< Exodus 14 >
1 And Jehovah spoke to Moses, saying,
Ndipo Bwana akamwambia Mose,
2 Speak to the sons of Israel, that they turn back and encamp before Pihahiroth, between Migdol and the sea, before Baal-zephon. Ye shall encamp opposite it by the sea.
“Waambie Waisraeli wageuke nyuma na wapige kambi karibu na Pi-Hahirothi, kati ya Migdoli na bahari. Watapiga kambi kando ya bahari, mkabala na Baal-Sefoni.
3 And Pharaoh will say of the sons of Israel, They are entangled in the land; the wilderness has shut them in.
Farao atafikiri kwamba, ‘Hao Waisraeli wanatangatanga katika nchi kwa kuchanganyikiwa, nalo jangwa limewafungia.’
4 And I will harden Pharaoh's heart, and he shall follow after them, and I will get for me honor upon Pharaoh, and upon all his army, and the Egyptians shall know that I am Jehovah. And they did so.
Nami nitaufanya moyo wa Farao mgumu, naye atawafuatilia. Lakini nitajipatia utukufu kwa ajili yangu mwenyewe kupitia Farao na jeshi lake lote, nao Wamisri watajua kuwa mimi ndimi Bwana.” Kwa hiyo Waisraeli wakafanya hivyo.
5 And it was told the king of Egypt that the people were fled. And the heart of Pharaoh and of his servants was changed towards the people, and they said, What is this we have done, that we have let Israel go from serving us?
Mfalme wa Misri alipoambiwa kuwa Waisraeli wamekimbia, Farao na maafisa wake wakabadili nia zao kuhusu Waisraeli, wakasema, “Tumefanya nini? Tumewaachia Waisraeli waende zao na tumeukosa utumishi wao!”
6 And he made ready his chariot, and took his people with him.
Kwa hiyo akaandaliwa gari lake la vita, naye akaenda pamoja na jeshi lake.
7 And he took six hundred chosen chariots, and all the chariots of Egypt, and captains over all of them.
Akachukua magari bora mia sita, pamoja na magari mengine yote ya Misri, pamoja na maafisa wa magari hayo yote.
8 And Jehovah hardened the heart of Pharaoh king of Egypt, and he pursued after the sons of Israel, for the sons of Israel went out with a high hand.
Bwana akaufanya mgumu moyo wa Farao, mfalme wa Misri, kwa hiyo akawafuatia Waisraeli, waliokuwa wakiondoka Misri kwa ujasiri.
9 And the Egyptians pursued after them, all the horses and chariots of Pharaoh, and his horsemen, and his army, and overtook them encamping by the sea, beside Pihahiroth, before Baal-zephon.
Nao Wamisri, yaani farasi wote wa Farao na magari ya vita, wapanda farasi na vikosi vya askari, wakawafuatia Waisraeli, wakawakuta karibu na Pi-Hahirothi, mkabala na Baal-Sefoni walipokuwa wamepiga kambi kando ya bahari.
10 And when Pharaoh drew near, the sons of Israel lifted up their eyes, and, behold, the Egyptians were marching after them, and they were very afraid. And the sons of Israel cried out to Jehovah,
Farao alipokaribia, Waisraeli wakainua macho yao, wakawaona Wamisri wakija nyuma yao. Wakashikwa na hofu, wakamlilia Bwana.
11 and they said to Moses, Because there were no graves in Egypt, have thou taken us away to die in the wilderness? Why have thou dealt thus with us, to bring us forth out of Egypt?
Wakamwambia Mose, “Je, ni kwamba hayakuwako makaburi huko Misri hata umetuleta tufe huku jangwani? Umetufanyia nini kututoa Misri?
12 Is not this the word that we spoke to thee in Egypt, saying, Let us alone, that we may serve the Egyptians? For it were better for us to serve the Egyptians, than that we should die in the wilderness.
Hatukukuambia tulipokuwa huko Misri, tuache tuwatumikie Wamisri? Ingekuwa vyema zaidi kwetu kuwatumikia Wamisri kuliko kufa jangwani!”
13 And Moses said to the people, Fear ye not. Stand still, and see the salvation of Jehovah, which he will work for you today, for the Egyptians whom ye have seen today, ye shall see them again no more forever.
Mose akawajibu Waisraeli, “Msiogope. Simameni imara, nanyi mtauona wokovu Bwana atakaowapatia leo. Hao Wamisri mnaowaona leo kamwe hamtawaona tena.
14 Jehovah will fight for you, and ye shall keep silent.
Bwana atawapigania ninyi, nanyi mnatakiwa kutulia tu.”
15 And Jehovah said to Moses, Why do thou cry to me? Speak to the sons of Israel, that they go forward.
Ndipo Bwana akamwambia Mose, “Kwa nini wewe unanililia? Waambie Waisraeli waendelee mbele.
16 And lift thou up thy rod, and stretch out thy hand over the sea, and divide it, and the sons of Israel shall go into the midst of the sea on dry ground.
Inua fimbo yako na unyooshe mkono wako juu ya bahari ili kuyagawa maji, hivyo kwamba Waisraeli wapate kupita mahali pakavu baharini.
17 And I, behold, I will harden the hearts of the Egyptians, and they shall go in after them, and I will get for me honor upon Pharaoh, and upon all his army, upon his chariots, and upon his horsemen.
Nitaifanya mioyo ya Wamisri kuwa migumu kusudi waingie baharini wakiwafuatia. Nami nitajipatia utukufu kupitia Farao pamoja na jeshi lake lote, kupitia magari yake ya vita na wapanda farasi wake.
18 And the Egyptians shall know that I am Jehovah, when I have gotten for me honor upon Pharaoh, upon his chariots, and upon his horsemen.
Nao Wamisri watajua kwamba Mimi ndimi Bwana nitakapojipatia utukufu kupitia Farao, magari yake ya vita na wapanda farasi wake.”
19 And the agent of God, who went before the camp of Israel, moved and went behind them, and the pillar of cloud moved from before them, and stood behind them.
Ndipo malaika wa Mungu, aliyekuwa akisafiri mbele ya jeshi la Israeli, akaondoka akakaa nyuma yao. Pia ile nguzo ya wingu ikaondoka hapo mbele yao na kusimama nyuma,
20 And it came between the camp of Egypt and the camp of Israel. And the cloud and the darkness was there, yet it gave light by night. And the one did not come near the other all the night.
ikakaa kati ya majeshi ya Misri na Israeli. Usiku kucha wingu likaleta giza upande mmoja na nuru kwa upande mwingine, kwa hiyo hakuna aliyemkaribia mwenzake usiku kucha.
21 And Moses stretched out his hand over the sea, and Jehovah caused the sea to go back by a strong east wind all the night, and made the sea dry land, and the waters were divided.
Ndipo Mose akanyoosha mkono wake juu ya bahari, naye Bwana akayasukuma maji ya bahari nyuma kwa upepo mkali wa mashariki usiku ule wote na kupafanya nchi kavu. Maji yakagawanyika,
22 And the sons of Israel went into the midst of the sea upon the dry ground, and the waters were a wall to them on their right hand, and on their left.
nao Waisraeli wakapita baharini mahali pakavu, maji yakiwa ukuta upande wao wa kuume na upande wao wa kushoto.
23 And the Egyptians pursued, and went in after them into the midst of the sea, all Pharaoh's horses, his chariots, and his horsemen.
Wamisri wakawafuatia ndani ya bahari, pamoja na farasi wote wa Farao, magari ya vita na wapanda farasi.
24 And it came to pass in the morning watch, that Jehovah looked forth upon the army of the Egyptians through the pillar of fire and of cloud, and troubled the army of the Egyptians.
Karibia mapambazuko, Bwana akaliangalia jeshi la Wamisri kutoka ile nguzo ya moto na ya wingu, akalifadhaisha.
25 And he took off their chariot wheels, and they drove them with difficulty, so that the Egyptians said, Let us flee from the face of Israel, for Jehovah fights for them against the Egyptians.
Mungu akayaondoa magurudumu ya magari yao, kwa hivyo wakayaendesha kwa shida. Nao Wamisri wakasema, “Tuachane na Waisraeli! Bwana anawapigania dhidi ya Misri.”
26 And Jehovah said to Moses, Stretch out thy hand over the sea, that the waters may come again upon the Egyptians, upon their chariots, and upon their horsemen.
Ndipo Bwana akamwambia Mose, “Nyoosha mkono wako juu ya bahari ili maji yarudiane yawafunike Wamisri, magari yao ya vita na wapanda farasi wao.”
27 And Moses stretched forth his hand over the sea, and the sea returned to its strength when the morning appeared, and the Egyptians fled against it, and Jehovah overthrew the Egyptians in the midst of the sea.
Mose akanyoosha mkono wake juu ya bahari, wakati wa mapambazuko bahari ikarudiana na kuwa kama kawaida. Wamisri wakajaribu kuyakimbia maji, lakini Bwana akawasukumia ndani ya bahari.
28 And the waters returned, and covered the chariots, and the horsemen, even all the army of Pharaoh who went in after them into the sea, there remained not so much as one of them.
Maji yakarudiana na kuyafunika magari ya vita na wapanda farasi pamoja na jeshi lote la Farao lililokuwa limewafuata Waisraeli ndani ya bahari. Hakuna hata mmoja wao aliyenusurika.
29 But the sons of Israel walked upon dry land in the midst of the sea, and the waters were a wall to them on their right hand, and on their left.
Lakini Waisraeli wakapita baharini mahali pakavu, ukiwepo ukuta wa maji upande wao wa kuume na upande wao wa kushoto.
30 Thus Jehovah saved Israel that day out of the hand of the Egyptians, and Israel saw the Egyptians dead upon the sea-shore.
Siku ile Bwana akawaokoa Waisraeli kutoka mikononi mwa Wamisri, nao Waisraeli wakawaona Wamisri wamelala ufuoni mwa bahari wakiwa wamekufa.
31 And Israel saw the great work which Jehovah did upon the Egyptians. And the people feared Jehovah, and they believed in Jehovah, and in his servant Moses.
Basi Waisraeli walipoona uwezo mkubwa Bwana aliodhihirisha dhidi ya Wamisri, watu wakamwogopa Bwana na wakaweka tumaini lao kwake na kwa Mose mtumishi wake.