put of it before the testimony in the tent of meeting, where I will meet with thee: it shall be unto you most holy.
Saga baadhi yake kuwa unga na uweke mbele ya Sanduku la Ushuhuda ndani ya Hema la Kukutania, mahali ambapo nitakutana nawe. Itakuwa takatifu sana kwenu.
37 And the incense which thou shalt make, according to the composition thereof ye shall not make for yourselves: it shall be unto thee holy for Jehovah.
Msitengeneze uvumba mwingine wowote wa namna hii kwa ajili yenu wenyewe; uoneni kuwa ni mtakatifu kwa Bwana.
38 Whosoever shall make like unto that, to smell thereof, he shall be cut off from his people.
Yeyote atakayetengeneza uvumba kama huu ili kufurahia harufu yake nzuri lazima akatiliwe mbali na watu wake.”