< Job 36 >

1 Elihu also proceeded, and said,
Elihu akaendelea kusema:
2 Allow me a little, and I will show thee. For I have yet somewhat to say on God's behalf.
“Nivumilie kidogo zaidi nami nitakuonyesha kwamba yako mengi zaidi ya kusemwa kwa ajili ya Mungu.
3 I will fetch my knowledge from afar, and will ascribe righteousness to my maker.
Ninayapata maarifa yangu kutoka mbali, nami nitamhesabia haki Muumba wangu.
4 (For truly my words are not false.) He who is perfect in knowledge is with thee.
Uwe na hakika kwamba maneno yangu si ya uongo; mmoja aliye mkamilifu katika maarifa yuko pamoja na wewe.
5 Behold, God is mighty, and does not despise. He is mighty in strength of understanding.
“Mungu ni mwenye nguvu, lakini hamdharau mwanadamu; ni mwenye nguvu, naye ni thabiti katika shauri lake.
6 He does not preserve the life of the wicked, but gives to the afflicted their right.
Hawaachi waovu waendelee kuishi, bali huwapa walioteswa haki yao.
7 He does not withdraw his eyes from the righteous, but he sets them forever with kings upon the throne, and they are exalted.
Yeye haondoi macho yake kwa wenye haki; huwaketisha penye viti vya enzi pamoja na wafalme na kuwatukuza milele.
8 And if they be bound in fetters, and be taken in the cords of afflictions,
Lakini ikiwa watu wamefungwa kwenye minyororo, wakiwa wameshikiliwa na kamba za mateso,
9 then he shows them their work, and their transgressions, that they have behaved themselves proudly.
huwaonyesha yale waliyoyatenda, kwamba wametenda dhambi kwa majivuno.
10 He also opens their ear to instruction, and commands that they return from iniquity.
Huwafanya wao kusikia maonyo, na huwaagiza kutubu uovu wao.
11 If they hearken and serve him, they shall spend their days in prosperity, and their years in pleasures.
Kama wakitii na kumtumikia, wataishi siku zao zilizobaki katika mafanikio, na miaka yao katika utoshelevu.
12 But if they do not hearken, they shall perish by the sword, and they shall die without knowledge.
Lakini wasiposikiliza, wataangamia kwa upanga, nao watakufa pasipo maarifa.
13 But those who are godless in heart lay up anger. They do not cry for help when he binds them.
“Wasiomcha Mungu moyoni mwao huficha chuki; hata anapowafunga, hawamwombi msaada.
14 They die in youth, and their life perishes among the unclean.
Wanakufa wangali vijana, miongoni mwa wanaume hanithi wa mahali pa kuabudia miungu.
15 He delivers the afflicted by their affliction, and opens their ear in oppression.
Bali wao wanaoteseka huwaokoa katika mateso yao, na kuzungumza nao katika dhiki zao.
16 Yea, he would have allured thee out of distress into a broad place, where there is no confinement, and that which is set on thy table would be full of fatness.
“Yeye anakubembeleza utoke katika mataya ya dhiki, ili kukuweka mahali palipo na nafasi mbali na kizuizi, hadi kwenye meza yako ya faraja iliyojaa vyakula vizuri.
17 But thou have fulfilled the judgment of the wicked. Judgment and justice take hold,
Lakini sasa umelemewa na hukumu kwa ajili ya uovu; hukumu na haki vimekukamata.
18 and there shall be wrath upon the impious because of the ungodliness of bribes which the unrighteous receive.
Uwe mwangalifu ili yeyote asikushawishi kwa utajiri; usipotoshwe kwa fungu kubwa la rushwa.
19 Will thy cry not avail in distress, or all the forces of strength?
Je, utajiri wako hata nguvu zako nyingi vinaweza kukusaidia usiingie kwenye dhiki?
20 Do not desire the night, when peoples are cut off in their place.
Usiutamani usiku uje, ili uwaburute watu mbali na nyumba zao.
21 Take heed. Do not turn to iniquity, for thou have fixed on this because of affliction.
Jihadhari usigeukie uovu, ambao unaupenda zaidi kuliko mateso.
22 Behold, God does loftily in his power. Who is a teacher like him?
“Mungu ametukuzwa katika nguvu zake. Ni nani aliye mwalimu kama yeye?
23 Who has enjoined him his way? Or who can say, Thou have wrought unrighteousness?
Ni nani aliyemwelekeza katika njia zake, au kumwambia, ‘Wewe umetenda yasiyo sawa’?
24 Remember that thou magnify his work, of which men have sung.
Kumbuka kuzitukuza kazi zake, ambazo watu wamezisifu katika wimbo.
25 All men have looked on it. Man beholds it afar off.
Wanadamu wote wameiona; watu wanaikazia macho kwa mbali.
26 Behold, God is great, and we do not know him. The number of his years is unsearchable.
Tazama jinsi Mungu alivyo mkuu, kupita ufahamu wetu! Hesabu ya miaka yake haitafutiki.
27 For he draws up the drops of water, which distil in rain from his vapor,
“Yeye huvuta juu matone ya maji, ayachujayo kama mvua kutoka kwenye vijito;
28 which the skies pour down and drop upon man abundantly.
mawingu huangusha chini maji yake, nayo mvua nyingi huwanyeshea wanadamu.
29 Yea, can any understand the spreadings of the clouds, the thunderings of his pavilion?
Ni nani ajuaye jinsi ayatandazavyo mawingu, jinsi angurumavyo kutoka hemani mwake.
30 Behold, he spreads his light around him, and he covers the bottom of the sea.
Tazama jinsi anavyotandaza umeme wa radi kumzunguka, naye huvifunika vilindi vya bahari.
31 For by these he judges the peoples. He gives food in abundance.
Hivi ndivyo atawalavyo mataifa, na kuwapa chakula kwa wingi.
32 He covers his hands with the lightning, and gives it a command that it strike the mark.
Huujaza mkono wake kwa umeme wa radi, na kuuagiza kulenga shabaha yake.
33 The noise of it tells concerning him. The cattle also concerning the storm that comes up.
Ngurumo zake hutangaza dhoruba inayokuja; hata mifugo hujulisha kukaribia kwake.

< Job 36 >