< Openbaring 15 >
1 Toen zag ik een ander teken in de hemel, groot en wonderbaar: Zeven engelen met zeven plagen, de allerzwaarste; want hiermee heeft Gods toorn zijn toppunt bereikt.
Tena nikaona ishara nyingine mbinguni, kubwa na yenye kushangaza; Kulikuwa na malaika saba wenye mapigo saba, ambayo yalikuwa mapigo ya mwisho (katika hayo hasira ya Mungu ilikuwa imetimilika).
2 Ook zag ik een glazen zee, doorstreept als met vuur; en de overwinnaars van het Beest, van zijn beeld en het getal van zijn naam, stonden boven op de glazen zee, dragend de citers van God.
Niliona kile kilichotokea kuwa bahari ya bilauri iliyochanganywa na moto, na ikasimama pembeni mwa bahari ambapo wale waliokuwa washindi dhidi ya mnyama na sanamu yake, na juu ya namba inayowakilisha jina lake. Walikuwa wameshikilia vinubi walivyopewa na Mungu.
3 En ze zongen het lied van Moses, den dienaar van God, en het lied van het Lam; en ze zeiden: Groot en wonderbaar zijn uw werken, O Heer en almachtige God! Rechtvaardig en waarachtig zijn uw wegen, O Koning der volken!
Walikuwa wakiimba wimbo wa Musa, mtumishi wa Mungu, na wimbo wa Mwana Kondoo: “Kazi zako ni kubwa na zenye kushangaza, Bwana Mungu, utawalaye vyote. Mwaminifu na njia zako ni za kweli, Mfalme wa mataifa.
4 Wie zou U niet vrezen, o Heer, uw Naam niet verheerlijken, Want Gij alleen zijt heilig; Alle volken zullen U komen aanbidden, Want uw oordelen worden thans geopenbaard.
Nani atashindwa kukuhofu wewe Bwana na kulitukuza jina lako? Kwa kuwa wewe peke yako ni mtakatifu. Mataifa yote yatakuja na kukuabudu mbele zako kwa sababu u mwema na matendo yako yamejulikana.”
5 Na dit alles bleef ik nog toezien. Daar ging de hemelse tempel van de openbaringstent open!
Baada ya mambo hayo nilitazama, na sehemu takatifu sana, ambapo palikuwa na hema ya ushuhuda, iliyofungukia mbinguni.
6 En de zeven engelen met de zeven plagen traden de tempel uit, gekleed in rein, schitterend lijnwaad, de borsten met gouden gordels omgord.
Kutoka mahali patakatifu sana wakaja malaika saba wenye mapigo saba, wamevaa mavazi safi, kitani yenye kung'aa na mshipi wa dhahabu kuzunguka vifua vyao.
7 Eén van de vier Dieren gaf aan de zeven engelen zeven gouden schalen, vol van de gramschap van God, van den Levende in de eeuwen der eeuwen. (aiōn )
Mmoja wa wale wenye uhai wanne akatoa kwa malaika saba mabakuli saba ya dhahabu yaliyojaa ghadhabu ya Mungu mwenye kuishi milele na milele. (aiōn )
8 En de tempel werd vervuld met rook door de heerlijkheid Gods en zijn macht; en niemand kon de tempel binnengaan, vóórdat de zeven plagen der zeven engelen waren voltrokken.
Mahali patakatifu sana kulijawa moshi kutoka kwenye utukufu wa Mungu na kutoka kwenye uwezo wake. Hakuna hata mmoja aliyeweza kuingia mpaka mapigo saba ya malaika saba yalipokamilika.